Hizo betring zipo kila Route. Route ya Mbeya-Dar kuna Sauli na Golden Dear. Matrafiki na vyombo vya usalama vinaangalia tu ule upuuzi siku zikichinja watu wote ndio wanajifanya kutia huruma. Kuna siku naenda Mbeya mimi nina V8 ila siwapiti jamaa na mbaya zaidi wanafanya overtaking ya hovyo. Kufika Pale Makambako, nikawashtaki kwa Polisi ile naondoka, jamaa hawa hapa nyuma league inaendelea. Inawezekana hata wale Mapolisi walinitukana huko nyuma. Tuombe Mungu yasiyokee ya kutokea ila vyombo vya usalama vinaona na kunyamaza tu.