Nilikuwa Nina shida Fulani, itabidi nikamuone shekhe ndio anaweza kunisaidia, ila baada ya kunisomea Dua , akanipa hili karatasi kama niweke kwenye wallet
Naomba tasfiri yake wakuu, isije ikawa nimepewa jini kijanja, maana napata hela, sijui zinapo ishia
Juu ya karatasi kaandika surat nasr (idhajaa), kushoto ni kamtaja Allah (the almighty mara tatu) , chini ni dua na katika kibox ni herufi tu za kiarabu , ila kuna shida mahali 👇👇👇
"Nilikuwa Nina shida Fulani, itabidi nikamuone shekhe
ndio anaweza kunisaidia........."
1. Tengua hiyo kauli hapo juu hakuna shaikh anaweza kukusaidia ukiwa na shida si shaikh tu hakuna nabii wala mtume (hapa naongelea wakina Nuhu(alayhi salaam), ibrahim(alyhi salaam) , isa(alayhi salaam) na hata mtume muhammad (swalallahu alayhi wasalam) anayeweza kukusaidia ukiwa na shida anayeweza hayo ni ALLAH (the almighty) PEKEEE HAKUNA MWENGINE FULL STOP
2. Watu tunapokosea ni kwamba hatufanyi ibada , wala kujituma kukamilisha ibada za faradhi na nyenginezo kwa wakati na kujikurubisha kwa Muumba wetu halafu tunataraji tukipata shida na matatizo ndo tunamkumbuka 😂 utaenda kwa mashaikh , utaenda kwa waganga utamaliza kila kitu kumbe tatizo ni WEWE.
3. SISAPOTI KWENDA KWA SHAIKH ILI KUTATULIWA SHIDA ZAKO , MAOMBI YAKO KWENYE SIJDA YANA NGUVU KULIKO KITU CHOCHOTE HIVYO KAMA UNA SHIDA JUA WEWE NDO UNA NAFASI KUBWA YA KUSIKILIZWA NA MUUMBA KULIKO MWENGINE IBADA IBADA IBADA FULLSTOP.
4. KWA MSAADA WA HARAKA CHUKIA KIBERITI CHOMA HIYO TAWIZ , yaani unaandikiwa dua kwenye karatasi kwa kutumia zafarani halafu anakwambia ubebe nenda kachome hiyo kitu hakuna mtu anaweza kukusaidi kwa kukuandikia dua chache kwenye karatsi shida ipo kwako , kwa msaada kachukue wudhu swali na kila sijda lalamika kweli kweli mpaka ujibiwe inshaallah.
N.B
kuna watu ni waganga ila wanatumia kivuli cha dini kujitia u shaikh chungeni mtabebeshwa majini