Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?

Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?

magufuli alichomaanisha ni kuwa wale majambazi wanaokuwa na silaha na kwenda kuvamia kituo cha polisi polisi achukue tahadhari ya kuanza kumshambulia, binafsi sijaona tatizo hapa, yaani jambazi anapora silaha polisi halafu asiuawe?
 
Katika biblia kuna mwandishi anaitwa Paulo maandiko yake mpk leo inawachanganya wasomi wengi wa biblia na wanazuoni wa elimu Mungu kwakuwa Paulo alikuwa bingwa wa falsafa na aliongea kwa ustadi wa hali yajuu wenye IQ ndogo ni vigumu kumwelewa vivyo ivyo mh Rais wetu ni bingwa wa falsafa watu waropokaji wasiyotakafari kwa kina wanashindwa kumuelewa maneno yake ndiyo maana kila moja anakuja na tafsiri yake. Ni vyema kabla hujaanza kufanya uchambuzi wa maneno ya Dr Magufuli unatakiwa upate tafakuri ya kutosha ili uweze kumuelewa, mh rais aliongelea suala la wanatumia barabara ya mwendokasi watu wakamtafsiri vibaya, juzi kaongelea kuhusu ushirikiano na vyama vya siasa watu wachovu wa fikra wakasema wamezuia vyama siasa kufanya siasa Jana kaongelea mapambano ya polisi na majambazi wamebadilisha kasema majambazi wauwawe. Nadhani sasa tufike wakati tuwe watafakari zaidi kabla ya kufanya uchambuzi. Mungu mbariki shujaa na mzalendo halisi Dr John Pombe Magufuli
Words should be given their literal meaning before going into the intricacies of employing other meanings
 
Si juzi tu kasema anasimamisha vyeo kwa muda kama miezi hivi leo tena vyeo. Halafu huwezi kuwa unapandisha vyeo tu kwa watu wakitekeleza majukumu yao vinginevyo itakuwa kila mtu boss. Na ile dhana ya kubana matumizi imepotea maana cheo ni pesa pia.
 
Mnaogopa nini mjambazi wamejichagulia kazi ya kupora Mali za watu na kuwauwa wakiwa hawana hatia mbona majambazi hawatumii sheria katika kuuwa watu wala hawachaguwi wa kumuuwa badhi ya watanzania ni wa ajabu mnasimama kutetea majambazi bila aibu!!!!!!
 
Una kumbukumbu yoyote juu ya kuuliwa kwa wafanyabiashara watatu wa madini toka Mahenge(hapa soma majambazi)pale Sinza?Pamoja na kazi nzuri ya jeshi letu la polisi ya kukabiliana na wahalifu na uhalifu,lakini yapo makosa mengi ya kiutendaji ndani ya jeshi hilo.

Wapo wengi waliopoteza Maisha kwa kuhisiwa ni majambazi lakini hawakuwa majambazi bali ni Raia wema waliohitaji ulinzi wa jeshi badala ya kuwauwa.Imrani Kombe aliuwawa kikatiri na jeshi la polisi kwa kumdhani ni jambazi,baada ya kutekeleza mauwaji,baadae wakagundua kuwa aliyeuliwa hakuwa jambazi bali alikuwa bosi wao.

Vijana wale watatu wa madini walichomolewa roho zao kwa kudaiwa ni majambazi,kumbe walikuwa ni raia wema ambao walihitaji ulinzi wa polisi badala ya kuzawadiwa kifo na polisi wetu.Tukirudi kwenye magereza yetu,wapo wengi waliofungwa huko kwa makosa ya kusingiziwa,si kila mfungwa aliyepo gerezani alitenda uhalifu,wapo wengi humo ambao hawakupaswa kufikia huko.
Kiongozi wa nchi anapotoa kauli za nama hii alipaswa aangalie na weledi wa jeshi letu katika kukabiliana na matukio ya kihalifu na uhalifu wenyewe,polisi wetu bado wanapungukiwa mbinu za kipelelezi za kubaini uhalifu,walipaswa wajengewe uwezo wa kubaini viashiria vya uhalifu na kuvitumia kuwanasa wahalifu badala ya kuelekezwa kupambana na yeyote watakao muhisi ni muhalifu kama walivyopambana na Imrani Kombe na kuuondoa uhai wake.

