Alwayz on top
JF-Expert Member
- Jun 5, 2012
- 706
- 268
Mungu amuweke Shekhe ponda issa ponda..
Mola amhifadh kila ajae na Shari aivunje yake dhamiri..
Amiin amiin
Mola amhifadh kila ajae na Shari aivunje yake dhamiri..
Amiin amiin
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yapi ambayo Tundu Lissu ameyaeleza kwa waislamu hadi waislamu wampigie kura? au kuhusu hao masheikh wa uamsho?
Mkuu mimi siwezi kuendelea kufanya debate na wewe bhana maana naona umeegemea kwenye mfumo wa dini zaidi kuliko siasa za dunia zinazotuongoza.Thank you very much
Waislamu wakisema Rais mkristo anawafanyia waislamu dhulma tunatoa vielelezo mfano mkapa aliua mamia ya wapemba na waumini wa mwembechai msikitini
Kweli mashekh wa muamsho walikamatwa na SMZ 2014 kule Zanzibar kabla huyu kafiri haja kua Rais lakini Mara baada ya yeye kua Rais akaagiza waletwe Tanganyika ili aweze kuwatesa bila huruma na hao ni 72 tu
Sisi tunazungumzia mashekh wengine zaidi ya 200 ambao wamekamatwa kuanzia mwaka 2016 wakati kaffir tayari ni Rais
Kuhusu BAKWATA ni wanafiki wanafanya ubadhirifu Mali za waislamu ulisema kidogo wanakubambikizia kesi ya ugaidi
Je wajua miaka mitano ya kafiri watanzania wengi wamekamatwa kwa tuhuma za ugaidi kuliko hata Afghanistan!!!
Ndugu zetu wanateswa Sana kwenye magereza bila kufikishwa mahakamani
Huyu kafiri anachuki Sana na anatuchukia bila sababu
Tundu Lisu ameahidi katiba mpya, ndio muarobani wa kero zote.Tundu Lissu amezungumzia kuhusu mfumo kristo au bado? maana haya ndio mambo ambayo waislamu wamekuwa wakiyalalamikia miaka kwa miaka kabla hata hilo la masheikh wa uamsho.
Ni muhimu kuyajua haya ikiwa anahitaji kura za waislamu.
Ndio serikali ya awamu ya tano inavyoendeshwaMudawote mpumbavu muda wote. Awe kaburini kisa kikiwa kutofautiana na wewe mtizamo tu au kuna jingine?
Wewe huna dini ungekuwa muslim usingesema unachokisema sisi waislamu tunachukia kitendo hicho na tunakipinga kabsaaaWaislamu wote na hata sisi tusio na dini tunamuelewa shehe Ponda.
Shehe ponda anawakilisha mawazo ya waislamu wote.
HAKI NA UHURUYapi ambayo Tundu Lissu ameyaeleza kwa waislamu hadi waislamu wampigie kura? au kuhusu hao masheikh wa uamsho?
Hakuna wakuishinda CCM na wala atokuja kutokea CCM chama kubwa kama mlishindwa 2015 amtoweza miaka yoteeeNdio serikali ya awamu ya tano inavyoendeshwa.
Tunakwenda kumalizana nao tarehe 28, zimesalia siku chache tu kuondowa utawala wa Magufuli.
Hata ukimuangalia wakati anaongea kuna wakati alikuwa anataka kucheka kudhihirisha wakisemacho siyo sawa.Sasa mtu kama Sheikh Kipozeo naye ni wa kumtilia maanani yeye kazi yake kuzungumzia makalio ya Wanawake tu
Hawa masheikh wanaoongozana za Alhady shida tupu.
Nimesikia Alhady ni qaumu luut.
Je ni kweli?
Mkuu hii google translator imegoma kuitafsiri hii "qaumuHawa masheikh wanaoongozana za Alhady shida tupu.
Nimesikia Alhady ni qaumu luut.
Je ni kweli?
Hoja haina mashiko ndio maana viongozi wenu wa CCM hawathubutu kuitumia..katiba mliyotunga inalinda faragha..Ni Lissu mwenye mchezo huo yy na Amsterdam
Kawaambie watu waliopoteza Familia zao kwa sababu ya watu wasiojulikanaAnayeipenda Tanzania na anayeipenda imani yake, ni lazima apende kutenda haki. Kama unaipenda Tanzania, ni lazima upiganie haki za makundi yote katika jamii yetu.
