Hili la mbunge baraza la wawakilishi kuwadharau samaki aina ya Kambale na Sato wa ziwa Victoria lisipite pasipo mjadala. Linatoa picha mbaya

Hili la mbunge baraza la wawakilishi kuwadharau samaki aina ya Kambale na Sato wa ziwa Victoria lisipite pasipo mjadala. Linatoa picha mbaya

" go do more research on this fish, we don't use it" 😁😁
 
Jamani kama taifa tuna kazi ya kufanya kweli kweli.

Wakati viongozi wakuu wa wizara zinazo husika na muungano wakiumiza vichwa kuimarisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar bado kuna wabunge wanaharibu juhudi hizo.

Sikikizeni hapo ili kwa umoja wetu tunajadili.

View attachment 2252519

Huu Si muungano ni uvamizi wa Tanganyika kwa Zanzibar
 
No yuko sahihi japo lugha zake ni za kukosa heshima kwa watumiaji. Mimi mfano ukimiambia nile ngisi au konokono na majongoo bahari au kenge hata kwangu sikukaribishi maana nahisi we hata akili huna so amezungumza kwa mazingira ya Zanzibar. Kwakumsaidia tu Huku bara kunachinjwa punda lkn hatuli punda ila ni biashara wachina for export so hata kahambaleee ni kwa wabara na export
 
Haya wewe unayeijua nieleze iweje Kisiwa kilichozungwa na Bahari wale Kambale wa mtoni kwenye maji machafu au tu waletewe samaki wa kwenye mabwawa maji baridi ?
Huenda hujui ulichoandika; sikulaumu. Wakati mwingine tulia na ufikiri kwanza.
 
Jamani kama taifa tuna kazi ya kufanya kweli kweli.

Wakati viongozi wakuu wa wizara zinazo husika na muungano wakiumiza vichwa kuimarisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar bado kuna wabunge wanaharibu juhudi hizo.

Sikikizeni hapo ili kwa umoja wetu tunajadili.

View attachment 2252519
Sasa ubaguzi wao uko wapi. Au ndio sijaelewa, wao Zanzibar ni nchi kwa mujibu wa karibu yao na uhalisia wa maisha yao na anaongea mambo ya nchini kwao sato na kambale sio samaki wa asili kwao na kifupi hawatakuwa na wapenz kwann serikali itumie pesa vibaya? Hao kambale na sato kambale kuleni ninyi watanganyika. Kwao ni samaki wa ajabu ajabu tu.
 
Huenda hujui ulichoandika; sikulaumu. Wakati mwingine tulia na ufikiri kwanza.

Sasa changu na kolekole wameenda wapi? Kwa nini Kisiwa kilichozungukwa na bahari wale Kambale wa mtoni?
 
Wao hawahitaji Kambale na Sato samaki wa "ajabu ajabu" wao samaki wao ni Changu, kolekole, Nguru, Tasi.

Kambale na Sato hawana soko huko kwao hivyo serikali haina haja ya kutumia Bln of money kuzalisha samaki hao kwani hawatapata soko huko.

Hayo ni maoni yake kama mbunge/muwakilishi wa Wananchi wa huko, shida ni pale anapowaita Kambale na Sato samaki wa "ajabu ajabu" utadhani kwamba anaweza kuumba hata gamba moja tu la Sato!!--- ana kiburi sana huyo.
Mwakishi huyu yuko sahihi sana, bamoja na kutumia luga ya ukakasi,lakini ukweli ni huo.
Zanzibar tumezungukwa na bahari,
Zanzibar haina Maziwa wala mito ya maji matamu.
Zabnzuibar haina soko la Kambale na sato.
Uwekezaji ambao Serikali ingelipaswa kuwekeza ni uvuvi wa Bahari kuu na Vitalu vya Ngisina samaki wa bahareini.
Kiulweli hii ni Miradi ya Kiupigaji hela, na itawawia ghali kuiendesha na uzalishaji utakuwa expensive na hatuna mazingira ya kujenga mabwawa ya aina hiyo yatakayoweza kuleta tija ZNZ.
Hii ndiyo context ya Mwakilishi.
 