Kuwapoteza ndugu zetu kwa vifo vya kikatiri vya jeshi la polisi kwa kisingizio cha kupambana na uhalifu ni jambo lisilovumilika.Kauli ya kumpandisha cheo polisi aliyempora jambazi silaha,inaweza kupelekea ujambazi feki mtu akakamatwa na kushikishwa silaha,kisha akaporwa silaha na kujeruhiwa vibaya nakutangazwa kuwa alikuwa jambazi sugu aliyekuwa anatafutwa kwa muda mrefu kumbe ni uongo ulioandaliwa mahususi ili watu wapandishwe vyeo.

Tuendelee kushangilia hotuba za viongozi wetu,lakini tuchukue tahadhari,unaweza kujikuta ni mwathirika wa kwanza wa harakati za jeshi kutafuta vyeo.Chukua tahadhari,kifo hakina Rufaa ukifa umekufa kama alivyokufa mh.Kombe na wale vijana toka Mahenge.



Tatizo vijana wa Lumumba wengi wao wanakosa hekima kama hizi sijajua wamepatwa nanini!! Maana hoja iliyopo mezani ni sensitive sana kwa mutakabali wa Taifa letu na maisha yakila mmoja wetu lkn wao wanaleta siasa hata kwenye mambo yasiyokuwa ya kiitikadi!! Huwa nafurahia sana ninapopata comments zilizoshiba kama hizi ajabu inakuja mijinga fulani fulani ikiongozwa na tutusa mmoja aitwae lizaboni inaharibu atmosphere humu[emoji15] [emoji15]
 
Unaandika maandishi meengi na marefu wakati ungeweza kuyafupisha tu, Raisi Magufuli anatumia metaphor anachokisema kina mlengwa na mlengwa siku zote huelewa raisi anamaanisha nini, nitakupa mfano Raisi alivyosema kwamba wanaotumia br. ta DART wakamatwe na magari yao yang'olewe matairi sasa hiyo ni metaphor na wahusika walielewa alichomaanisha kwamba wachukuliwe sheria kali lkn watu mkafanya ikawa ishu kuuubwa wkt ni kitu kidogo tu lkn matokeo yake leo hii wanaovunja hii sheria ni wachache na watu wameanza kustaarabika!

Hivyo raisi Magufuli ni kipimo cha IQ TanZania asiyemuelewa ni kwamba IQ yake haitoshi ni rahisi kihivyo tu ndiyo maana unaona watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri kama Mbowe, Msigwa, Sugu &Co. wanapata shida sana kumuelewa raisi anachomaanisha, watu kama ninyi mmezoea mtu awape jibu kwamba 2 +5 =7 lkn akikwambia kinyume na hapo unashindwa kupata jibu na ndiyo maana mnakuja na tafsiri zenu za ajabu ajabu lkn leo hii ukienda kuongea na wahusika wakuu wa Askari wetu watakwambia Raisi alichomaanisha, na kazi itafanyika na matokeo yataonyekana wote tutakuwa mashahidi!
Well said mkuu..
Comment Yako inafaa iwe Uzi mkuu...
Point tupu..shukrani
 

Wanabodi,

Wewe kama mwana JF, unapata an added advantage to be the first to know, ambapo leo katika tukio la maboresho ya jeshi la polisi, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais, Dr. John Pombe Magufuli, ametoa kauli kwa kutumia fasihi, ambapo ameliamuru jeshi la polisi, kukabiliana na majambazi wenye silaha kwa "kuwanyang'anya silaha kwa kutumia mbinu za medani, (kivita) (MM) ambazo hutumiwa na majeshi wakati wa vita, ambapo kazi huwa ni moja tuu, kumteketeza adui!.

