Wakati tunapoendelea kwenye mageuzi yanayoleta matumaini kwa Tanzania kuna kundi dogo sana linapinga kila kitu kuhusu Mageuzi haya.
Hili kundi lina nia gani na Nchi yetu? Ni akina nani?
Ukitazama hapa JFs kwa mfano kuna ID zisizo 10 ndio zimeshupaza shingo kuhakikisha Reforms za maendeleo hazifanyiki.
Tunawauliza watu hawa wana nia gani na Nchi yetu? Nguvu yao inatokana na nini?
Lakini je hawa watu tangu Miaka ya 90 wamekuwa wakipinga.
Walimpinga Jaji Francia Nyalali
Walimpinga Jaji Mark Boman
Walimpinga Jaji Josef Sinde Walioba
Walipinga Kikosi Kazi cha Prof yule wa UDSM.
Wamepinga matakwa ya Wananchi kwenye maandamano, wamepinga maoni ya Shura ya Maaimam, maoni ya TEC, maoni ya Umoja wa makanisa ya kikristo, wamepinga maoni ya Jukwaa la Katiba Tanzania.
Je hawa watu ni Watanzania kweli? Ninapata wasi wasi mkubwa.
Umewaza kwa uyakinifu mkubwa sana.
Tume zilianza kwa Mwinyi, akaja Mkapa, akaja Kikwete kuhusu mustakabali wa kisiasa na kikatiba wa nchi hii, zote zilileta majibu anuai na baada ya tume hizo kuwasilisha ripoti zao na kusomwa, kila mtu akasema kwamba kwakweli tunaelekea kwenye mwarobaini!
Lakini tume zote hizo majibu yake yakawekwa kapuni!
Na tawala zote zilikuwa na mabunge lakini hakuna hatua ya maana iliyochukuliwa, kwa nini!
Je tume hizo ziliundwa kwa amri ya nani, alikuwa na dhumuni gani, kwa nini tawala zote ziliyatia kapuni mapendekezo yote ya tume hizo?
Je marais wote wanafanana akili na maamuzi yao?
Kwa nini Kikwete alikuja kuvuruga mapendekezo ya Warioba?
Samia alikuwa naibu Spika wa Bunge la Katiba, kutokana na haiba na kauli zake ndiyo zilizomfanya apendwe na Wabunge pamoja na raia.
Leo kashikishwa fupa, kitu gani kimembadilisha na kuonekana huyu ni Samia mwingine na si yule wa Bunge la katiba?
Kwa matukio yote haya, yanaonesha kuwa Rais siyo mwenye maamuzi ya mwisho, yupo chini ya uongozi wa kakikundi flani ka watu kwa ajili ya maslahi yao na siyo kwa manufaa ya wananchi na Rais hawezi kukiuka wala kuwapinga wakitakacho wao.
Iwe ni kuua, kuteka ama kubambikia watu kesi wapinzani, Rais hawezi kuzuia wala kuokoa kwa kutumia maamuzi yake kama mkuu wa nchi na mifano tumeishuhudia.
Ina maana sasa, kundi hilo linaloshikilia maamuzi ya kumuongoza Rais cha kufanya, kamwe haliwezi kukubali mabadiliko yatakayoleta afueni kwa raia wa nchi hii kidemokrasia.
Kama raia tutafunguka kutoka kwenye mnyororo wa kifikra tunaweza kujitambua na kuwa kitu kimoja bila kujali itikadi za kisiasa na kufanya maamuzi magumu sana.
Haiwezekani maoni ya makanisa, wachungaji pamoja na baadhi ya mashehe, wanasiasa wote kwa pamoja na baraza la maboresho ya Katiba kushauri vizuri sana na kwa uadilifu, Rais kawa hasikii maoni ya umma, kwa nini!
Ni kweli hasikii au anakatazwa?
Mjadala huu unaweza kutusaidia kufumbua macho na kupelekea kulifahamu hilo kundi linalotutawala lililopo kisogoni mwa Rais likimuongoza na kumuelekeza cha kufanya.