Hili la Jonas Mkude kuingia kambini akiwa kapendeza sio poa kabisa

Hili la Jonas Mkude kuingia kambini akiwa kapendeza sio poa kabisa

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Jana nilipata nafasi ya kuzama Kambini kwa timu ya Taifa.

Nikiwa Bongo mara nyingi napenda kujibanza na watu wa soka ili kujua mambo mbalimbali ambayo kwa namna moja au nyingine siyatambui.

Kwa bahati nzuri/mbaya mwamba mmoja hivi kutoka pande za Msimbazi akaingi akiwa amependeza kinoma. Nadhani aliutumia vyema ule wakati wa alasiri wa siku ya jana kufanya yake.

Labda huenda alidhani ameonja kidogo na hakuna mtu angeshindwa kumtambua, kwa bahati mbaya mwana alionekana dhahiri hata na wachezaji wenzake kuwa Jey yuko pombe.

Mwalimu hakuweza kulitambua hilo mapema ila baadhi ya maafisa wa benchi la ufundi la Stars waliligundua hilo.

Nikaona Nadir Cannavaro akimuita kando na kuzungumza na mkude kwa dakika kadhaa kabla drill ya kupasha misuli haijaanza.

Baadaye nikapewa taarifa kuwa Nadir alikuwa anamsaidia Jey ili hadha ili isije kujulikana kwa Kocha, Nadir akamshauri kuwa ajifanye kama anaomba ruhusa ya kwenda nyumbani ya kuwa kumetokea na dharura.

Jey akasaidiwa na baadhi ya maafisa wengine hadi akapata ruhusu ya kuondoka.

Ni kocha pakee ambaye mpaka sasa hajafahamu kuwa Mkude alikuja kambini amelewa. Baadhi ya viongozi wengine wa benchi hilo hilo hawakupendezewa kabisa kwa Jey kuja amelewa, waliona kama ni kitendo cha dharau na ukosefu wa heshima kwa kazi.

Leo Nikiwa naongea kwa simu na mmoja wa afisa niliyekutana naye jana kambini jana, akanitaarifu kuwa Kocha ameambiwa mchezo wote ulio tokea. Huenda ametonywa na lile kundi dogo ambalo walichukizwa na lile tukio.

Akaongeza zaidi kwa kuniambia kuwa Kocha ameanza kujenga "kutokuwa" na uaminifu na baadhi ya watu katika benchi la Ufundi. Akasema nisisangae kama baada ya game ya Benin kukawa na mabadiliko katika benchi hilo.

Nashauri:- Ni wakati sasa Jonas Mkude asitishe kuichezea Taifa Stars na awape nafasi Vijawa wengine chipukizi.
 
Ulikua unashangaa nini sasa?
Inamshangaza kwa sababu Jonas Mkude ni msakata kabumbu.

Pombe ina hasari nyingi zana kwa mwili wa binadamu ukilinganisha faida kwa mwili.

Hivyo hata mimi sitegemei msakata kabumbu anayejitambua ashiriki katika kitendo kinacho athiri mwili wake ikiwa kazi yake inategemea pakubwa utimamu wa mwili wake.
 
Wachezaji wakubwa wa Uingereza walikuwa walevi mbwa wakiongozwa na steve g na jt
 
Inamshangaza kwa sababu Jonas Mkude ni msakata kabumbu.

Pombe ina hasari nyingi zana kwa mwili wa binadamu ukilinganisha faida kwa mwili.

Hivyo hata mimi sitegemei msakata kabumbu anayejitambua ashiriki katika kitendo kinacho athiri mwili wake ikiwa kazi yake inategemea pakubwa utimamu wa mwili wake.
Kwani ni wachezaji wengine hawanywi pombe mkuu? Au hujawahi kutana nao! Nachojua asilimia kubwa Wachezaji wanavuta sigara na kunywa pombe
 
Back
Top Bottom