Hiki ni nini? Naombeni ushauri nachanganyikiwa. Nimekopa Milioni 14 natakiwa kurudisha Milioni 39

Hiki ni nini? Naombeni ushauri nachanganyikiwa. Nimekopa Milioni 14 natakiwa kurudisha Milioni 39

Kwanini usingeenda NMB au CRDB?
Bayport walinifata ofisini ili wanikopeshe nilipowauliza riba ni asilimia wakaanza chenga chenga braah braah kibao,nikambananisha mmoja wao akaniambia riba ni 47% nikawafukuza ofisini.
Duuuh 47%????

Huo ni wizi, hiyo yaani kwa makadirio pasu pasu ukikopa 10,000,000 unalipa 15,000,000
 
Mikopo mingi kwa Watumishi wa Umma na Binafsi kwenye Mabenki ya biashara sio rafiki hata kidogo.

Maana riba zimekuwa kubwa kuliko wanavyosema.

Kwa hesabu ya haraka, ni kama vile Riba imekuwa ni asilimia 60 tofauti na hiyo asilimi 17 ama 19 inayoandikwa kwenye Mkataba wa Mkopo wako.

Kama hauna ulazima sana, sio vyema kukopa.

Ndiyo maana inashauriwa;

"Tukope kwa Malengo"
 
1. Mkuu inamaana huko ulipo hamna NMB au CRDB?

2. Halafu wewe ni mwalimu wa Aina gani? Inamaana hukuambiwa makato ni kiasi gani Kwa mwezi?

Ukakopa tu?

Pathetic

Wakati wenzio Kwa makato hayo wanakopa zaidi ya Milioni 20.
 
Waalimu kabla ya kukopa uliza riba ni asilimia ngapi? Kama huwezi kujua hilo ,waambie rejesho kwa mwezi litakuwa kiasi gani uzidishe kwa idadi ya miezi uliyekopa halafu jumla yake utoe kwenye mkopo waliokupitishia.Mara nyingi huwa Wana take advantage ya umbumbumbu wa waalimu kwenye elimu ya fedha kwani wao huuluza tuu watapata kiasi gani na kwa muda gani tuu, suala la riba, garama za mkopo kama loan processing fee , bima nk hawajui, na ukiuliza riba kichwa kichwa badala ya kukuambia riba kwa mwaka , anaigawanya kwa 12 anakuambia riba ya mwezi wewe ukiona digit ni ndogo inaingia mkenge
Sidhani Kama Inahitaji kwenda Hadi chuo ili mtu ajue ulazima wa kuuliza kiwango Cha kulipa baada ya kukopa

Shida
 
Back
Top Bottom