Amri hiyo kwa Jeshi la Polisi, inamaanisha, Polisi hawahitaji tena kuwakamata majambazi wanaotumia silaha, bali kukabiliana nao kwa kuwaua papo kwa papo, na polisi wataofanya mauaji hayo ya kuwauwa majambazi hayo papo kwa papo bila kuwapeleka mbele ya vyombo vya sheria, hawatafikishwa tena mahakamani, kama zamani, bali sasa watapandishwa vyeo!.

Agizo hilo limepokelewa kwa shangwe na makofi kwa kila aliyekuwe pale.

Rais huku akisema kwa msisitizo kwa kutumia fasihi ya "kuwanyanganya silaha", kwa vile majambazi wanatumia silaha, zenye risasi kufanya ujambazi, na jeshi la polisi nalo wanazo silaha zenye risasi, haoni kwa nini majambazi hayo yasinyang'anywe silaha zao!. Namna pekee ya kunyanganya silaha jambazi mwenye silaha, ni kumalizana nao, papo kwa papo!.

Sina shaka kabisa na nia ya dhati ya rais Magufuli, kutoa amri, hiyo, kufuatia nchi na wananchi kuchoshwa na vitendo vya ujambazi kuongezeka, hivyo majambazi wakijua kuwa wakikamatwa watauwawa right away, then, amri hii badala ya kupunguza ujambazi wa kutumia silaha, ndio kwanza utaongeza impunity kwa majambazi wanaotumia silaha, na wakati huo huo kuligeuza jeshi letu la polisi kugeuka Gestapo!.

Sio majambazi wote wanaotumia silaha, huzitumia silaha hizo kufanyia mauaji!, sio silaha zote zinazobebwa zinakuwa loaded!, wengine huzitumia kutishia tuu, lakini hawana nia ya kufanya mauaji, na kuna wengine hubeba silaha ambazo hazina risasi, na wengine hutumia toy pisto!,na majambazi wengine, hubeba silaha, na ziko loaded, lakini hawafanyi mauaji baada ya kupata walichotaka!, lakini kufuatia amri hii, hao majambazi wenye huruma na maisha ya watu, hawatakuwa na huruma tena, na kama polisi ndio kwanza wamekuwa licenced to kill kwa mtindo wa MM, then every encounter ya polisi na majambazi, tutegemee nothing, no justice but blood bath!.

Tanzania ni nchi ya kidemokasia inayofuata katiba yenye kuzingatia haki na utawala wa sheria!, amri kuu ya kwanza ya haki, ni "no one is condemned unheard", yaani hakuna mtu atakayehukumiwa bila kusikilizwa!. Amri hii ya rais, imewapa mamlaka polisi, sio tena kuchunguza, kukamata na kuwapeleke majambazi wanaotumia silaha, mbele ya sheria, bali sasa polisi hawana tena haja ya kukamata na kufanya uchunguzi, bali kukitokea tuu tukio la uhalifu wa kutumia silaha, polisi wamepewa mamlaka kuwa ni wachunguzi, prosecutors, mahakimu tena kwa kutoa "capital punishment", na hakuna tena haja ya kumsubiri rais kuzisaini hizo hati za capital punishment, bali, wao wenyewe kutumia MM, kuitekeleza adhabu ya kifo, na baada ya hapo kusubirria kupandishwa vyeo!. Just imagine mashindano ya kupanda vyeo miongoni mwa polisi wetu!.

Kama wanasheria wetu, hawatashitushwa na amri hii ya rais, nitaamini sasa Watanzania wameanza kumwelewa rais wetu, na ukiisha elewa, huna haja ya kuhoji!.

