DOKEZO Hili daraja lilojengwa huko Ngara wengi wasema halijajengwa kwa viwango vinavyotakiwa

DOKEZO Hili daraja lilojengwa huko Ngara wengi wasema halijajengwa kwa viwango vinavyotakiwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
View attachment 3472255
Daraja la Ngara.

Hili daraja limejengwa na wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA na limegharimu kiasi cha shilingi milioni 763 kupitia mpango wa serikali wa kupunguza vikwazo unofadhiliwa na Benki ya Dunia.

Nimejaribu kuangalia kasoro kadhaa ambazo zajionyesha wazi katika daraja hilo na baadhi yake ni:

1. Hakuna njia ya waenda kwa miguu jambo linoweza kusababisha ajali.

2. Kingo za pembeni za daraja zimejengwa kimasihara.

3. Daraja halina kingo imara khasa mwanzoni na linapoishia kwa kujazwa tu na vifusi vya udongo ambavyo vitaweza kumomonyoka endapo mvua kubwa itanyesha na kusababisha daraja kubomoka.

4. Ujenzi wa daraja haujazingatia viwango vya kimataifa na yaonyesha limejengwa kwa mtindo wa bora daraja na sio daraja bora.

5. Daraja limejengwa kihatari mno.

Tunapenda serikali iwajibike kwa kuiona hata ikijitahidi kujenga madaraja mazuri yenye kuzingatia viwango vya kimataifa.

Wahandisi wetu wapo wapi?

Chanzo: Habari leo.

Over to Mr Kavishe.
Kwanza Hilo sio daraja pia wewe una professional Gani ili nijue naongea na wewe. Mambo sio kihisia ,
Mfano unaweza ukanipa viwango vya daraja likoje.
Pia ujenzi wa iyo unajua ni nini kinaangaliwa
 
Washukuru Mungu kwa kupata hata daraja hilo vinginevyo wangeona cha mtema ushuzi
 
. Hakuna njia ya waenda kwa miguu jambo linoweza kusababisha ajali.
Waenda kwa miguu inatakiwa iweje ama idadi yao kwa wastani kwa siku katika mwaka mzima wapewe njia yao,
Unajua AADT ni ngapi kwa iyo njia yenu?
Iyo ni aina gani ya Barabara katika makundi ya Barabara?
Sorry umesema 700m au 7m?
Maana sioni project ya 700m hapo.
Lete hesabu zako za materials, transport, mobilization, demobilization, manpower and professional personnel ni kiasi gani kwa akili yako.

2. Kingo za pembeni za daraja zimejengwa kimasihara
Ilitakiwa ziweje labda Sasa inabidi wafundishe hao jamaa, Lete daraja la ina iyo iyo tuone likoje.
 
Kwanza Hilo sio daraja pia wewe una professional Gani ili nijue naongea na wewe. Mambo sio kihisia ,
Mfano unaweza ukanipa viwango vya daraja likoje.
Pia ujenzi wa iyo unajua ni nini kinaangaliwa
Huna haja ya kutoa povu angalia picha ya daraja (namba 6) la kawaida tu lilojengwa kwa fedha ndogo na kwa ustadi.

Angalia kingo, angalia vizuizi (reinforcements) angalia mawe yalopangwa kuzuia mmomonyoko na daraja kuvnjwa na mafuriko.

Unapojenga iwe nyumba au kitu kama daraja kwanza waweka "impression" kwa mtazamaji, wavutia soko upate zabuni zaidi na mengine.

Hujengi kama watolewa mbio na hujengi bora daraja, wajenga daraja bora.
 
Back
Top Bottom