Hili la kufungwa barabara limekaaje? Kwa namna hali ilivyokuwa leo kwenye usafiri maeneo ya Posta na Kivukoni mpaka ifike hiyo tarehe 30 tutakuwa hoi

Hili la kufungwa barabara limekaaje? Kwa namna hali ilivyokuwa leo kwenye usafiri maeneo ya Posta na Kivukoni mpaka ifike hiyo tarehe 30 tutakuwa hoi

Half american

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
38,283
Reaction score
97,793
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam imetangaza kuwa Barabara tisa Jijini Dar es Salaam, zimefungwa kwa siku sita kuanzia leo Januari 25 hadi Januari 30, 2025 ili kupisha misafara ya viongozi wanaokuja kutoka nchi mbalimbali kuhudhuria mkutano wa Nishati Afrika.

Taarifa ya Polisi iliyotolewa leo Jumamosi Januari 25,2025 na Kamanda Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Jumanne Muliro, imesema Mkutano huo utakaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Januari 27 hadi Januari 28, 2025, unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya marais 25 na mawaziri 60 kutoka nchi mbalimbali za Afrika ambapo pia bajaji na bodaboba hazitaruhusiwa kuingia katikati ya Jiji katika kipindi chote ambacho mkutano huo utakuwa ukifanyika.

Barabara zitakazofungwa ni pamoja na Barabara ya Nyerere kutokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwenda katikati ya Jiji, Barabara ya Sokoine, Kivukoni na Lithuli kuanzia taa za Gerezani kwenda Hoteli ya Johari Rotana, Hyatt Regency hadi Ikulu; Barabara ya Ohio kutokea Kivukoni kwenda Hoteli ya Serena na Barabara ya Ghana kutokea barabara ya Ohio kwenda Hoteli ya Onomo

Zingine ni Barabara ya Bibi Titi kutokea makutano ya barabara za Ohio na Ally Hassan Mwinyi kwenda Hoteli ya Crowne; Barabara ya Azikiwe kwenda Hoteli ya Four Points, Hoteli ya Golden Tulip City Center na Hoteli ya Holiday Inn; Barabara ya Morogoro kutokea Sokoine kwenda Hoteli ya Tiffany No. 1; Barabara ya Makunganya kutokea Azikiwe kwenda Hoteli ya Tiffany No. 2 na Barabara ya Garden kutokea barabara ya Lithuli kwenda Hoteli ya Southern Sun pamoja na Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa JNICC.
 
Wamekurupuka hawakufanya tathimini ni barabara zipi zifungwe. Mbona ni rahisi kupanga road pattern kwa misafara ya viongozi hao? Hizo siku itakuwa kero kubwa wa wakazi wa jiji la dar, wavumilie tu hakuna namna
Inakua kero sana kuanzia kwa wenye vyombo vya usafiri hadi kwa wasafiri.
 
IMG-20250125-WA0090.jpg
IMG-20250125-WA0091.jpg
 
Wala sishangai kwa waafrika kukurupuka bila maandalizi
Mwingine nae kabeba vifagio kwenda kufagia barabara

Wao walipokuja UK na kupakiwa kwenye mabasi hawakuona traffic zilikuwa zinaenda tu kila mahali?
Yaani siku zote hizo kweli No hurry in Africa
Siku zaidi ya 4 kuanzia leo, hii ndio Afrika.
 
Back
Top Bottom