Hiki ndiyo kitu bora kabisa unachopaswa kufanya wakati huu wa vita ya Urusi na Ukraine

Makirita Amani

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2012
Posts
1,915
Reaction score
3,422
Rafiki yangu mpendwa,

Chombo kikubwa cha habari nchini China (Horizon News), kilichapa kwa makosa maelekezo yaliyokuwa yametolewa kwa wahariri wake.

Pamoja na mengine mengi, maelekezo hayo yaliwataka wahariri kuhakikisha hawachapishi habari yoyote inayoichafua Urusi au kusiria upande wa magharibi.

Pia walisisitizwa kudhibiti maoni yanayowekwa na wasomaji ili kuhakikisha hakuna chochote kinachoharibu upande wao kinawekwa.

Rafiki, huu ni upande mmoja wa mashariki kwenye vita inayoendelea kati ya Urusi na Ukraine.

Kwa upande wa magharibi nao wana mikakati yao katika kuruhusu habari gani zisambae ili kutengeneza picha wanayotaka wao.

images.jpeg-117.jpg

Hivyo basi, kitu bora kabisa unachoweza kufanya wakati huu wa vita ni kutokufuatilia habari yoyote.

Ndiyo, usijisumbue kabisa kufuatilia habari wakati huu wa vita.

Hiyo ni kwa sababu sehemu kubwa ya habari unazopewa siyo ukweli, bali ni propaganda zilizoandaliwa kwa makusudi maalumu.

Sehemu kubwa ya vita hii ipo kwenye propaganda zaidi.

Kila upande ukipambana kuonyesha kwamba upo sahihi kwenye hii vita.

Kama haupo eneo la tukio, ni vigumu sana ukaweza kujua hali halisi ya vita.

Watu wametumia mpaka picha za zamani kusambaza propaganda zao kuhusu vita hii.

Hivyo basi rafiki yangu, ili kupata utulivu wa akili na kupunguza msongo usio na maana, acha kufuatilia habari za hii vita.

Sisemi kwamba hakuna vita au kwamba haina madhara.

Nina hakika kuna watu wasio na hatia ambao wanakufa kila siku kutokana na vita hii.

Nina hakika familia zinavurugika, miji kubomolewa na mengine mabaya yanaendelea.

Lakini huwezi kusaidia lolote kwenye hayo kwa kufuatilia habari kwa masaa 24 kutaka kujua kila kinachoendelea kwenye hii vita.

Kwa bahati mbaya sana hii ndiyo vita kubwa inayotokea kwenye zama hizi za mitandao ya kijamii, zama ambazo watu wamekuwa na uraibu mkubwa kwenye mitandao hiyo.

Hivyo vita ya propaganda imeshamiri kwenye mitandao ya kijamii.

Kila upande ukitumia kila mbinu kusambaza propaganda zake ili kupata huruma kutoka kwa wengi.

Usikubali kutumiwa kwa namna hiyo, wewe achana na habari hizo za vita, maana hakuna unachoweza kufanya kuathiri vita hiyo.

Ufanye nini sasa kama hufuatilii habari wakati huu wa vita?

Jibu ni moja, tumia muda huo kujifunza na kuboresha kazi au biashara unayofanya.
Hicho ndiyo kitu pekee kilicho ndani ya uwezo wako wa kuathiri.

Na kama kazi yako inahusu kufuatilia hizo habari za vita, basi jifunze namna ya kupata habari halisi na siyo propaganda.

Wakati huu wa vita uraibu wa habari na mitandao ya kijamii umekuwa mara dufu.

Hivyo ni wakati mzuri sana kwako kusoma kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI ili uweze kuondokana na mitego ya kipropaganda uliyotegewa ili kunasa huruma yako.

Jipatie nakala yako ya kitabu hiki leo kwa kuwasiliana na 0752 977 170 ili usitumike kwa manufaa ya watu wengine.

epuka-utumwa-frontcover-1.jpg

Utulivu wako ni muhimu sana katika safari ya mafanikio kwenye maisha yako.

Usiuvuruge kwa kufuatilia vitu ambavyo huna namna ya kuviathiri.

Peleka umakini wako kwenye yale unayoweza kuathiri.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani.
 
Sijaona kipya maana hata west nao wanafanya hili hili. Watu wanalalamika huko linkedin na twitter zikipandishwa video au picha zinazowaonyesha wanajeshi au raia wa Ukraine wakiwazuia wahindi, waafrika, waarabu kupanda usafiri au kuvuka mpaka zinaondolewa mara moja.

Hivyo kila pande inatoa picha inayotaka.
 
Unachoeleza ki kitu bora sana.

Nakumbuka corona ilipoanza niliona sasa ni mwisho wa dunia na nikaona mimi na familia yangu tukiwa na hofu mno.

Baada ya Mh Rais Magufuli Mungu Mrehemu na kumponya nafsi yake alitueleza Mambo mazuri mno hakika nilivyaa ujasiri mkali mno na nilianza kuishi kwa furaha sana.

Kuhusu hii vita ni kweli kuna mafioso maficho fiche mengi na ni vizuri kutaka taarifa lakini kujifunza namna ya kuchuja hizi taarifa.

Usiache kupata update maana tunatarajia kuja kiwaeleza watoto na hata wajukuu wetu.
 
Kama tangazo la biashara sawa. Lakini si ushauri muafaka kwa watu wenye akili zao, walio objective na wenye uwezo wa kupitia sources mbali mbali za habari na kupima ukweli na uhalisia wa habari hizo. Ni kutaka nao wakumbatie ujinga (ignorance).