Kama wewe ni mkristo, unaipenda imani yako, basi hakikisha imani nyingine zote zinatendewa haki. Amani, furaha na utulivu wako unategemea zaidi amani, furaha na utulivu wa wanaokuzunguka. Kama unaipenda sana CCM, upiganie haki ya vyama vingine vya siasa. Amani na utulivu wa CCM utategemea jinsi vyama vingine vinavyotendewa haki.
Kosa kubwa alilolifanya Magufuli mara baada ya kuapishwa kuwa Rais mwaka 2015 ni kuamini kuwa kuyanyima haki baadhi ya makundi na vyama vya upinzani, ndiyo kutampa utulivu na urahisi wa kutawala. Jibu amelipata. Utawala wake ukaishia kulalamikiwa, kupingwa na kulaaniwa ndani na nje ya nchi. Nanukuu maneno ya Gavana yule wa Kenya, "utawala wa Maguguli umekuwa aibu kwa Afrika nzima".
Tukitaka tuishi kwa amani, furaha na upendo, siku zote, kila mmoja atende haki. Rais Magufuli inaonekana hajajifunza chochote na wala hajabadilika. Kwenye kampeni hizi zinazoendelea, bado anaongelea kuendeleza utawala wa kibaguzi na upendeleo. Huyu ni adui wa Taifa. Mtu wa namna hii, anaweza kuja kuliangamiza Taifa. Yeye bado anaongelea eti watu wasipomchagua mgombea wa CCM, watanyimwa miradi ya maendeleo! Kama mtu ametamka hivyo wazi, kweli kuna haja ya kumpa kura mtu wa namna hiyo? Huyu anaelewa juu ya haki ya raia kuwachagua viongozi wanaowataka? Huyu anaelewa juu ya kiapo cha Rais cha kuwatendea watu wote haki bila ya ubaguzi wa namna yoyote ile?
Naamini CCM, kwa kadiri ya katiba yetu ya nchi, ina mgombea mbaya kuliko wote.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mimi siwezi kuendelea kufanya debate na wewe bhana maana naona umeegemea kwenye mfumo wa dini zaidi kuliko siasa za dunia zinazotuongoza.
Kuna vitu vingine vinahitaji uelewa wa kawaida, kwa mfano suala kama la mkapa kuua watu pemba 2001 sidhani kama linahusiana na uonevu wa uislam,labda ni wewe ndiyo unaona hivo ila mimi naona yalikuwa matukio tu ya kisiasa kama matukio mengine wala haihusiani na uonevu dhidi ya waislam,Labda kwa sababu yalitokea eneo ambalo wakaazi wengi ni waislam basi wewe ukadhani walengwa walikuwa waislam ila si kweli na mkapa aliwahi kuomba msamaha kuhusu hilo tukio maana lilimuyumbisha kisiasa pia.
Ishu ya mashehe kukamatwa kamatwa inabidi uwaulize mashehe waliobaki uraiani kwamba kwanini wenzetu wanakamatwa kamatwa sana nadhani watakupa majibu sahihi ila si hayo yako iliyonayo kichwani ya uonevu au kukwamisha uislam usiende mbele, si kweli kabisa hapo.
Alafu cha mwisho huwezi kumwita Rais wetu "Kafiri" bhan, sidhani kama ni jina zuri sana inabidi umtake radhi Rais wetu.
Qaumu luut ni watu wa sodoma na GomorrahMkuu hii google translator imegoma kuitafsiri hii "qaumu
Luut ,ifungue ustaadh.
Sheikh Ponda kamaliza kila kitu,hao vibaraka wa watawala wajiandae kupata kile walichojiandalia
Comparative religions, we unatuletea mihadhara kwenye nchi ambayo haina udini.Kwenu Masheikh na wahadhiri wetu
Nawasalimien Assalam Aleikum.
