DOKEZO Hili daraja lilojengwa huko Ngara wengi wasema halijajengwa kwa viwango vinavyotakiwa

DOKEZO Hili daraja lilojengwa huko Ngara wengi wasema halijajengwa kwa viwango vinavyotakiwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Richard

Platinum Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
16,890
Reaction score
26,440
1757897521761.png

Daraja la Ngara.

Hili daraja limejengwa na wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA na limegharimu kiasi cha shilingi milioni 763 kupitia mpango wa serikali wa kupunguza vikwazo unofadhiliwa na Benki ya Dunia.

Nimejaribu kuangalia kasoro kadhaa ambazo zajionyesha wazi katika daraja hilo na baadhi yake ni:

1. Hakuna njia ya waenda kwa miguu jambo linoweza kusababisha ajali.

2. Kingo za pembeni za daraja zimejengwa kimasihara.

3. Daraja halina kingo imara khasa mwanzoni na linapoishia kwa kujazwa tu na vifusi vya udongo ambavyo vitaweza kumomonyoka endapo mvua kubwa itanyesha na kusababisha daraja kubomoka.

4. Daraja halina taa za kutosha (ipo moja tu upande wa kulia mwisho) hata zile za umeme wa jua Solar street lights ambazo ni kwa ajili ya usalama wa daraja, watembea kwa miguu na usalama wa magari na vyombo vingine kama pikipiki zitazopita hapo.

5. Ujenzi wa daraja haujazingatia viwango vya kimataifa na yaonyesha limejengwa kwa mtindo wa bora daraja na sio daraja bora.

6. Daraja limejengwa kihatari mno.

Tunapenda serikali iwajibike kwa kuiona hata ikijitahidi kujenga madaraja mazuri yenye kuzingatia viwango vya kimataifa.

Wahandisi wetu wapo wapi?

Chanzo: Habari leo.

Over to Mr Kavishe.
 
View attachment 3472255
Daraja la Ngara.

Hili daraja limejengwa na wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA na limegharimu kiasi cha shilingi milioni 763 kupitia mpango wa serikali wa kupunguza vikwazo unofadhiliwa na Benki ya Dunia.

Nimejaribu kuangalia kasoro kadhaa ambazo zajionyesha wazi katika daraja hilo na baadhi yake ni:

1. Hakuna njia ya waenda kwa miguu jambo linoweza kusababisha ajali.

2. Kingo za pembeni za daraja zimejengwa kimasihara.

3. Daraja halina kingo imara khasa mwanzoni na linapoishia kwa kujazwa tu na vifusi vya udongo ambavyo vitaweza kumomonyoka endapo mvua kubwa itanyesha na kusababisha daraja kubomoka.

4. Ujenzi wa daraja haujazingatia viwango vya kimataifa na yaonyesha limejengwa kwa mtindo wa bora daraja na sio daraja bora.

5. Daraja limejengwa kihatari mno.

Tunapenda serikali iwajibike kwa kuiona hata ikijitahidi kujenga madaraja mazuri yenye kuzingatia viwango vya kimataifa.

Wahandisi wetu wapo wapi?

Chanzo: Habari leo.

Over to Mr Kavishe.
Tumejenga kama hili kijijin kwa bei nzur kwa kuchangishana
 
Mvua ikinyesha linaweza kwenda, ila hizi ni taarifa zinazoleta taharuki, msizirushe mtandaoni zitaathiri umoja wetu wa kitaifa
 
Dah! Sisi wananchi tumekuwa ni wapumbavu sana. Yaani wezi wanaiba mchana kweupe, tunaishia tu kulalamika! halafu tunafunika kombe.
 
Back
Top Bottom