Mimi sipingi usahihi wa hoja yake, kinachokera ni njia aliyotumia kuwasilisha hiyo hoja yake, huwezi kuita vyakula HALALI wanavyokula watu kuwa ni vyakula vya "ajabu ajabu" tena kwa ukali na jazba, ni hiyo kauli hasa ndio inayotia doa hoja yake.

Huwezi kupakua chakula safi katika sahani chafu na bado udai kwamba hicho chakula ni safi, chakula safi ni hoja yake na sahani chafu ni maneno yake aliyotumia ku present hiyo hoja.
 
Nasikia kiti moto unakipenda sana
Endelea kusikia, ukishasikia, soma Biblia...

Kumbukumbu la Torati Mlango 14
8 na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse.
 
Endelea kusikia, ukishasikia, soma Biblia...

Kumbukumbu la Torati Mlango 14
8 na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse.
Ushapitwa na wakati wewe kigagula
 
Kuna video moja fupi inazunguka mitandaoni anaonekana mbunge wa baraza la wawakilishi akiwaongelea kwa dharau samaki wa Ziwa Victoria. Anasema wao kwa maana ya watu wa visiwani hawana utamaduni wa kula samaki wa aina hiyo, kwamba isitokee mbegu zao zikawekwa kwenye bahari iliyo karibu na visiwa vya Unguja na Pemba!.

Hii ni kebehi mbovu sana, ina maana watu wa visiwani wanaoishi kule mikoa ya Ziwa Victoria hawali samaki wanaovuliwa kutoka kwenye maji yale!!?. Huku kujiona wa maana kunakojionyesha katika maneno ya yule mheshimiwa kunaleta taswira ya dharau kwa jamii pana ya Tanzania.

Waunguja na wapemba tumeishi nao tangu utoto mwetu, tukasoma nao vyuo vikuu na kufanya nao kazi. Na ninao uhakika vyakula vingi vinavyolisha visiwa hivyo na vile vya Comoro vinatoka huku Bara. Ni mazao yanayolimwa na wakulima wa mikoa ya Bara. Kama familia moja ya Kiembesamaki au Mwanakwerekwe inaweza kula wali unaotokana na mchele wa Mbeya lipi la hatari kwa afya ya familia hiyo iwapo itakula samaki wa maji baridi?.

Mbunge huyo wa baraza la wawakilishi kwa lugha ya kweli isiyo ya kuremba ni kwamba ameropoka, tena bila ya kujua madhara ya kauli yake. Alipaswa kutumia aina ya maneno yasiyoleta ukakasi kwa wavuvi wa Ziwa Victoria na wakazi mamilioni wanaoishi maeneo ya kanda ile. Wabunge kutoka Zanzibar wanaoingia ndani ya bunge la Jamhuri wanakula kila aina ya vyakula ambavyo baadhi vinalimwa na wakulima wa kanda ya Ziwa.

Wapo wazanzibari wengi tu waliokuzwa na Sato pamoja na Sangara kule kanda ya Ziwa, wanaujua utamu wa samaki hao. Hivyo mbunge yule atahadharishwe tu na waungwana kwamba kauli yake ndani ya kikao cha baraza la wawakilishi, inaweza kuwa imekera watu.
View attachment 2253929
Huyo mbunge hana akili za kumtosha.
Anafikiri kama mla urojo.
Na hilo ndio tatizo la makuzi mabaya na ukosefu wa exposure.
Huyo jamaa akienda nchi za nje atarudi na povu akishangaa vinavyoliwa kwingine.

Mtu mjinga aliyejiwekea ukomo wa kufikiri tuna mwacha alivyo.
Let sleeping dogs lie.
 
Usipoteze muda kushangaa watu wasio na visogo

They have no brains
 
Back
Top Bottom