Medecin
JF-Expert Member
- Nov 29, 2011
- 8,221
- 22,496
KabisaWw kama mm nakereka mpaka basi yaani sipendi hata kidogo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
KabisaWw kama mm nakereka mpaka basi yaani sipendi hata kidogo
You're among them. But u pretendBora hao kuliko Wale wa kuandika jomoni,bhana,xaxa,p,pouwah. Me akiandika maneno hayo kwenye text message naacha kuchat nae hapo hapo.
Siyo kweli,siku hizi watu wengi(me & ke) wanaandika huo ujinga.Wanawake sana sana ndiyo Lugha zao hizi hasa hawa wanaoitwa mademu
Makabila mengi yenye asili ya mkoa wa Kagera haweka H pasipo na herufi hiyo na huacha kuitumia panapostahili kutumika.Hiyo ni athari ya lugha mama, na hao ni watani wangu wa kutokea mkoa wa Kagera wanaojisifu sana kwa usomi,na maarufu sana kwa ulaji wa panzi wa kijani.
Wengi waongezao H, ni watu wa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha. jaribu kuchunguza
Mi bhana (nafanya makusudi) sina clue kabisa hao watu wanaweza kuwa ni wa asili gani ila kama nataka kuwaamini amini hivi... Kilimanjaro, Kagera au mkoa mwingine wowote ule unaojivuta jivuta kidogo kielimu kama vile Mbeya!Hiyo ni athari ya lugha mama, na hao ni watani wangu wa kutokea mkoa wa Kagera wanaojisifu sana kwa usomi,na maarufu sana kwa ulaji wa panzi wa kijani.
Madem na wavulana, mwanaume ukikuta anaandika hivyo lazima utafakari Mara mbiliSiyo kweli,siku hizi watu wengi(me & ke) wanaandika huo ujinga.
Lugha ya Kiingereza inatupa changamoto sana ktk kuandika na kuongea kuna wakati utamkuta mtu yupo vizuri ktk maandishi lkn kuongea shida. Sasa huu mfumo umekuja ktk lugha ya Kiswahili kwahiyo linapokuja ktk suala la kuandika ni shida tupu. Jinsi watu wanavyohangaika ktk lugha ya Kiingereza ndivyo hivyo wanavyohangaika ktk lugha ya KiswahiliUnaposema haina tofauti na lugha ya Kiingereza una maana gani mkuu?
Kuna wale waliokuja mjini juzi na Kiswahili wamejifunza ukubwani, hao naelewa sababu.Huwa najiuliza kama mtu amesoma kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba na labda akaenda sekondari pia, inawezekanaje anaandika hivi:
Neno Hakuna anaandika akuna, Usipite anaandika husipite, Ibada anaandika Hibada, hifadhi anaandika ifadhi, akiba anaandika hakiba, usitupe anaandika husitupe, mahindi anaandika maindi, hayupo anaandika ayupo. n.k.
Yani nimebaki najiuliza hiki ni kiswahili cha kisasa au?
Naweza kumtetea mtu anayepata shida kwenye lugha ya Kiingereza.Lugha ya Kiingereza inatupa changamoto sana ktk kuandika na kuongea kuna wakati utamkuta mtu yupo vizuri ktk maandishi lkn kuongea shida. Sasa huu mfumo umekuja ktk lugha ya Kiswahili kwahiyo linapokuja ktk suala la kuandika ni shida tupu. Jinsi watu wanavyohangaika ktk lugha ya Kiingereza ndivyo hivyo wanavyohangaika ktk lugha ya Kiswahili
Umeeleza vyema. Wataalamu wa lugha ya Kiswahili wanahitajika sana kwasbb miaka inayokuja lugha ya Kiswahili itapoteza hadhi kwasbb ya kuwepo makosa ya kisarufi.Naweza kumtetea mtu anayepata shida kwenye lugha ya Kiingereza.