Ukiwa mfuatiliaji mzuri wa habari za kimataifa huwezi kudanganyika wala kujidanganya kirahisi. Sources ambazo ni notorious kwa kutoa habari fake, biased zinajulikana. Hata namna ya kupima mielekeo na milengo ya media mbali mbali ipo. Uchaguzi ni wako kuishi katika giza au mwanga.

Kwa mfano hapa nasoma makala kwenye website ya CNN inayosema: Denmark opens its arms to Ukrainians, while trying to send Syrian refugees home, By Tara John, CNN. Imetoa uchambuzi mzito jinsi nchi za Magharibi zilivyoipa kipaumbele hii vita na zinavyojali zaidi wakimbizi wa kizungu na kubagua watu wa mataifa mengine na rangi tofauti wenye shida hiyo hiyo ya ukimbizi tena toka kwenye hatari kubwa zaidi. Ni elimu tosha.

Kwa wale ambao uwezo wao unaishia kwenye ushabiki tu katika masuala ya kimataifa, ushauri wako uko sawa. Haya mambo hayana afya kwao. Heri wasome kitabu chako.
 
CNN ni chombo namba moja cha propaganda za magharibi, hasa za kiliberali.
Huwezi kupata chochote objective kutoka CNN.
 
CNN, BBC, DW, VOA wanampumbaza nani katika vita vya ukraine na russia? Habari zao zinaipendelea ukraine tu
 
Unachoeleza ki kitu bora sana.

Nakumbuka corona ilipoanza niliona sasa ni mwisho wa dunia na nikaona mimi na familia yangu tukiwa na hofu mno.

Baada ya Mh Rais Magufuli Mungu Mrehemu na kumponya nafsi yake alitueleza Mambo mazuri mno hakika nilivyaa ujasiri mkali mno na nilianza kuishi kwa furaha sana.

Kuhusu hii vita ni kweli kuna mafioso maficho fiche mengi na ni vizuri kutaka taarifa lakini kujifunza namna ya kuchuja hizi taarifa.

Usiache kupata update maana tunatarajia kuja kiwaeleza watoto na hata wajukuu wetu.
Noise vs Signal
Kwa sasa kinachoendelea ni kelele nyingi za propaganda,
Ni baada ya muda kupita na mambo kutulia ndiyo watu wataona wazi kipi kilikuwa kweli na kipi kilikuwa uongo.
Hivyo ni ngumu sana kupata kitu cha kuja kuwasimulia wajukuu baadaye kwa kufuatilia yanayoendelea sana.
Na pia, kumbukumbu zetu binafsi huwa zinatusaliti, labda kama unakuwa ukiandika mahali.
Lakini miaka 20 ijayo, ni machache mno yanayoendelea sasa utakuwa unayakumbuka au yataonekana kuwa hata na maana.
Kama ulikuwa na utimamu miaka ya osama, afgan na iraq, kumbuka ni mangapi yalikuwa yanaendelea na yapi unayakumbuka au yanaonekana kuwa na umuhimu kwa sasa.
 
CNN ni chombo namba moja cha propaganda za magharibi, hasa za kiliberali.
Huwezi kupata chochote objective kutoka CNN.
Wewe sio msomaji/msikilizaji wa CNN. Wana habari za uhakika. Mlengo ndio wa demokrasia ya kiliberali. Hii huheshim binadamu wa mataifa na rangi zote. Ukiwa na uwezo wa kuchuja milengo utaweza kufaidika na CNN. Hakuna propaganda za magharibi. Haifanani na the likes of RT, TBC na Channel 10.

Kama hupendi uhuru ulioko CNN basi fuatilia right-wing media kama Fox News. Huko ndiko Utaka koele wana na modeli za watu kama Trump.
 
Kinachonishangaza hata humu jukwaani watu na ufahamu wao wanazileta na kuzisambaza hata hawafikirii!,tukianza kuwaita nyumbu wanasema hatuna adabu si ajabu hii!
 
Umenena Kweli Kwasasa Hata hii mitandao imekuwa na Unyanyasaji Usio na Mfano
yaani Wanakupangia nini Upende yaani Kile wakitakacho wao ndio Ukitake na ww
Usiposti Jambo linalo kwenda kinyume na wao
Twitter Kosa Kuipongeza Urusi au Kuiunga mkono Urusi
wao wanataka Uipondee tu Urusi!
Hii dunia Inashida sana na ukiona Wanazuia Kwa nguvu upande Mmoja wa Habari Ujue Wanahali Mbaya
 
Wewe sio msomaji/msikilizaji wa CNN. Wana habari za uhakika. Mlengo ndio wa demokrasia ya kiliberali. Hii huheshim binadamu wa mataifa na rangi zote. Ukiwa na uwezo wa kuchuja milengo utaweza kufaidika na CNN. Hakuna propaganda za magharibi. Haifanani na the likes of RT, TBC na Channel 10.

Kama hupendi uhuru ulioko CNN basi fuatilia right-wing media kama Fox News. Huko ndiko Utaka koele wana na modeli za watu kama Trump.
Duh,
Mkuu kama unaweza kushupaza shingo kabisa kwamba CNN ni chombo objective cha habari basi tuseme tu kwamba propaganda za waliberali zimekunasa, na hakuna namna tunaweza kukusaidia.
CNN siyo tu chombo kilicho biased, bali pia ni chombo chenye habari za hovyo kabisa.
Wakati mwingine hata satirical sites kama The Babylon Bee au The Onion vinafanya vizuri kuliko hata CNN.
 
Wewe ni mfuatiliaji wa babylon bee, the onion?

Kama ni hivyo uko sawa. CNN ni media ya ovyo kabisa.
 
Back
Top Bottom