Jana mmefanya press conference, mmezungumza na kutoa kauli yenu kuhusu hatua ya Sheikh Ponda kusimama na kuwataka Waislamu na wananchi wamchague mheshimiwa Lissu katika uchaguzi huu.
Mmepinga vikali kauli yake kuwa Waislamu wamekubaliana kumchagua Ndugu Lissu katika uchaguzi huu, naomba niwakumbushe yafuatayo.
1. Je, mnafahamu kuwa kuna waraka wa shura ya maimamu unaoelezea mtu gani anafaa kuchaguliwa?
Kabla hamjamuita Sheikh Ponda muongo kwamba eti waislamu hawana makubaliano juu ya mtu gani wa kumchagua, ningependa muurejee waraka wa majuzi wa shura ya maimamu, umetoa orodha ya Sifa nyingi sana za mtu anayefaa kuchaguliwa sifa mojawapo awe mtu anayependa HAKI.
Sasa nyie Masheikh wetu hebu tuambieni, kama kwenye waraka wa Shura maimamu wamekemea suala la kutokuwepo kwa haki nchini katika utawala huu wa rais Magufuli, hapo Shura ya Maimamu ina maana gani inaposema waislamu wachague mtu wa HAKI?, Kiufupi shura inaelezea kuhusu kubadili utawala kwenye uchaguzi huu na hicho ndicho Sheikh Ponda anachokifanya sasa hivi, Yaani kujaribu kusimamia azimio la Shura la kuondoa utawala wa dhulma na kuleta nchini utawala wa HAKI. Waislamu tunasimama na wapenda haki wote nchini bila kujali dini zao.
2. Wahadhiri na Masheikh wetu mmeonyesha double standard
Kwenye hiyo press conference mliyofanya hapo jana, mlikuwa chumba kimoja na Masheikh wanaoipigia kampeni CCM waziwazi, mlikuwa na Alhadi (huyu siyo sheikh anyway ni mjanjamjanja tu aliyesoma dini), Pia alikuwepo Sheikh Majini, wote hawa wameipigia kampeni CCM waziwazi, Tena huyo Alhadi amefanya kufuru kubwa kwa kuomba kwa jina la asiye ALLAH, na mnafahamu Qur'an imefundisha nini kuhusu wale wafanyao shirki kwana hukumu gani mbele ya ALLAH.
Kwenye hiyo press conference nilitegemea Ustaadh Mazinge umpe kwanza huyo Alhadi vifungu vya Bible na Qur'an kuonyesha kuwa amekosea kwa sababu wewe ni mtaalamu wa elimu ya Comparative religions (yaani malinganisho ya dini mbalimbali kwa kutumia vitabu vyao) na tunakupenda na kukuheshimu sana kwa kazi uliyoifanya kwa Takriban zaidi ya miaka 25 sasa. Tulitegemea umuambie Alhadi auombe radhi umma wa Waislamu kwa kuidunisha dini yetu, wakati inapaswa iwe juu na kusiwepo kuchanganya haki na batili hata kidog katika dini. Sasa utamnyoosheaje Kidole Ponda wakati pembeni yenu wamekaa wakosaji wa wazi?
3. Waislamu tunaumizwa sana na Masheikh wetu walioko jela kiuonevu
Leo hii sisi ni wakiwa, Masheikh wetu wako jela, wako jela Dar, Arusha, Mtwara, wako Jela kila mahali. Sisi waumini tunaumia, nyoyo zetu zimepigwa ganzi, tumejishika tama, tunahuzunika sana. Ni nani atakayetufundisha neno la ALLAH, ni nani atakayetupa faraja ya mtume wetu, ni nani atakayetufundisha mema tupate faida za duniani na mbinguni kama siyo Masheikh wetu walio jela?. Wamewekwa ndani na serikali ya CCM, wananyakuliwa mmoja mmoja kama mwewe anyakuavyo kifaranga na kuswekwa ndani. Sasa kweli nyie wahadhiri Mnamnyooshea kidole Ponda mtu anayetaka aingie madarakani mtu wa HAKI ili awatoe jela Masheikh wetu?.
