Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?

Hahaaaaaaaaaaa, achana nae,,unaweza ukakwazika ukimsikiliza huyu mtu.kwake Jpm Ni zaidi ya saint!!!
 

Mkuu kwani unafikiri hawajui Rais anamaanisha nini? Wanajua sana - kuali zake zinakuwa grossily misintepreted kimakusudi/delibaretly lengo lao kuu ni kutaka kudhilishia Dunia kwamba kumbe Dk.Magufuli uongozi hauwezi - yaani wanataka kuzuga Watanzania kwamba tulifanya makosa kumpigia kura ya ndio Mh.Magufuli, kwa mawazo yao wanafikiri propaganda zao zinaweza kubadiri mawazo ya wapiga kura come 2020 mtu wao itinge Ikulu kiulaini.

Nasena hivi: kwa mtaji wao iliyo seheni disiformation kuhusu Administration ya Tingatinga na kujaribu ku demonise Dk.Magufuli personally sioni kama mbinu hizo zitawafikisha popote.

Ingawa wanaonekana wako highly organised/determined kupotosha watu - vinara wa scam hii wanajulikana, wakumbuke wenzao wanajua jinsi ya kuwa contain kisayansi.
 
Nilisoma zamani sana Physics, kanuni moja ya mwendo ikisema hivi kama sijakosea : Action and reaction are equal but opposite. Jambazi akijua kama hafikishwi Mahakamani na amezingirwa na polisi au raia halafu ana bunduki yenye risasi sijui kama atajisalimisha hivi kikondoo asilete uharibifu mkubwa.

Wapo watu wamehukumiwa kwa kuua wahalifu mbalimbali wakiwemo majambazi kwa kosa la kujichukulia sheria mkononi.

Huu ni Mtego wa panya, utanasa hata wasio kuwemo. Wapo watakao bambikwa kesi na kuuawa kama Mwangosi ukaambiwa alikuwa na siraha.

Kama Jambazi anaua na wewe raia mwema unaua nani sasa mhalifu? Je tunajenga jamii ya aina gani?
 
mbona raia tunaua wizi vibka kwani hatuvunji sheria?kama tunavunja mbona hatuchukuliwi hatua
mungu aliandika ktk torati ya mussa aliyeua nae awawe hakuna jinsi
 



Ni bora nichekwe kwa kupinga hoja zisizo na afya kwa ustawi wa Taifa letu,kuliko kufurahiwa na kupigiwa makofi kwa "kusapoti" hoja za kujenga viwanja vya kumbukumbu ya push-ups,kujenga sanamu la Diamond,Kuleta Kilimo cha umwagiliaji wa ubuyu,kung'oa matairi ya gari na kuyauza ili askali wetu wapate vijisenti na mengine mengi yanayofanana na hayo.

Endelea kusali "Ritania ya watakatifu" na kumuomba "Mtakatifu wako akuombee".
 
Kwenye waiting list ya U DC atakuweka pale juu kabisa. Ingawaje namna yako ya kupima IQ yachekesha kidogo. Umejiweka kuwa kiwango? Lumumba iko tatizo
 
siungi mkono police kujichukilia sheria mkononi
lakin pia sidhani kama kuna jambazi anayekwenda kufanya uhalifu na silaha ya kutishia anapoacha kufanya mauaji ni pale tu anapofanikisha kazi yake.

amri hii ya raisi ikifanyiwa kazi ipasavyo
bila mizengwe itasaidia kupunguza uhalifu.

ni aibu kwa police kubeba silaha isiyoweza kumsaidia kumnyanga'nya jambazi silaha.
 
Kwa mfululizo wa kauli za rais nimeshamsoma ni mtu wa aina gani. Tulieni baada ya miaka yake mitano tutapata majibu. Anaendesha nchi kwa moyo wake badala ya kichwa.
 

Hawaelewi kwanini TTCL imechukuliwa jumla na simu zote fake zimezimwa, na nini kipo nyuma ya pazia.

Ni aibu sana kwa mtu kama Pasco kuendelea kuja JF kupotosha umma.

Raisi Magufuli, piga kazi mkulu.

Wananchi wa kawaida tupo nyuma yako asilimia 100.
 




Usilete utetezi mwepesi kwenye masuala mazito,hakuna anayepingana na nia njema ya Mh.Rais ya kupambana na uhalifu,tunachopinga ni Lugha na maelekezo anayoyatoa kwa vyombo vyake.

Mheshimiwa M.P.K.Pinda aliwahi"kuchomoka bungeni kwa mwendokasi uliokadiriwa kufikia division 4.30km/saa, akaagiza watakaokamatwa kwa kosa la kuua Albino nao wauwawe,pamoja na kuonesha kuguswa na mauwaji ya ndugu zetu albino,mh.Pinda alipingwa vikali na kwa uungwana wake japo hoja yake aliitoa huku akimwaga machozi mbele ya bunge,lakini aliisahihisha baada ya kuona ilikuwa na mapungufu mbele ya sheria.

