Hiki ndiyo kituko nlichowahi kukutana nacho makaburini usiku. Sitosahau

Hiki ndiyo kituko nlichowahi kukutana nacho makaburini usiku. Sitosahau

Yeah mimi binafsi nashukuru sijawahi kukutana na hayo mauzauza na naomba nisikutane nayo mpaka siku nakufa ila naamini hivi viumbe vipo sana tuu
Ndio ndugu, hivi viumbe vipo tena tuko navyo kila sehemu. Ila huwa havipendi kuonekana mpaka pale kunapokuwa na sababu maalum ya wao kufanya hivyo.
 
Vitu vya ajabu vipo sana ,nakumbuka kipindi nipo kidato cha tatu mwaka 2005 shule x maeneo ya shiyanga.
Baada ya kutoka kwenye kipindi kile cha usiku mida kama ya saa nne kasoro hivi ,kwenye mabweni kuna uwanja wa mpira wa kikapu na baada ya uwanja unavuka barabara kuna kipori fulani

Sasa kwenye pori hilo tulikuwa tunapenda kwenda kujisaidia kama unavyojua vyoo vya shule kukuta vichafu ni jambo la kawaida kwa kipindi kile,hivyo kuna baadhi hatukupendelea kujisave toilet hasa mida ya usiku.
Tulikuwa na tabia ya kualikana kwenda pori kujisave ,sa siku hiyo nikakosa wadau ,ikabidi niliunge mwenyewe nikazama pori peke angu,

Nilienda nikavuka barabara,nikavuka kiwanja cha mipira wa kikapu ,huyooo pori .
Nilijisaidia ,ile nipo hatua ya kumaliza nikashangaa naona gari linapita mle porini,yani kulingana na hali ya pori kwa gari kupita haiwezekani,pana miti ,mashimo ,mawe,visiki nk.

Ila pamoja na hali yote hiyo ile gari ilipita hadi kwenye miti ,inakuwa kama inaigonga miti lakini inazidi kutokomea.
Niliduwaa sana pale chini nilipokuwa nimechuchumaa kwa mana ilipita mbele yangu upande wa kule nilikotoka.

Nilichomoka mbie kutoka huko pori hadi kwenye dom langu.Niliogopa sana ,sikujua kabisa maana ya ile gari iliyo kuwa imejaa watu ikipita kwenye sehemu yenye vikwazo vya miti na vichaka vyote bila tatizo utazani ipo kwenye lami.
Tangu siku hiyo sikurudia kwenda porini kujisaidia.
Maeneo ya mapori na ukimya ukimya ndio huwa makazi yao. Unaweza kuwa unapita kila siku usiwaone, lakini wao wanakuona ila wanaamua kukuchunia tu.

Sasa siku wakitaka kukuonesha vihoja ndo wanafanya kama walivyokufanyia au nifanyia mimi.
 
Niaje waungwana,

Hiki kisa, au tukio lilintokea miaka mingi kidogo. Enzi zile za kwenda kuangalia movie katika vibanda vya video. Sasa siku hiyo nilienda kuangalia video katika banda moja nililokuwa napenda kwenda kuangalia.

Banda hilo lilikuwa maeneo ya Manzese Midizini kwa mama fulan jina kapuni, na mimi home ni maeneo ya Magomeni mikumi jijini Dar es Salaam.

Njia yangu kubwa kutoka home hadi Midizini, ilikuwa kagera kimamba, nakatiza daraja la mbao, napandisha pale Mburahati Mianzini, napasua Makaburi ya Mburahati kwa jongo hadi midizini. Na kurudi i was doing the same thing kwa kufuata njia ile ile niliyokuja nayo.

Ratiba yangu kwa siku ilikuwa ni shule kwanza, nlipotoka shule, nlielekea mazoezini (mpirani), baada ya kutoka mpirani ndo nikawa naenda sasa kujipoza vibandani kumuangalia Dharmendra, Amita Bachan, Rambo, Anord, Bruce Lee nk.

Ratiba yangu ya mwisho baada ya kutoka huko katika banda la video, ilikuwa ni kwenda katika maskani yetu fulan ambayo ni ya uncle wangu kujifunza mchezo wa karate. Uncle ndo alikuwa masta wetu. Hivyo nilijiamini sana kwamba hakuna kitu au mjinga yeyote anaeweza kunifanyia ushen.z.i mbele yangu. Karate na ngumi ni michezo ambayo humfanya mchezaji ajiamini sana, kwamba anaweza kupambana na mtu yoyote, mahali popote na kwa muda wowote.

