Hiki ni nini? Naombeni ushauri nachanganyikiwa. Nimekopa Milioni 14 natakiwa kurudisha Milioni 39

Hiki ni nini? Naombeni ushauri nachanganyikiwa. Nimekopa Milioni 14 natakiwa kurudisha Milioni 39

Nimevumilia ila nimechoka acha niwaambie, ndugu walimu nimekopa AbC bank shilingi milioni 14 nikatwe kwa miaka nane sawa na miezi 96, nakatwa shilingi laki nne na elfu 14 kwa mwezi.

Nimeshangaa kukuta kwenye salary slip deni ni milioni 39😥😥😥, nimelia sana yaani nakopa 14M narudisha 39?
Mimi kwakua nilikua nina dharula ya haraka sana nilienda ABC maana niliabiwa kule hauzunguki sana na nilipofika niliongea nao tu mda ule ule nikajaza fomu nikaondokq mkopo ukaingia kesho yake, najuta sikupata mda wa wenda kusoma makubaliano na wala hawakunipa nakala yoyote!

Hii sio haki serikali iko wapi jamani?

Nifanyeje naombeni ushauri wenu
View attachment 2744997
Una level gan ya elim?

Maana umefanya mambo kienyeji sana kana kwamba shule kidogo kama ilikusumbua

Ilikuwaje uchukue mkopo bila kusoma taratibu za mkopo?

Sasa ukatwe zaid ya laki 4 kwa miaka 8 si ujinga huo?

Mbaya zaid unailaum serikali kana kwamba wao ndio waliokutuma ukakope
 
Hizo benki uchwara ni wahuni mno, mkopo wao wanatoa haraka ila sasa ukichukua atajutia mno ni lazima kujiridhisha na kuomba ushauri kabla ya yote.
 
Hata kumpa pole hamuwezi mnamlumu tukio lishatokea nyie mnarud palepale mara ooh sijui mjinga
 
Wengi wanaumia kwa kutokujua, wanaweza kukutajia riba yao ni asilimia 17 kwa mwaka ila ukipiga hesabu vizuri unaona dhahiri uhalisia haupo yaan ni zaidi ya utapeli.
 
Nimevumilia ila nimechoka acha niwaambie, ndugu walimu nimekopa ABC bank shilingi milioni 14 nikatwe kwa miaka nane sawa na miezi 96, nakatwa shilingi laki nne na elfu 14 kwa mwezi.

Nimeshangaa kukuta kwenye salary slip deni ni milioni 39[emoji26][emoji26][emoji26], nimelia sana yaani nakopa 14M narudisha 39?
Mimi kwakua nilikua nina dharula ya haraka sana nilienda ABC maana niliambiwa kule hauzunguki sana na nilipofika niliongea nao tu muda ule ule nikajaza fomu nikaondoka mkopo ukaingia kesho yake, najuta sikupata muda wa wenda kusoma makubaliano na wala hawakunipa nakala yoyote!

Hii sio haki serikali iko wapi jamani?

Nifanyeje naombeni ushauri wenu.

View attachment 2744997
pole sana... na siku nyingine soma vizuri hizo terms and conditions za mkataba kumbuka hawakupi msaada bali mnaingia biashara apo koo kua makini siku nyingine ila sidhani kama utarudia kukopa hata kwa mangi tu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Nimevumilia ila nimechoka acha niwaambie, ndugu walimu nimekopa ABC bank shilingi milioni 14 nikatwe kwa miaka nane sawa na miezi 96, nakatwa shilingi laki nne na elfu 14 kwa mwezi.

Nimeshangaa kukuta kwenye salary slip deni ni milioni 39😥😥😥, nimelia sana yaani nakopa 14M narudisha 39?
Mimi kwakua nilikua nina dharula ya haraka sana nilienda ABC maana niliambiwa kule hauzunguki sana na nilipofika niliongea nao tu muda ule ule nikajaza fomu nikaondoka mkopo ukaingia kesho yake, najuta sikupata muda wa wenda kusoma makubaliano na wala hawakunipa nakala yoyote!

Hii sio haki serikali iko wapi jamani?