1. Lugha hiini ya kigeni sana,haipo hata katika tawi sawana lugha zetu za kibantu.
2. Lugha ya Kiingereza ni lugha iliyotokana na mchanyato wa lugha nyingi tofauti tofauti (lingua franca) na ingawa sifa hii si lazima iifanye lugha ikose mtiririko wa kimantiki (Kiswahili ni lingua franca pia, lakini ina mtiririko mzuri wa kimantiki) kwenye Kiingereza, lugha imepoteza mtiririko wa kimantikikatika sarufi. Lugha imekuwa kama nusumoja ya lugha ni sheria, na nusu nyingine ni ukiukwaji wa hizo sheria. Kwa mtu ambaye amezoea lugha ambayo kiasi kikubwa sana inakwenda kwa sheria, na ukiukwaji wa sheriani mdogo sana, katika sarufi, kujifunza Kiingereza ni kama kujifunza kuongea lugha iliyo na makosa kibao. Kiswahili's grammar is more logical and consistent than English's.
3. Katika Kiingereza, hakuna mfululizo mzuri wa matamshi. Ni kama vile inabidi ujifunze kutamka kila neno. Si kama Kiswahili ambacho, ukijifunza matamshi yake, unaweza kutamka karibu kila neno, maneno ambayo yanachepuka kutoka kanuni za matamshi ni machache sana. Kiswahili is a phonetic language.
Kwa sababu hizi tatu, nitaelewa mtu wa Afrika Mashariki aambaye kakua katika lugha zetu za Kinabtu au Kiswahili, akipata tabu kuelewa Kiingereza.
Tatizo watu wanaharibu mpaka Kiswahili!
Hapo, kuwatetea nashindwa.
Ha ha haUkiniandikia msg yenye maneno hayo sikujibu milele.
Umeangalia kwa makini hiyo sentensi, ungedundua nimeiwekea " " na mwanzo mwisho nimeweka makosa yanayofanywa na watumiaji wa lugha ikiwemo hiyo "hunabisha!"Hiyo "hunabisha" ndo moja ya makosa yenyewe.
Twambie origin yako
Cha ajabu ni kwamba mpaka baadhi ya walimu wa kiswahili wanafundisha hivyo hivyo kwenye a wanaweka h, kwenye h wanaweka a (mfano hakuna wanaweka akuna)Makabila mengi yenye asili ya mkoa wa Kagera haweka H pasipo na herufi hiyo na huacha kuitumia panapostahili kutumika.
Pia jamii hizo kwa asili yao hawawezi kutamka neno lenye herufi ng'__ .
Mfano:- Ngambo badala ya Ng'ambo.
Ngombe badala ya Ng'ombe.
Ila kuhusu hao hili tatizo la mleta mada ni kutokana na ujinga kuongezeka. Na ukifuatilia utagundua tatizo kuongezeka badala ya kupungua
Walioko mitandaoni ni watu wa aina zote usiseme wa mikoa fulani, ila swali ni kwamba si wamesoma kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba na wamefundisha (a, e, i, o, u) (ha, he, hi, ho, hu) darasani?Mi bhana (nafanya makusudi) sina clue kabisa hao watu wanaweza kuwa ni wa asili gani ila kama nataka kuwaamini amini hivi... Kilimanjaro, Kagera au mkoa mwingine wowote ule unaojivuta jivuta kidogo kielimu kama vile Mbeya!
Nasema haya kwa sababu nashawishika kuamini kwamba, ni hiyo mikoa ndiyo huenda ina watu wengi mitandaoni kutokana na exposure yao ya elimu! Na ni huko mitandaoni ndiko zimeshamiri "akuna yeyote wa kumcheka mwenzake apa, mbona ata uko kwenu wapo na kama hunabisha; sema!"
Kuna tofauti kati ya kuwa mitandaoni na kuwa mitandaoni kwa idadi kubwa!!Walioko mitandaoni ni watu wa aina zote usiseme wa mikoa fulani, ila swali ni kwamba si wamesoma kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba na wamefundisha (a, e, i, o, u) (ha, he, hi, ho, hu) darasani?
Watu wa mikaoni ndiyo Watu gani?
Demu akikuandikia 'Mupenzi njoo hule Mzigo' utamchunia?Ukiniandikia msg yenye maneno hayo sikujibu milele.
Ingekuwa ni katika kuzungumza ingeeleweka, lakini kwenye uandishi athari hizo hazipaswi kuwepo. Mi nadhani tuna matatizo ya msingi ya kutozingatia yale tujifunzayo.usomi