Basi bwana siku hiyo nimemaliza kumuangalia Dharmendra mida ya usiku, nakumbuka ilikuwa movie fulan inaitwa LOHA. Tukatoka kila mtu akawa anaelekea kwao. Mimi nikawa natambaa mdogo mdogo kuelekea home.

Nilivyofika katika makaburi ya mburahati kwa jongo kama kawaida yangu, nikageuka nyuma kuangalia huku na huko, sikuona mtu ananifuata nikaendelea na safari yangu.

Sasa nimesogea sogea hadi katikati ya makaburi, kwa mbele nikaona kitu kama mbuzi mweupe, lakini kilichonishangaza na kunitia hofu ni kwamba yule mbuzi alikuwa kama vile amekaa kwenye kitu anavuta sigara, nikafikicha macho kama vile siamini ninachokiona.

Nikaendelea kusogea taratibu ili nihakikishe kuwa ninachokiona ni chenyewe au.

Kusogea nikasikia mbuzi anakohoa, ikabidi nigeuke ili nitoke nduki maana niliona pale hata karate zangu haziwezi kunisaidia.

Sasa wakati nageuka nikaona nyuma yangu kuna kundi la watu wamebeba jeneza wanakuja upande wangu halafu juu ya jeneza kuna mtu kakaa na yeye anavuta fegi, halafu kila jamaa wakipiga hatua, yeye anajamba.

Nikaona nyuma hakufai bora huku huku nilipotaka kupakimbia. Nikageuka na kuanza kutoka nduki kuelekea kwa mbuzi anaevuta sigara. Ghafla nikaona na mbuzi na yeye anatoka nduki na sigara yake.

Akili ikanijia nikaacha kukimbia ule upande anakimbilia mbuzi, nikaelelea upande wangu.

Breki ya kwanza ikawa Magomeni Mapipa, yani sikumbuki hata mikumi home nilipapita saa ngapi, au kule Mapipa nilifika fikaje fikaje.

Nikarudi nyumbani salama. Toka siku hiyo sikurudi tena kwenda video usiku, na ukawa mwisho wa kuendekeza movie.

Ni nani mwngine ambae ashawahi kukumbana na songombingo la aina hiyo?

Aisee it was scary
Screenshot_20231130_140348_X.jpg
 
Hapo ndio tangawizi ya hii chai ilipo...
Dogo we utakuwa wa juzi juzi.
miaka hiyo kulikuwa na Cinema za ukutani kwenye kumbi chache za mabar kideo kilikuja baadae sana na wamiliki walikuwa wachache so haikuwa ajabu kutoka Buguruni hadi Mapipa kucheck videos, Mi mwenyewe nilikuwa natoka kigogo hadi Mapipa au Manzese Midizini/Tandale kufuata hizo Muvi
 
Niliandaa maisha yang katika pande zote muhim kama vile elimu na michezo.

Sema ndo hivyo binadam tunapanga yetu na Mungu nae anapanga yake hivyo nilipishana na malengo yangu. Kama wewe mtu mzima utakuwa umeifungua code niliyoweka hapa 😂😂😂

Sawa Mkuu
 
Hiyo ninayokwambia mimi imetokea miaka ya 90. Alafu haya mambo hutokea pale ambapo mtu hukutarajia.

Mimi mwenyewe kama unavyosema, nilikuwa napita sana usiku yani ndio ilikuwa njia yangu ya kila siku. Sasa siku ile nahisi vibwengo walikuwa washachoka kunivumilia kupita pale, wakaamua kutaka kuniteka ndo nikatoka nduki.
Watu hawajui tu hao
 
Ulikimbiaje kumshinda pepo? Speed ya pepo ni sawa na mwanga unavyosafiri kwa kasi. Ni chai ya tangawizi.
 
Dogo we utakuwa wa juzi juzi.
miaka hiyo kulikuwa na Cinema za ukutani kwenye kumbi chache za mabar kideo kilikuja baadae sana na wamiliki walikuwa wachache so haikuwa ajabu kutoka Buguruni hadi Mapipa kucheck videos, Mi mwenyewe nilikuwa natoka kigogo hadi Mapipa au Manzese Midizini/Tandale kufuata hizo Muvi
Sahihi kabisa nduguyangu. Huyo ni mtoto wa 2005, ndomaana haya mambo hayafahamu.
 
Ulikimbiaje kumshinda pepo? Speed ya pepo ni sawa na mwanga unavyosafiri kwa kasi. Ni chai ya tangawizi.
Pepo alishindwa na nguvu za Mungu. Si unaona hata mimi mwenyewe sikujua nimefikaje fikaje Magomeni mapipa. Hii inamaana kuwa nilipata nguvu ya ziada ya kunitoa pale bila mimi mwenyewe kujijua.
 
Back
Top Bottom