Hiki wanachofanya benki ya CRDB ni unyanga'nyi wa peza za watu

Hiyo michezo hata Yas/Tigo wanayo, walishanidhulumu Sh15,000 hivi hivi
 
Ukisoma maoni ya watumiaji wa hizi simbanking apps huko play store utashangaa. Matatizo ni mengi, sio CRDB tu.

Ni bora utumie app kwa ajili ya miamala pekee, lipia huduma kwenye app zake husika au tumia menu za mitandao ya simu.
 
Andika barua Kwa mkurugenzi wa bank crdb utume Kwa njia ya EMS, usipopata majibu nenda BOT, usipopata majibu tafuta ziara ya kiongozi mkubwa wa kitaifa eg. Waziri mkuuu,makamu raisi ikifikia muda wa kutoa kero za wananchi kuwalipue benki hakikisha una ushahidi wa maandishi wa kutosha
 
Hiyo michezo hata Yas/Tigo wanayo, ni wezi wakubwa
Nilishalipiaga precision mara 2. Nilipa baada ya wao kusema ticket moja huwezi lipia mara mbili, nikarudia kulipa nikiamini ile iliyofail mwanzo itarudi.
Tigo walisumbua zaidi ya week.. mwisho wa siku wakaniambia liko nje ya uwezo wao niongee na precision sbb hela imeenda kwao.

Nikawacheck precision hela ikarudi.. kwahiyo hata huyu mtoa mada adeal na wote, CRDB hiyo hela imepita kwake imeenda Tanesco. Tanesco ndio warudishe hela au watoe token
 
CRDB inashuka viwango kwa haraka sana.

Kufanya miamala kupitia SimBanking siku hizi ni hatari.
Sitasahau siku nilipotoa pesa kwa ATM kwa kutumia Tembocard yao nilitoa Rand 4000 ilikua kama Sh563000 kuanagalia statement nikakuta wamenikaya Sh73,000. Wakat NCBA wanakata kama Sh 22,000 hivi.
 
Aisee pesa yako mwenyewe usumbuke hivi huu ni uonevu
 
Sitasahau siku nilipotoa pesa kwa ATM kwa kutumia Tembocard yao nilitoa Rand 4000 ilikua kama Sh563000 kuanagalia statement nikakuta wamenikaya Sh73,000. Wakat NCBA wanakata kama Sh 22,000 hivi.
Acha kabisa aisee.

Yaani ukitumia kadi yao kutoa pesa nje ya nchi hiyo ada wanayokukata itabidi uangalie mara mbilimbili kuhakiki kama ni kweli au la.

Lakini, majuzi hapa nimetoa hela kwenye ATM na sikukatwa ada kubwa. Sasa sijui wamebadili viwango vyao vya ada au labda nilibahatika tu siku hiyo…..
 
Bank zote kwa sasa ni upumbavu mtupu hata DCB
 
Na hii tabia ya kukiri kosa halafu hakuna action ndiyo inakera zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…