Hili la ligi ya Mabasi Serikali ilitazame kwa jicho la 3

Hili la ligi ya Mabasi Serikali ilitazame kwa jicho la 3

Hiyo ligi ni ya kichovu afu ya kawaida kabisa. Gari zinatoka saa 9 usiku zinafika Msamvu Moro saa 12 jioni ?! (Zaidi ya saa 12 njiani) zinakaa Bene hotel weee ndio zinatoka tena kwenda Dar zinafika saa 3usiku.. hii ni kuendana na ratiba ya Latra.
Hapo hamna ligi yoyote..maana unaeshindana nae anabanwa na ratiba.. wanachofanya ni kujitahidi tu kuwahi kufika kwa kuvizia nani anashusha njiani Misungwi, Usagara ili umpite..
 
Hizo betring zipo kila Route. Route ya Mbeya-Dar kuna Sauli na Golden Dear. Matrafiki na vyombo vya usalama vinaangalia tu ule upuuzi siku zikichinja watu wote ndio wanajifanya kutia huruma. Kuna siku naenda Mbeya mimi nina V8 ila siwapiti jamaa na mbaya zaidi wanafanya overtaking ya hovyo. Kufika Pale Makambako, nikawashtaki kwa Polisi ile naondoka, jamaa hawa hapa nyuma league inaendelea. Inawezekana hata wale Mapolisi walinitukana huko nyuma. Tuombe Mungu yasiyokee ya kutokea ila vyombo vya usalama vinaona na kunyamaza tu.
 
Back
Top Bottom