Angalizo: Sitetei vitendo vyovyote vya uhalifu wa aina yoyote, bali natetea utoaji wa haki!, hata jambazi anayetumia silaha, anastahili kutendewa haki!. Natolea mfano wa nchi mbili za Maekani na Uingeeza. Miaka ya nyuma nchi zote hizi zilikubwa na vitendo vingi vya mauaji. Uingeeza ikafuta adhabu ya kifo!, vitendo vya mauaji, vikapungua kwa kiasi kikubwa!. Maekani ikaendelea na adhabu ya kifo, vitendo vya mauaji bado vimeongezeka!.

Amri ya kuwaua majambazi papo kwa papo, haitapunguza ujambazi, bali itawafanya hao majambazi ndio kugeua wauwaji wakuu, kwa hoja za "ama zao, ama zetu" na kwenye tukio lolote la ujambazi wa kutumia silaha, polisi wakitokea, sasa sio tena kutuliza amani bali kufanya a blood bath!, hivyo polisi sasa pia watakuwa ni target ya majambazi!.

Kwetu sisi waandishi, ikitokea polisi wakakutana na gun mike, au boom mike, au hata kamera wakaiona ni kama sihaha!, kama ilivyotokea mwa Daudi Mwangosi!, askai mhusika, atapandishwa cheo!. Kama wale vija wa Zombe, sasa watawadiwa vyeo!.

Huko nyuma niliwahi kushauri, kama katiba ni kikwazo, rais Magufuli, aiweke pembeni katiba na badala yake atawale kwa kutumia 'presidential decrees' tuu!. Hivyo kwa amri hii ya polisi kuua majambazi papo kwa papo, kama mahakama ni kikwazo, pia anaweza kuiweka pembeni, na kuwatumia polisi kutoa hukumu za kifo cha papo kwa papo, tena hili litaokoa fedha nyingi sana, maana majaji wa mahakama zetu, wanahudumiwa kwa gharama kubwa sana!.

Wasiwasi wangu kwa amri kama hizi, sio ili kuokoa maisha ya majambazi wanaotumia silaha, au kuwaacha tuu majambazi wanaotumia silaha kuua, lakini wao kuuliwa tuinawatetea!, no!, wasiwasi wangu ni utekelezaji wa amri za aina hii, zisije kuwa kwa majambazi ni mwanzo tuu, baadae amri kama hizi za 'kinyemela' zikaelekezwa kwa makundi mengine, yanayoonekana ni kero!.

Mwaka 1976, kulifanyika mauaji ya wazee waliokuwa wakituhumiwa kuwa ni wachawi. Serikali kupitia waziri wa Mambo ya Ndani kipindi hicho, Ali Hassan Mwinyi Mwinyi, kupitia Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mwanza, chini ya RC Peter Kisumo, RSO, RPC, DSO, na OCD wakadhamiria kwa kauli moja kukomesha vitendo hivyo kwa hizo hizo MM alizoamrisha Magufuli zitumike!.

Katika Mahojiano, yaliyoendeshwa eneo la Kigoto, watuhumiwa wawili, Masanja Makula Mazengenuka, na Isaack Mwanamkoboko, walipoteza maisha!.

Mwalimu Nyerere alikasika sana, Waziri Mwinyi, IGP, Pundugu, Director wa TISS Mzena, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Kisumo, RSO, RPC, DSO na OCD wote wakastaafishwa kwa manufaa, na wengine kupandishwa kizimbani, ambapo wote walifungwa, isipokuwa mshtakiwa Mzee wangu, tena aliokoka kwa vile tuu alikuwa anatetewa na wakili Murtaza Lakha!.