Uungwana ni vitendo,kuliko kukomaza shingo kuzitetea kauli zenye ukakasi,ni bora watu wakiri kuwa walipotoka na kutoa nafasi kwa Taifa kuimaliza mijadala hii yenye kuleta utata.

Kuwalazimisha watu wote waitikie "mdundo" wa ngoma(matamko ya serikali) hata pale mdundo huo unapokuwa na tafsiri zenye utata,ni kuwaweka watu kwenye "vifungo vya fikra". Hatuwezi kukubali kutiishwa na kuwekewa mipaka ya ukomo wa fikra zetu kama walivyofanya kwa wabunge wa ccm pale walipowapiga marufuku kutofautiana na hoja za serikali bungeni.Hilo halikubariki.
 
Hapa naona kila polis wote watapandishwa vyeo maana akiona hajapanda na ana siraha piga raia hpa lamcng raia na wale weny tabia ya udokoz kaz kwao
 
Mimi nilidhani dhana ya maboresho ya jeshi la polisi ililenga ktk haya;

1. Jeshi la polisi kufanya kazi yake ya kulinda usalama wa raia na mali zao kwa mbinu za kisasa zaidi

2. Jeshi la polisi kutumia mbinu hizo za kisasa kuzuia uhalifu kabla haujatokea

Kauli ya Mr President ina kasoro na matobo tobo mengi. Nakubaliana na Pasco kuwa kinachobaki ni busara za mapolisi wenyewe kutumia akili zao kuamua huku wakikumbuka kuwa sheria zipo zinazowaongoza kutekeleza majukumu yao

Wakumbuke kuwa kwa mujibu wa katiba yetu ya JMT ya mwaka 1977 mwenye kinga ya kutoshitakiwa ni Rais pekee akiwa madarakani na aachapo madaraka yake.....nyie wengine mapolisi wenzangu sheria za nchi hii zipo na kamwe hamuwezi kuzipiga chenga!!

Huwezi kukomesha uhalifu kwa kutenda uhalifu. Nimesemema sheria zipo na Pasco kashauri vyema sana kuwa, kama Rais JPM anataka kuwalinda hawa aliowapa hii amri batili iliyo kinyume na katiba aliyoapa kuilinda, basi afanye hivyo kwa kutumia "Presidential decree" ambayo hii huwalinda wale wote wanaotekeleza maagizo ya serikali kama hili!!

Kinyume chake hakuna polisi mjinga atakayeamua kuua tu eti kwa kuwa Rais kasema kwa kauli tu za kisiasa za majukwaani na ukaenda mahakamani ukajitetea kwa kusema nilikuwa natekeleza maelekezo ya Rais!!

Nyie polisi wetu nyie, nawashauri muazime busara za kauli hii kutoka kwa Rais mtaafu wa awamu ya nne ndg Kikwete aliyowahi kuitoa wakati mmoja kuwashauri wafuasi wa vyama vya upinzani waliokuwa wakiandamana mara kwa mara kama njia ya kushinikiza mambo flani flani hata pale ambapo jeshi la polisi liliwakatalia. Kwa mtazamo wake Kikwete ni kuwa aliamini wafuasi hawa walikuwaga wanashinikizwa na viongozi wao kuandamana. Alisemaga...

"....akili za kuambiwa changanya na za kwako......" kabla ya kuchukua uamuzi flani

Polisi wetu akili hizi za kuambiwa changanyeni na za kwenu kabla ya kuchukua maamuzi yoyote ktk hili.

Na zaidi sana tekelezeni majukumu yenu ya ajira zenu kwa mujibu wa sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo na mliyopewa ya utekelezaji wa majukumu yenu!!

Vinginevyo kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe
 
  1. Ninamshangaa sana Mpemaanavyoshabikia majambazi nayeye nimojawao nn?? Badala ya kuleta haja maendeleo unakomaa na habari zamajambazi siku wakikutembeleautaelewa vizuri umuhimu wa kauli ya raisi.

    ReportEditDelete
    + QuoteReply
1101112131415
 
Hapa naona kila polis wote watapandishwa vyeo maana akiona hajapanda na ana siraha piga raia hpa lamcng raia na wale weny tabia ya udokoz kaz kwao

Mkuu kumbuka Mapolisi si mazuzu wana akili timamu na weledi wa kujua wafanye nini wahache nini - Polisi wa Taifa letu hawana kanuni ya ku "shoot first and ask questions later" - Polisi wa Tanzania hawana hulka ya Ma-polisi wa Kiyankee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…