Hiki ni Kiswahili cha kisasa au?

Hiki ni Kiswahili cha kisasa au?

Hiyo ni athari ya lugha mama, na hao ni watani wangu wa kutokea mkoa wa Kagera wanaojisifu sana kwa usomi,na maarufu sana kwa ulaji wa panzi wa kijani.
Makabila mengi yenye asili ya mkoa wa Kagera haweka H pasipo na herufi hiyo na huacha kuitumia panapostahili kutumika.

Pia jamii hizo kwa asili yao hawawezi kutamka neno lenye herufi ng'__ .
Mfano:- Ngambo badala ya Ng'ambo.
Ngombe badala ya Ng'ombe.

Ila kuhusu hao hili tatizo la mleta mada ni kutokana na ujinga kuongezeka. Na ukifuatilia utagundua tatizo kuongezeka badala ya kupungua
 
Wengi waongezao H, ni watu wa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha. jaribu kuchunguza
Hiyo ni athari ya lugha mama, na hao ni watani wangu wa kutokea mkoa wa Kagera wanaojisifu sana kwa usomi,na maarufu sana kwa ulaji wa panzi wa kijani.
Mi bhana (nafanya makusudi) sina clue kabisa hao watu wanaweza kuwa ni wa asili gani ila kama nataka kuwaamini amini hivi... Kilimanjaro, Kagera au mkoa mwingine wowote ule unaojivuta jivuta kidogo kielimu kama vile Mbeya!

Nasema haya kwa sababu nashawishika kuamini kwamba, ni hiyo mikoa ndiyo huenda ina watu wengi mitandaoni kutokana na exposure yao ya elimu! Na ni huko mitandaoni ndiko zimeshamiri "akuna yeyote wa kumcheka mwenzake apa, mbona ata uko kwenu wapo na kama hunabisha; sema!"
 
Kuna jamaa alinitumia text message inayosema Pg. Kila nikiangalia sipati jibu maana yake, akatuma tena, Pg. Jamaa mwenyewe alikuwa amechukua namba yangu siku si nyingi na hatuna mazoea, nikauliza jamaa yangu maana ya Pg ni nini? ndiyo akaniambia ni Piga. Dah. Na mimi nikamtumia message Spg. Nadhani alinielewa kwamba Sipigi.
 
Unaposema haina tofauti na lugha ya Kiingereza una maana gani mkuu?
Lugha ya Kiingereza inatupa changamoto sana ktk kuandika na kuongea kuna wakati utamkuta mtu yupo vizuri ktk maandishi lkn kuongea shida. Sasa huu mfumo umekuja ktk lugha ya Kiswahili kwahiyo linapokuja ktk suala la kuandika ni shida tupu. Jinsi watu wanavyohangaika ktk lugha ya Kiingereza ndivyo hivyo wanavyohangaika ktk lugha ya Kiswahili
 
Huwa najiuliza kama mtu amesoma kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba na labda akaenda sekondari pia, inawezekanaje anaandika hivi:

Neno Hakuna anaandika akuna, Usipite anaandika husipite, Ibada anaandika Hibada, hifadhi anaandika ifadhi, akiba anaandika hakiba, usitupe anaandika husitupe, mahindi anaandika maindi, hayupo anaandika ayupo. n.k.

Yani nimebaki najiuliza hiki ni kiswahili cha kisasa au?
Kuna wale waliokuja mjini juzi na Kiswahili wamejifunza ukubwani, hao naelewa sababu.

Tatizo kuna watu tumesomanao tangu shule ya msingi wapo mjini miaka mingi, Kiswahili hawajajifunza ukubwani, nao wanaandika na kusema hivyo.

Wanakera sana.
 
Lugha ya Kiingereza inatupa changamoto sana ktk kuandika na kuongea kuna wakati utamkuta mtu yupo vizuri ktk maandishi lkn kuongea shida. Sasa huu mfumo umekuja ktk lugha ya Kiswahili kwahiyo linapokuja ktk suala la kuandika ni shida tupu. Jinsi watu wanavyohangaika ktk lugha ya Kiingereza ndivyo hivyo wanavyohangaika ktk lugha ya Kiswahili
Naweza kumtetea mtu anayepata shida kwenye lugha ya Kiingereza.

