Hiki Kipupwe ni Komesha! Kwa majobless ni kipindi kigumu Sana

Haha! Kipupwe kweli kinatunyanyasa kila kona—pua kugandamana ni dalili tu ya hali halisi ilivyo baridi na ngumu. Kama “makamu rais wa jobless,” ningependekeza:

1. Kuungana kwenye miradi midogo midogo ya kujikomboa kiuchumi.
2. Kushirikiana kwa taarifa kuhusu fursa—hata ndogo ndogo.
3. Kuwahamasisha wasakatonge wasikate tamaa, msimu utapita lakini juhudi ziendelee.

Na kwa pua zilizogandamana—vicks na mafuta ya nazi yanaweza kusaidia, lakini kazi ya kweli ni kukabiliana na hali ya uchumi baridi.
Hamjambo!

Sijajua! Wala sio mtaalamu wa masuala ya hali ya hewa.
Ila kwa elimu ndogo ya kitaaolojia ninaweza kusema hakuna kipindi kigumu na kibaya kwa Majobless na watu wasio na hela kama msimu huu wa kipupwe ambapo baridi yenye kukera na upepo wenye kusudi la kupausha vinashirikiana kuwaadhiri washikadau!

Sijajua wakazi wa Dodoma, Singida, Kahama, Mafinga, Makambako, Mbeya, Makanya kwetu na Same yote, ambapo niliwahi kukaa msimu huu wa kipupwe. Hakika inakuwa adhabu inshadida!

Kipindi cha Kipupwe kama sasa unatakiwa upake mafuta maalum yatakayotunza unyevunyevu kwenye ngozi. Mafuta ya ngozi yenye kuifanya ngozi iwe salama na inawiri.
Ajabu ni kuwa mafuta ya ngozi ya aina hiyo ni gharama Sana. Kama huna pesa kupauka hakuepukiki!

Picha linaanza ngozi inakakamaa, kisha inapauka. Ukishindwa kutatua mpauko kinachofuata ni Mfubao. Unafubaa.
Hutamaniki tena. Unakuwa kinyang'unya, kinyago cha mpabure.

Nywele zinapoteza rutba. Midomo inasinyaa kisha mipasuko midogomidogo inajitokeza. Unyafunzi sio unyafunzi.

Kingine kipindi cha Kipupwe ni kigumu kwa ambao hawana usafiri. Wasaga ardhi, wakung'uta vumbi, haishauriwi kutembea nje Kwa umbali wa nusu Kilometa au kutembea kwa zaidi ya dakika kumi vumbi la kipupwe likikupiga. Lazima uchakae.

Sasa kwa kazi zetu za nje hizi, kutembeza vitu, kuuza vitu sokoni, yaani KAZI za nje tupo kwenye Risk-list ya kupata athari za kipupwe.

Shida ya kipupwe ni pua kugandamaa, nostrils ndani ya pua zinakauka, kisha panakuwa na mgando unaofanya pua zikakamae na ziume. Unajua nostril zikikauka kinachofuata ni magonjwa kama mafua au kikohozi.

Rais wa Majobless Intelligent businessman Sijui kama unampango wowote kusaidia jobless kwa kipindi hiki kigumu.

Rais wa Wasakatonge na walianamungu sijui umejipangaje kusaidia hawa wavujajasho katika msimu huu.

Kwa kweli mimi sijui!

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa Sasa Dar es salaam
 
Kurahisisha mchakato wa passport vijana wajilipue
 
Mtaani kwangu kwa mangi majobless wanakanyagana kutafuta video.
Wapo wanapkunywa bia, visungura, banging na ugoro. Wengine vyote
Hakika wamekata tamaa
 
Back
Top Bottom