Utendaji wa Jeshi la Polisi unaongozwa na kitu kinachoitwa Police General Ordes ambacho tumekirithi kutoka kwa Waingereza kama tulivyorithi sheria zetu mbalimbali, ambazo zina maelekezo yote ni kwenye mazingira gani polisi anaruhusiwa kutumia silaha kuwadhibiti wahalifu na kuna polisi maalum wa kazi hiyo wanaoitwa snipers au wadunguaji, ambao wana shabaha na uwezo wa kulenga maeneo rasmi ya kulenga ili kumdestabilize mhalifu kwa lengo la kumkamata lakini sio kwa lengo la kumua!. Agizo la jana la Rais Magufuli, ni kuwaelekeza polisi kuua tena kwa haraka bila kuchelewa, na sasa kwa kila mauaji ya polisi, polisi hao badala ya kupandishwa kizimbani, sasa watapandishwa vyeo!.

Japo lengo la agizo hilo la rais, amelitoa kwa dhamira njema,(in good faith), lakini utekelezaji wake, unaweza kuligeuza jeshi letu la polisi kugeuka Gestapo!, na hata Adofu alipoanza, alianza hivi hivi kwa kuwa a populist leader, anayeshangiliwa sana na umati wa watu!, ni baadae sana, ndipo watu wakaja kugundua, by that time, it was too little too late, wakaishia kujuta!, kwa upande wetu, chonde chonde twendeni taratibu jamani, tufungue macho mapema before it is too late, tusije kujuta!.

Jumamosi Njema.

Pasco
Rejea.
Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know ...
IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality
Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa .
Simshangai Pasco wa JF tu; hapana, nawashangaa waandishi wote wa ..

Hili ni jema maaana majambazi hawana nia nzuri wanapotaka kumuibia mtu wanakuja kwa kuua kabisa......so kama wana siraha wanyang'anywe harakaharaka na police atakayefanikisha apandishwe cheo tu!
Ngoja tuone.
 
Hakuna anaetetea majambazi hofu yetu kubwa ninamna jeshi letu litakavyoitumia hiyo opportunity kujinufaisha kwa kutenda kinyume na maagizo ya Rais maana uzoefu unaonesha kwamba polisi huwa natabia zakuwabambikia watu kesi za ajabuajabu ambapo hata muheshimiwa Rais amewahi lizungumzia hadharani, mm binafsi nalaani kwa nguvu zangu zote mauaji ya polisi wetu pamoja na raia wasio nahatia lkn kuruhu polisi kuua bila taratibu watu wengi wataguswa na hili either direct au indirect
 
Mimi nadhani IGP hatoshi kwenye nafasi yake, maana tumekuwa na matukio ya ujambazi kila kukicha bila njia stahiki za kukabiliana na waharifu na vile vile alikuwa anacheka cheka tu wakati rais anaongelea juu ya kuwanyang'anya majambazi silaha, sasa sijui kitu gani kilikuwa kinamfurahisha wakati kuna askari kibao tu na raia wamepoteza maisha kwa sababu ya majambazi. Mbona kipindi cha Mrema aliweza japo kupunguza?? Labda tusubiri Mwigulu. Ila kwa mtizamo wangu, Paul Makonda alifaa nafasi ya uwaziri wa mambo ya ndani.
😀😀 ina maana makomda ana uelewa zaidi ya mwigulu? Huu sasa utani jamani
 
Mnaogopa nini mjambazi wamejichagulia kazi ya kupora Mali za watu na kuwauwa wakiwa hawana hatia mbona majambazi hawatumii sheria katika kuuwa watu wala hawachaguwi wa kumuuwa badhi ya watanzania ni wa ajabu mnasimama kutetea majambazi bila aibu!!!!!!



Hoja zilizopo kwenye huu Uzi wa mkuu Pasco zinakuzidi "kimo cha fikra",hata ukichuchumia au kupanda juu ya stuli,bado hutoweza kuzifikia. Pasco ametumia fikra za juu sana kufikisha hoja yake hapa jukwaani.