1. Lugha hiini ya kigeni sana,haipo hata katika tawi sawana lugha zetu za kibantu.

2. Lugha ya Kiingereza ni lugha iliyotokana na mchanyato wa lugha nyingi tofauti tofauti (lingua franca) na ingawa sifa hii si lazima iifanye lugha ikose mtiririko wa kimantiki (Kiswahili ni lingua franca pia, lakini ina mtiririko mzuri wa kimantiki) kwenye Kiingereza, lugha imepoteza mtiririko wa kimantikikatika sarufi. Lugha imekuwa kama nusumoja ya lugha ni sheria, na nusu nyingine ni ukiukwaji wa hizo sheria. Kwa mtu ambaye amezoea lugha ambayo kiasi kikubwa sana inakwenda kwa sheria, na ukiukwaji wa sheriani mdogo sana, katika sarufi, kujifunza Kiingereza ni kama kujifunza kuongea lugha iliyo na makosa kibao. Kiswahili's grammar is more logical and consistent than English's.

3. Katika Kiingereza, hakuna mfululizo mzuri wa matamshi. Ni kama vile inabidi ujifunze kutamka kila neno. Si kama Kiswahili ambacho, ukijifunza matamshi yake, unaweza kutamka karibu kila neno, maneno ambayo yanachepuka kutoka kanuni za matamshi ni machache sana. Kiswahili is a phonetic language.

Kwa sababu hizi tatu, nitaelewa mtu wa Afrika Mashariki aambaye kakua katika lugha zetu za Kinabtu au Kiswahili, akipata tabu kuelewa Kiingereza.

Tatizo watu wanaharibu mpaka Kiswahili!

Hapo, kuwatetea nashindwa.
 
Umeeleza vyema. Wataalamu wa lugha ya Kiswahili wanahitajika sana kwasbb miaka inayokuja lugha ya Kiswahili itapoteza hadhi kwasbb ya kuwepo makosa ya kisarufi.
 
Hiyo "hunabisha" ndo moja ya makosa yenyewe.
Twambie origin yako
Umeangalia kwa makini hiyo sentensi, ungedundua nimeiwekea " " na mwanzo mwisho nimeweka makosa yanayofanywa na watumiaji wa lugha ikiwemo hiyo "hunabisha!"
 
Makabila mengi yenye asili ya mkoa wa Kagera haweka H pasipo na herufi hiyo na huacha kuitumia panapostahili kutumika.

Pia jamii hizo kwa asili yao hawawezi kutamka neno lenye herufi ng'__ .
Mfano:- Ngambo badala ya Ng'ambo.
Ngombe badala ya Ng'ombe.

Ila kuhusu hao hili tatizo la mleta mada ni kutokana na ujinga kuongezeka. Na ukifuatilia utagundua tatizo kuongezeka badala ya kupungua
Cha ajabu ni kwamba mpaka baadhi ya walimu wa kiswahili wanafundisha hivyo hivyo kwenye a wanaweka h, kwenye h wanaweka a (mfano hakuna wanaweka akuna)
 
Mi bhana (nafanya makusudi) sina clue kabisa hao watu wanaweza kuwa ni wa asili gani ila kama nataka kuwaamini amini hivi... Kilimanjaro, Kagera au mkoa mwingine wowote ule unaojivuta jivuta kidogo kielimu kama vile Mbeya!

Nasema haya kwa sababu nashawishika kuamini kwamba, ni hiyo mikoa ndiyo huenda ina watu wengi mitandaoni kutokana na exposure yao ya elimu! Na ni huko mitandaoni ndiko zimeshamiri "akuna yeyote wa kumcheka mwenzake apa, mbona ata uko kwenu wapo na kama hunabisha; sema!"
Walioko mitandaoni ni watu wa aina zote usiseme wa mikoa fulani, ila swali ni kwamba si wamesoma kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba na wamefundisha (a, e, i, o, u) (ha, he, hi, ho, hu) darasani?
 
Kuna tofauti kati ya kuwa mitandaoni na kuwa mitandaoni kwa idadi kubwa!!

Btw, hivi hata kama wamesoma kwani kuna mtu anafundishwa kuandika maneno yote au kinachotokea ni mtu kujifunza jinsi ya kuumba na kuchanganya herufi kisha kupata maneno husika na kinachofuata ni mazoea yake?!

Kwamba, kwa mfano baada ya kujifunza, akafahamu salamu ya asubuhi inaitwa "habari za asubuhi" lakini atakachoandika ni kile ambacho amezea kutokana na hoja walizotoa wadau!

Kwamba, ameshazoea wakati anaongea anasema "abari za asubui"... unatarajia hiyo salamu ataiandikaje siku akilazimika kuandika?!
 
Back
Top Bottom