Zanzibar 2020 Hili la Jecha kuchukua fomu limeitia doa kubwa CCM

Zanzibar 2020 Hili la Jecha kuchukua fomu limeitia doa kubwa CCM

silent lion

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2012
Posts
1,278
Reaction score
1,794
Amani ya Bwana iwe nanyi.

Sote tunafahamu utata mkubwa uloiojitokeza mwaka 2015, na nafasi ya Jecha katika utata huo.

CCM kama chama tawala ambacho kinajinasibu kukubalika na wananchi na ambacho kinda kushinda kwa kura halali, hakikutakiwa kujihusisha na mtu kama Jecha.

Ukila na kipofu usimshike mkono.
 
UVCCM wanajifanya kuwa surprised na JECHA kutoka kwenye makabati ya maCCM kisiwandui kuchukua form za Urais, yani kama vile walikuwa hawajui ni kada… watu wanapolalamikia IMPARTIALITY ya Tume ya Uchaguzi, UVCCM ndio wanaoongoza kutetea… Hata sasa watasema, ni haki yake kikatiba
 
Amani ya Bwana iwe nanyi.

Sote tunafahamu utata mkubwa uloiojitokeza mwaka 2015, na nafasi ya Jecha katika utata huo.

CCM kama chama tawala ambacho kinajinasibu kukubalika na wananchi na ambacho kinda kushinda kwa kura halali, hakikutakiwa kujihusisha na mtu kama Jecha.

Ukila na kipofu usimshike mkono.
Amethibitisha pasipo shaka yoyote ile kuwa yeye kumbe alikuwa ni mwanachama mpenzi wa kindakindaki wa CCM.

Ni makosa makubwa sana kuteua "refa" uwanjani ambaye ni shabiki wa timu Fulani, kwa kuwa ni dhahiri ataminya haki, kama alivyofanya kwenye uchaguzi wa 2015
 
Huyo mzee abarikiwe sana kwa kupoka ushindi.
 
Huo ndio ukomavu wa kisiasa na ukuaji wa demokrasia ndani ya CCM. Ndani ya CCM kila mtu ana nafasi sawa na wenzake hata Kama kaingia Jana.
 
Hakuna nchi yenye watu ma ntindio wa akili kuizidi tanzania duniani.
Hata Zimbabwe ni waelewa mbele ya watanzania.
Nani aliiloga hii nchi?
Kabaka kama jecha aliyekuwa kwenye tume ya uchaguzi na kufanya yale aliyofanya sasa anadhihirisha kwamba yeye ni mwanachama hai wa ccm na watu wananyamaza?
Nailaani ile siku niliyozaliwa Tz na kuitwa mtanzania!!
 
Lini mkawa na akili ? Mgekua na akili msingekubali aya kuendelea

Kama na wewe ni wale wale, basi usisahau kuwaambia wakubwa zako kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho.

Endeleeni tu kutuletea dharau. Muda utakapofika, mtaikimbia hii nchi.
 
Back
Top Bottom