Kwanza una umri gani? Nisije nikapoteza muda kubishana na mtoto.Lakini ngoja nikupe" benefit of doubt" kuwa wewe ni mtu mzima.Unakikumbuka vema kisa cha Mauwaji ya Mh.IMRAN KOMBE? Mh.huyu(Mungu amrehemu)aliuwawa kikatili na jeshi letu tukufu la polisi kwa kuhisiwa kuwa ni jambazi.Marehemu Kombe hakuwa mtu kapuku asiyefahamika kiasi cha polisi kutomfahamu na kupelekea kumuhisi ni jambazi.Alikuwa ni kiongozi Mwandamizi wa vyombo vyetu vya ulinzi,kama intelijensia ya jeshi letu ilishindwa kumtambua bosi wao(Marehemu Kombe) na kuishia kumuua kikatiri sana kwa kumuhisi ni jambazi,jiulize hali itakuwaje kwa makapuku kama Mimi na wewe tusiofahamika popote chini ya amri hii dharimu na uchu wa kupandishwa vyeo si tutauliwa makumi kwa maelfu?

Hatuyasemi haya kwa bahati mbaya,pamoja na nia njema ya Mh.Rais na kuonesha kukelwa na vitendo vya kihalifu,bado hakupaswa kutoa maagizo ya aina ile kwa jeshi letu la polisi lenye sifa ya "kutii bila shuruti" amri za kisiasa hata kama amri hizo zinaenda kinyume na katiba yetu.

Ni vema kile kilichoitwa "maboresho kwa jeshi letu" kingejikita katika kuwajengea uwezo wa kiintelejensia ya kisasa zaidi na kuachana na intelijensia za kuzuia shughuli za kisiasa za washindani wa serikali.Kauli za kuwahimiza polisi kumvamia mtu bila weledi,kumpola silaha au kung'oa matairi ya Gari na kuyauza hata kama tunaozipinga tunaonekana tuna I.Q ndogo,bado si kauli zilizopaswa kutoka kwenye kinywa cha kiongozi wetu.Masikio yetu yanapata shida kuamini kama yalichokisikia kimetoka kwa kiongozi au kwa mtu aliye pembeni yake?

Hii ni nchi yetu sote,hakuna anayetetea uhalifu,ila tunashauli uhalifu ukomeshwe kwa mbinu sahihi na si kutumia uhalifu kupambana na uhalifu,hilo halikubariki.Tusipoyakemea haya huko tuendako tunaweza kushuhudia viongozi wetu wapendwa ambao baadhi yetu tumeshawaingiza kwenye "orodha ya Sala za Ritania ya Watakatifu" wakikumbana na mkono wa sheria kwa kupelekwa ICC wakikabiliwa na mashitaka ya kuchochea uvunjifu wa haki za kibinadamu.Kitendo hicho cha "Mtakatifu wetu" kupelekwa ICC kinaweza kuikwaza imani yetu.Hatutaki tufike huko.
 
KATIKA YOTE TUSIBIRI KWANZA MZIGO HUO UANZE NDUGU ZANGU TUKIPATA MAJIBU YA HILO KUWA LINA FAIDA AU HASARA TUTAHAILISHA KAMA VILE ULE MZIGO WA MSOSI MUHIMBILI SIMPLE TU.SERIKALI NI SIKIVU SANA NAAMINI HIVYO NA INAJALI WANANCHI WAKE.PIA MSIMLAUMU SANA MTOA MADA...AMETOA HISIA NA MAWAZO YAKE KAMA VILE MKUU WA KAYA ALIVYOSEMA KWA HISIA.ILA SASA"UKIONA MAJAMBAZI WAMEVAMIA SEHEMU,UKAAMBIWA LALA CHINI..LALA HARAKA SAANA NA USIJE JISHAURI WALA KUJIFANYA MASTER"HIKI NI KIPIMO KIKUBWA SANA,TUTAJUA KUWA USAHIHI UPO WAPI PINDI TU MATUKIO YAKIANZA.NAMALIZIA PIA UKISIKIA TENA KUNA MAJIBIZANO YA RISASI BAINA NA NDUGU HAO NA ASKARI WETU PIA JIFUNGIE HARAKA SANA.SIOMBI NACHOWAZA KITOKEE ILA KILA KINACHOBANWA SAANA SANA KINA NAFASI PIA YA KUJIACHIA."KILA KITU NI SAWA TU"
Well said Mkuu na quote usemi wako tena "Kinachobanwa sana sana kina nafasi ya kujiachia". Maji ya kipanwa sana uwezekano wa kupasua pipe ni mkubwa. Uhuru ukibanwa sana uwezekano wa kutafuta namna ya kuwa huru utatafutwa kwa nguvu zote hata kwa kuruka ukuta. Hongera kwa maneno ya busara.
 
