Hiki kikohozi kisichoeleweka kimeikumba familia yangu tu, Au ni UPEPO?

Hiki kikohozi kisichoeleweka kimeikumba familia yangu tu, Au ni UPEPO?

Hivi yale ma Covidol sijui NImricuf sijui nini bado yapo huko Bongo? kuna jamaa waliaminishwa yanatibu mauviko 19
 
Kuna upepo wa Mafua na kikohozi unasumbua sana kuanzia January, February na sasa March! Familia nzima wanakohoa, kuanzia watoto wadogo, wanafunzi na hata wakubwa!

Mara nyingi navyojua kikohozi huwa ni cha mda mfupi kinapoa baada ya dawa! Lakini hiki cha awamu hii kinapungua tu lakini hakiishi wala hakisikii dawa za hospital wa mitishamba!

Familia nzima ni mwendo wa Koh koh koh koh! Hata haieleweki ni hapa tu au kuna upepo mbaya?

Mwenye uelewa juu ya hili atuambie! Hospital kila tukienda vipimo vyote wanasema ni mafua tu yakawaida!
Chukua limao, lioshe vizuri bila kumenya, katakata kisha chukua tangawizi ioshe ukatekate vipande vidogovidogo. Chemsha maji kisha saga kwa Brenda huku ukitumia hayo maji ya moto. Chuja kisha kunywa glasi moja asubuhi na moja jioni. Kumbuka usiiweke kwenye friji kwasababu sio rahisi kuharibika ata wiki. Kisha njoo na mrejesho hapa. Kumbuka usitoe mbegu za limao wala maganda yake, vyote saga. Ni chungu sana ila ndio dawa kwa sasa
 
Back
Top Bottom