Uchaguzi 2020 Hili la kuondoa vitambulisho vya machinga umebugi stepu

Uchaguzi 2020 Hili la kuondoa vitambulisho vya machinga umebugi stepu

Mkuu kuna watu hapa kazi yao kupinga kila kitu hata kama kiwe kizuri ni kupnga tu wamesahau wamachinga nao ni wa tz kuna ubaya gani nao wakichangia 20 kwa mwaka bila bugudha yoyote mbona wafanyakazi wanalipa kodi kila mwezi tena wanakatwa moja kwa moja kutoka kwenye mishahara?. Kwanza machinga wenyewe kwa sasa wana amani na kazi zao.
 
Vitambulisho vya machinga ni biashara ya Ikulu na hii lazima lisitishwe! Hatuwezi kuwa na kiongozi asiefata taratibu za nchi, We uliona wapi watu wakifanya biashara barabarani? Maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya soko tameisha? Tusitetee Ujinga ambao hauna mantiki yoyote.Je sheria zinasemaje kuhusu machinga?
Wewe umeajiriwa una ofisi mwacheni machinga aweke biashara yake wateja walipo, wewe Kama unakereka na machinga kafanye shopping mlimani city
 
Mh Lisu katika pitapita yake kasema atafuta vitambulisho vya machinga. Hapa amechemka mwambieni Bora aseme ataboresha usimamizi...
ccm wamefeli kwenye sera.
 
Lissu kunamatamshi mengine anajikaanga mwenyewe.kuna machinga walikua wanalipa ushuru wa miatatu mpaka miatano.kwa kila siku mara mwakamzima huo ushuru unazidi elfu 20.

Sasa sijui Lissu serikali yake akiwa Rais hatoitaji mapato labda.
 
Vitambulisho vya machinga na biashara ndogondogo ilikuwa ni njia moja ya kupata pesa!! Ilikuwa ni “ili usisimbuliwe, tupe 20,000 tukupe kitambulisho”. Mwanzoni ilionekana wenye vitambulisho wasingesumbuliwa - ikawa hivo. Sasa hivi hakuna tofauti kati ya wenye vitambulisho na wasionavyo. WOTE HAWASUMBULIWI!!

Na hii ndio point ya Lissu. Kusumbuliwa au kutosumbuliwa ni swala la utaratibu!! Utaratibu ukiwekwa kuratibu swala hili, hakuna haja ya “kuhonga” ili usisumbuliwe. Hakuna mtu anajua pesa zilitumika kwa mambo gani - japo inaweza kuwa ni jambo zuri sana! Lakini hakuna mtu anajua isipokuwa wanaoamua matumizi yake. Pesa za kuahirisha sherehe za uhuru na mambo mengine ya kitaifa zilielekezwa kwenye mambo wazi - hizi ilikuwaje??

Point ya Lissu ni kuwa hakuna uwazi kuhusu pesa hizo!!
 
Mfano wa inchi inayofata Utawala wa Sheria ni pamoja na raia wake wafate Sheria kanuni na taratibu tulizojiwekea kama Taifa, Machinga anapanga bidhaa zake mbele ya Maduka ya wafanyabiashara wanaolipia Leseni,Kodi ya Pango,Kodi TRA,Usafi wa mazingira, Ulinzi halafu machinga halipii chochote mbele ya Bishara za hao wanaolipa msururu wa kodi Useme ni Sheria? Sheria gani hizo katika Nchi inayoeshimu utawala wa sheria?
Wewe umeajiriwa una ofisi mwacheni machinga aweke biashara yake wateja walipo, wewe Kama unakereka na machinga kafanye shopping mlimani city
 
Mleta mada unaweza kuweka ushahidi kuwa kweli alisema hayo? Yaani taja ilikuwa muda wa saa ngapi, siku gani, tarehe ngapi, sehemu gani. Na aliyasema hayo mbele ya akina nani. Ni kwa nia njema kabisa.
 
Term kitambulisho inawatoa akili mno.

Wewe uliwahi kuwaza kuwa wamachinga watachangia pato la Taifa lao?

Nyie ndo mnaopiga ramli nchi iendeshwe kwa mikopo na misaada ya kipuuzi kutoka nje.

Tutakopa mikopo yenye akili
Tutakusanya kodi
Tutaendesha nchi
Asante sana, Mkuu!
 
Sijaona hata hoja moja ya maana inayotoa mbadala ya hivyo Vitambulisho.

Hao Maofisa walioorodheshwa hapo na Mleta Uzi ni kama Wanyonya damu, ni Wasumbufu hakuna mfano....nina uhakika mnaopinga wengi wala hamhusiki kutoa hizo pesa zaidi ya kulalamika kuwa pesa ni mradi wa Watu.
 
Mfano wa inchi inayofata Utawala wa Sheria ni pamoja na raia wake wafate Sheria kanuni na taratibu tulizojiwekea kama Taifa, Machinga anapanga bidhaa zake mbele ya Maduka ya wafanyabiashara wanaolipia Leseni,Kodi ya Pango,Kodi TRA,Usafi wa mazingira, Ulinzi halafu machinga halipii chochote mbele ya Bishara za hao wanaolipa msururu wa kodi Useme ni Sheria? Sheria gani hizo katika Nchi inayoeshimu utawala wa sheria?
Hakuna machinga anayefata mzigo china ni nyie wenye leseni huwauzia bidhaa na wao kuzitandaza chini ni mwaka Sasa hamna aliyefunga biashara kwa kuzibiwa njia na machinga.
 
kanuni zinazotambua haki za machinga kisheria.
Ndo mnashauriwa kuzitaja sasa (kama mnazo), raisi wenu wa vyuma kashindwa kuzitaja zaidi ya Magufuli na risasi. Angalau nyie wasaidizi wake mumsaidie, muache blah blah...
 
Back
Top Bottom