Uislamu umefundisha, ukiona Jambo baya liondoe kwa mkono wako, ukishindwa kemea, na ukishindwa hata kukemea basi chukia, ila hiyo option ya mwisho ni udhaifu wa Imani. Hebu nyie wahadhiri wetu mnaomnyooshea kidole Sheikh Ponda leo, Mmekemea lini mbele ya hadhara ya Watanzania suala la Masheikh wetu kukaa ndani bila haki?
4. Sheikh Ponda yuko sahihi, hatua yake ni kwa maslahi ya umma wa kiislamu
Katika nchi hii vyama vya siasa, chaguzi na haki za kikatiba ni vitu halali na vya kisheria. Ni mfumo wa kubadili uongozi ili kila mtu au kundi fulani la jamii kuweka utawala ambao wanahisi watanufaika au kupata ahueni, fursa na manufaa fulanifulani. Napenda kuwafahamisha wahadhiri wetu kuwa kumekuwepo kilio katika jumuia za kiislamu kuhusu Udini wa wazi katika awamu hii, Shura ya maimamu ilitoa waraka wenye kuonyesha kisayansi kabisa teuzi zilizofanywa na awamu hii zinavyonuka udini. Teuzi zimelalia upande wa imani moja mpaka aibu almost kwa uwiano wa 80:20.
Haya kwanza kabisa aliyakemea Sheikh Khalifa na baadae Shura ya maimamu ikatoa waraka mzito, wa kishujaa na wa kukumbukwa juu ya jambo hili. Sasa kwa ubaguzi huu wa dhahiri kabisa usio na aibu nyie wahadhiri wetu mnaanza kumpiga mishale mtu ambaye anatumia taratibu halali zilizoko nchini ili kusimika utawala utakaotenda haki kwa wote?
Hatua anayoichukua leo Sheikh Ponda ni hatua kama ambazo Masheikh wetu walichukua kumsaidia Nyerere ili kumtoa mkoloni ili kusimika utawala mpya utakaoheshimu maslahi yao na haki yao. Sheikh Ponda hana tofauti na masheikh akina Tambaza, Ramia, Chaurembo na wengineo waliosimama bega kwa bega na Nyerere kung'oa utawala dhalimu na kuleta utawala wa haki.
5. Masheikh na wahadhiri wetu tunaomba mtuache, tarehe 28 tuna jambo letu
Dhulma huondolewa kwa mkono na kauli. Kauli yetu ni HAKI, UHURU na MAENDELEO YA WATU na mkono wetu ni Kura zetu. Tunawaomba wahadhiri wetu mtuache, hii ni nafasi adimu na adhimu ya kuondoa Dhulma na Uonevu katika nchi. Huyu Tundu Lissu anayetetea haki zetu Si Muislamu lakini ni Mtu wa Haki, huyu hana tofauti na Annaajashi (King Negus of the ancient Ethiopia), alikuwa ni Mfalme Mkiristo lakini mpenda Haki na muadilifu, huyu ndiye aliyeunusuru Uislamu na Waislamu kwa kuwapa hifadhi katika himaya yake wanafunzi wa mtume waliokimbia mateso na manyanyaso ya wapagani wa Makka. Tundu Lissu ni mkiristo mpenda haki, huyu ndiye anayetufaa na siyo yule ambaye hatupi nafasi za kutosha kwenye serikali yake halafu anatuhadaa kutujengea misikiti, lini sisi tumewahi kuwa na shida ya kujengewa msikiti na mtawala?. Sisi Shida yetu ni HAKI, UHURU na MAENDELEO YA WATU!
Mwisho kabisa nitoe nasaha kwa Watanzania wenzangu
Hatua ya Sheikh Ponda ni hatua ya kizalendo sana, Si hatua ya Udini hata kidogo, Maana kama Ponda angekuwa mdini maana yake angemuunga mkono Hashim Rungwe au Lipumba ambao ni waislamu wenzie. Ponda kamuunga mkono Lissu ambaye yeye Lissu na Magufuli ni wa Imani moja na dhehebu moja ila tofauti yao kuu ni kuwa Lissu ni mtu wa Haki wakati Mgombea wa CCM si mtu wa haki hata kidogo (Ana double standard na ndimi mbili). Tuungane kumuweka Lissu madarakani ili atuondolee dhulma ya kutisha katika nchi!