Waalimu kabla ya kukopa uliza riba ni asilimia ngapi? Kama huwezi kujua hilo ,waambie rejesho kwa mwezi litakuwa kiasi gani uzidishe kwa idadi ya miezi uliyekopa halafu jumla yake utoe kwenye mkopo waliokupitishia.Mara nyingi huwa Wana take advantage ya umbumbumbu wa waalimu kwenye elimu ya fedha kwani wao huuluza tuu watapata kiasi gani na kwa muda gani tuu, suala la riba, garama za mkopo kama loan processing fee , bima nk hawajui, na ukiuliza riba kichwa kichwa badala ya kukuambia riba kwa mwaka , anaigawanya kwa 12 anakuambia riba ya mwezi wewe ukiona digit ni ndogo inaingia mkenge