mi nadhani kwa kauli hii ya rais, hakuna haja ya magereza yetu kujaa majambazi nao wafumuliwe risasi tu...Mana wakirudi mtaani na hii hali ya uchumi itakuwa shida mpya, pia kubana matumizi ya magereza yetu.
 
Hoja zilizopo kwenye huu Uzi wa mkuu Pasco zinakuzidi "kimo cha fikra",hata ukichuchumia au kupanda juu ya stuli,bado hutoweza kuzifikia. Pasco ametumia fikra za juu sana kufikisha hoja yake hapa jukwaani.

Kwanza una umri gani? Nisije nikapoteza muda kubishana na mtoto.Lakini ngoja nikupe" benefit of doubt" kuwa wewe ni mtu mzima.Unakikumbuka vema kisa cha Mauwaji ya Mh.IMRAN KOMBE? Mh.huyu(Mungu amrehemu)aliuwawa kikatili na jeshi letu tukufu la polisi kwa kuhisiwa kuwa ni jambazi.Marehemu Kombe hakuwa mtu kapuku asiyefahamika kiasi cha polisi kutomfahamu na kupelekea kumuhisi ni jambazi.Alikuwa ni kiongozi Mwandamizi wa vyombo vyetu vya ulinzi,kama intelijensia ya jeshi letu ilishindwa kumtambua bosi wao(Marehemu Kombe) na kuishia kumuua kikatiri sana kwa kumuhisi ni jambazi,jiulize hali itakuwaje kwa makapuku kama Mimi na wewe tusiofahamika popote chini ya amri hii dharimu na uchu wa kupandishwa vyeo si tutauliwa makumi kwa maelfu?

Hatuyasemi haya kwa bahati mbaya,pamoja na nia njema ya Mh.Rais na kuonesha kukelwa na vitendo vya kihalifu,bado hakupaswa kutoa maagizo ya aina ile kwa jeshi letu la polisi lenye sifa ya "kutii bila shuruti" amri za kisiasa hata kama amri hizo zinaenda kinyume na katiba yetu.

Ni vema kile kilichoitwa "maboresho kwa jeshi letu" kingejikita katika kuwajengea uwezo wa kiintelejensia ya kisasa zaidi na kuachana na intelijensia za kuzuia shughuli za kisiasa za washindani wa serikali.Kauli za kuwahimiza polisi kumvamia mtu bila weledi,kumpola silaha au kung'oa matairi ya Gari na kuyauza hata kama tunaozipinga tunaonekana tuna I.Q ndogo,bado si kauli zilizopaswa kutoka kwenye kinywa cha kiongozi wetu.Masikio yetu yanapata shida kuamini kama yalichokisikia kimetoka kwa kiongozi au kwa mtu aliye pembeni yake?

