Hiki ndicho kinatakiwa kuwa kiwango cha chini kabisa cha imani ya mtu ambaye bado anaingia nyumba za Ibada

Hiki ndicho kinatakiwa kuwa kiwango cha chini kabisa cha imani ya mtu ambaye bado anaingia nyumba za Ibada

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Kutoogopa au kuzungumzia mapepo, wachawi, majini kwa aina zake.

Cha ajabu, mapambano dhidi ya haya madubwana ndio imegeuzwa kuwa kigezo cha ubora wa imani.

Kama wasiamini Mungu (atheists) kwa aina zao wanaonyesha ujasiri wa kuyapuuza na hata kutoyazungumzia au kuyapa promo wanaomcha Mungu na kuamini uwezo wake hawapaswi kabisa kuyakubwisha kwa namna yoyote ile.

Wanaomuamini Mungu wanatakiwa kuogopwa na waganga, watumishi feki, wachawi, majini kwa aina zao. Kama unayaogopa imani yako inazidiwa hata na wasioamini kabisa uwepo wa Mungu.

Usiingie mahala ambapo hivyo vitu na kazi za yule bwana mdogo ibrisi anasifiwa na kupewa airtime. Hapo panaua imani yako.

Ni hayo tu

Mtumishi Matunduizi
 
Imani ya mtu binafsi kwa kuangalia matendo yake yanayokubalika na jamii ni muhimu , imani ya wengi ndio hawa ni kiongozi wa dini ila anafanya mambo ya hovyo .

Imani ya leo imebaki kama cheo ila sio matendo ya siri zaidi.
 
Unashangaa kila baada sekunde kadhaa mtumishi anamtaja shetani, uchawi, vifungo
Shetani anatajwa kuliko ata Mungu.
Kazi za shetani zinapewa promo kuliko matendo ya Mungu
Nyumba ya ibada ya namna hii siendi.
 
Nina muda mrefu sana sijaingia nyumba ya ibada, zaidi ya kujisalia tu nyumbani.
ukifa hakuna rangi utaacha kuona toka kwa viongozi wa imani yako ulikokuwa unaenda kusali. Utaipa shida familia yako wasijue wakuziki kwa taratibu za imani ipi
 
ukifa hakuna rangi utaacha kuona toka kwa viongozi wa imani yako ulikokuwa unaenda kusali. Utaipa shida familia yako wasijue wakuziki kwa taratibu za imani ipi
Wangekuwa wanalipia gharama za matibabu wakati najipigania uhai ingekuwa vizuri zaidi, kuliko kuja kusoma maandishi tu siku ya maziko na kuondoka na sadaka.​
 
Walokole ndo wanaongoza kwa uoga mpaka huwa najiuliza nini maana ya kuwa Mtumishi wa Mungu, unakuta mtu anaogopa wachawi, kidogo unasikia utalogwa au amelogwa. Kanisa wanaogopa wachawi na wale wenye Imani nusu nusu nao wanaogopa wachawi though Hawa sio sana

Nimeita walokole najua sio wote ila hata haya makanisa ya manabii ambao wapo busy kwenye social media nao ni walokole kama wanavyojiita (ni kwa muktadha visije mkanipopoa mawe)
 
kwanza fahamu dhana ya ulokole ndio uje na hoja yako
 
Back
Top Bottom