Hiki ni Kiswahili cha kisasa au?

Hiki ni Kiswahili cha kisasa au?

Vb

Huwa najiuliza kama mtu amesoma kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba na labda akaenda sekondari pia, inawezekanajevhu anaandika hivi:

Neno Hakuna u akuna, Usipite anaandika husipite, Ibada anaandika Hibada, hifadhi anaandika ifadhi, akiba anaandika hakiba, usitupe anaandika husitupe, mahindi anaandika maindi, hayupo anaandika ayupo. n.k.

Yani nimebaki najiuliza hiki ni kiswahili cha kisasa au?
 
Sio walio zaliwa mjin mkuu!!watu wameathiriwa na lugha mama
Sio kweli huo uandishi hauhusiani kwa namna yoyote ile na kuathiriwa na lugha fulani, kuna watu hawajui lugha nyingine yoyote zaidi ya kiswahili ila uandishi wao mbovu kuliko hata mimi ambaye nimeanza kujifunza kiswahili ukubwani.
 
Sio walio zaliwa mjin mkuu!!watu wameathiriwa na lugha mama
Yaani hata tatizo siyo lugha Mama, watu wanabadilika tu wanaiga iga tu, mi hadi nikadhani labda ni vimisemo tu vitaisha, lakini unakuta hadi watu kama waandishi wa habari, wasoma habari tena kwa luninga anasoma 'abali' mi nakereka kweli, nkajua ni ndugu zangu wahaya tu kumbe siku hizi kila MTU Kiswahili kinapoteza mvuto wake hivi tunakiona, ndo hapo unaposhangaa jamani kuwa 'jomoni' inakera kweli
 
Mimi nitasema, hiyo ni lugha ya watu wa kundi maalumu km vijana, watu wa kijiwe fulani, na kadhalika. Taabu inakuja pale ambapo watumiaji wa lugha ya namna hiyo wanaposhindwa kupambanua watu wanaotumia lugha hiyo na wale wasiotumia lugha hiyo.
Taabu ya kushindwa kutofautisha ANA na HANA ni tatizo la shule zetu. Watu hawasomi Kiswahili vizuri kabisa. Kadhalika RAKE na LAKE husemwa namna ile ile. Ni udhaifu wa shule.
 
Huwa najiuliza kama mtu amesoma kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba na labda akaenda sekondari pia, inawezekanaje anaandika hivi:

Neno Hakuna anaandika akuna, Usipite anaandika husipite, Ibada anaandika Hibada, hifadhi anaandika ifadhi, akiba anaandika hakiba, usitupe anaandika husitupe, mahindi anaandika maindi, hayupo anaandika ayupo. n.k.

Yani nimebaki najiuliza hiki ni kiswahili cha kisasa au?
Fuatilia post za Nikki wa II, jamaa pamoja na elimu ya uzamili ni bure kabisa.
 
Bora hao kuliko Wale wa kuandika jomoni,bhana,xaxa,p,pouwah. Me akiandika maneno hayo kwenye text message naacha kuchat nae hapo hapo.
Mkuu hauoni na wewe kwamba upo kundi hilo hilo?
Neno mimi wewe unaandika 'me', ndiyo maana nilipokuwa mwalimu kabla ya kustaafu nilikuwa nawalamba mboko sana wanafunzi wenye mapungufu ya uandishi wa sarufi kama wako.
 
Mkuu hauoni na wewe kwamba upo kundi hilo hilo?
Neno mimi wewe unaandika 'me', ndiyo maana nilipokuwa mwalimu kabla ya kustaafu nilikuwa nawalamba mboko sana wanafunzi wenye mapungufu ya uandishi wa sarufi kama wako.
shikamoo teacher hivi unadhani nimeandika me kwa bahati mbaya? Nimeandika hapo Ili kujitofautisha na hao wanaoandika uhuni wa xaxa,mm,ss n.k. Nilichoandika mimi ni lugha mbili katika sentensi moja me kiingereza na yaliyobaki nimeyaandika kiswahili. Au huoni rais wako anavyochanganya lugha. Hilo sio kosa
 
Kuna wapuuzi wengine, neno tu wanaandika "tyu".
Washenzi kabisa wa lugha hao.
 
Hao wanaboa lakini kuna wale wanaoongea na kuimba " tunakulaga" , "nakupendaga", hizo ga ga ga si Kiswahili kabisa!!

Nashangaa zinaendaje hewani kama hakuna vyombo vinavyosimamia hilo..
 
Back
Top Bottom