Hii ni nchi yetu sote,hakuna anayetetea uhalifu,ila tunashauli uhalifu ukomeshwe kwa mbinu sahihi na si kutumia uhalifu kupambana na uhalifu,hilo halikubariki.Tusipoyakemea haya huko tuendako tunaweza kushuhudia viongozi wetu wapendwa ambao baadhi yetu tumeshawaingiza kwenye "orodha ya Sala za Ritania ya Watakatifu" wakikumbana na mkono wa sheria kwa kupelekwa ICC wakikabiliwa na mashitaka ya kuchochea uvunjifu wa haki za kibinadamu.Kitendo hicho cha "Mtakatifu wetu" kupelekwa ICC kinaweza kuikwaza imani yetu.Hatutaki tufike huko.

Nasikitika kuona watanzania wengi hawana mtazamo,unaweza ukaongea kijiona una I.Q nzuri,kumbe walioko pembeni wanakucheka
Kwa ujumla watu wengi hamjui dunia imefikia wapi mpaka sasa,na hamjui kwanini kunamaboresho ndani ya jeshi la polisi na vilevile hamjui hali ya hewa iliopo ndani ya hii nchi,nikuache kama ulivyo nisije nikalala mimi.
 
Acheni kuingiza siasa kwenye maisha ya watu kama rais anatoa taMAILko kama lenye kulenga kulinda usalaama wa raia harafu mnaleta siasa. Kwahiyo pasco unashabikia majambazi au nawewe ni moja wao nn?? Kama hawajahi kukuvamia hawa watu hutajua uchungu ila wakikutembelea cku moja utajua umuhimu wa kauli ya raisi
 
Katika hili,ni vema kila anayefahamiana na jambazi
amshauri abadilishe mbinu ya kupata pesa.
sikubaliani na yeyeyote anayesema jambazi ana huruma(Tafuta maana ya jambazi kwenye kamusi).

Huruma si kuishia kutoua,kuna vifo vingine vinavyotokana
na madhara uliyosababishiwa na jambazi kukufanyia ujambazi.
mfano ni kukopa fedha benki na jambazi akakupola pesa hizo
ila akakuacha hai.Hujafa kwa risasi ila unakufa kwa presha ya nyumba yako uliyoweka
bond kuuzwa kwani fedha uliyokopa hukufanyia biashara uliyokusudia.

Polisi naamini mmemuelewa rais,wanyanganyeni majambazi silaha HARAKA.
wakiwapa silaha haraka wa hiari yao,zichukueni.Wakiwanyima wanyanganyeni msisahau neno "HARAKA"

Mwisho nawakaribisha wale waliojihusisha na ujambazi
njooni tukalime,mbona poa tu na maisha yanaenda
msisubiri kunyanganywa silaha HARAKA,Hii inaweza kuwaletea madhara.
 
Mimi nadhani IGP hatoshi kwenye nafasi yake, maana tumekuwa na matukio ya ujambazi kila kukicha bila njia stahiki za kukabiliana na waharifu na vile vile alikuwa anacheka cheka tu wakati rais anaongelea juu ya kuwanyang'anya majambazi silaha, sasa sijui kitu gani kilikuwa kinamfurahisha wakati kuna askari kibao tu na raia wamepoteza maisha kwa sababu ya majambazi. Mbona kipindi cha Mrema aliweza japo kupunguza?? Labda tusubiri Mwigulu. Ila kwa mtizamo wangu, Paul Makonda alifaa nafasi ya uwaziri wa mambo ya ndani.
Siku zooote unaongea pumba na kutetea uozo, lakini kwa hili, wow wow wooow, umenena point sana
 
Huyu jamaa vp au na ww jambaz nn unatetea upumbavu kwan wamekosa kaz za kufanya mpaka wapole raia Mali zao safi jpm nikuwagonga tu maana hamna namna na yeyote anayetetea mawili ajui uchungu wa kuibiwa au yeye mwenyewe mwizi
 
Majambazi sahvi ni mwendo wa kupigwa shaba tu,mleta mada hii elewa tangia kipindi cha nyuma polisi wamekuwa wakiwaua wale majambazi sugu....kwa siri Ila mains sasa magu kawapa green light polisi ya kuwashugulikia majambazi
 
Back
Top Bottom