Nifanyeje naombeni ushauri wenu.

View attachment 2744997Pole sana ndo mikopo ya bank ilivyo kwa Watumishi riba inakuwa kubwa kutokana na marejesho ya miaka mingi. Ila kama unakopa unawekeza hapo huna hasara yoyote.
 
Nimevumilia ila nimechoka acha niwaambie, ndugu walimu nimekopa ABC bank shilingi milioni 14 nikatwe kwa miaka nane sawa na miezi 96, nakatwa shilingi laki nne na elfu 14 kwa mwezi.

Nimeshangaa kukuta kwenye salary slip deni ni milioni 39[emoji26][emoji26][emoji26], nimelia sana yaani nakopa 14M narudisha 39?
Mimi kwakua nilikua nina dharula ya haraka sana nilienda ABC maana niliambiwa kule hauzunguki sana na nilipofika niliongea nao tu muda ule ule nikajaza fomu nikaondoka mkopo ukaingia kesho yake, najuta sikupata muda wa wenda kusoma makubaliano na wala hawakunipa nakala yoyote!

Hii sio haki serikali iko wapi jamani?

Nifanyeje naombeni ushauri wenu.

View attachment 2744997
R.I.P mr teacher.!
 
Ndugu zangu someni mikataba ya mikopo kabla ya kuchukua. Halafu kila siku mwombe sana Mungu akupe utulivu wa akili hata ukiwa kwenye matatizo. Wengi tunaomba Mungu atujalie riziki ila tunasahau kumwomba Mungu atupe utulivu wa kufanya maamuzi sahihi kwenye mambo yetu. Mwingine anaweza akapata hela ndefu kwenye dili lake ila akaishia kuipoteza pesa kwa maamuzi mabovu. Ukiwa na changamoto yoyote ya maisha tuliza akili kwasababu ukipaniki unaweza kujikuta kwenye matatizo mengine kama huyu mleta uzi. Watoa mikopo hawana huruma na kwa hizi biashara zetu riba ikishazidi 20% tayari ni majanga. Huyu mleta uzi hadi amalize deni atakuwa karudisha zaidi ya 184% ya hela aliyokopa. Huu ni uwendawazimu. Hii ishu sio ya kumwona mleta uzi ni mjinga. Ambao bado hayajawakuta mpate funzo. Wale mliokuwa mnakimbia somo la hisabati mna la kujifunza pia.
 
Mimi hata mitandao ya simu sikopi naogopa sana mikopo. Kuna siku TIGO wananilazimisha nikope nikakataa wakanitumia mkopo wao bila mimi kujua nikawapigia simu nikawaambia rudisheni pesa yenu wala siitaji mikopo yenu wananibebembeleza nikawaambia nitavyunja lain pesa wakarudisha

Hata uwe na dhiki kiasi gani jitahidi usikope jaribu kujiwekea savings zikusaidieni nyakati za shida na sio kutegemea mikopo hiyo inaumiza sana
 
Tumieni akiba zenu kwenye majanga ya ghafla msitegemee mikopo. Kuweni na nidhamu ya hela weka akiba ikuaidie kipindi cha emergency kama hizo usiwe bwege kutegemea mikopo utazidi kuwa masikini kila siku
 
Mleta mada umenikumbusha miaka ile kipindi Corona ndo inaingia wakazusha kwamba watu watakufa wengi !
mwanaume nikajirusha bank kuvuta mkopo wa 7M fasta tena na riba kubwa halafu pesa yote nikakimbilia kuwekeza kwenye biashara yangu ya majeneza nikijua misiba itakuwa mingi nirudishe mtaji na faida matokeo yake watu wakawa hawafi halafu ikafika kipindi Corona ikawa kama haipo hivi yaani sintosahau mateso ya yale marejesho ya kila mwezi ilifika mahali nikawa sina ujanja wa kupata marejesho nikauza kagari kangu(kama kale ka Mr. Bean) ndo nikamaliza deni la mkopo mpaka leo hii sitaki kabisa kusikia kitu kinaitwa mkopo!
 
Back
Top Bottom