Uchaguzi 2020 Hili la Sheikh Ponda liacheni. Hatua ya Ponda ni kwa maslahi ya Waislam na Watanzania

Uchaguzi 2020 Hili la Sheikh Ponda liacheni. Hatua ya Ponda ni kwa maslahi ya Waislam na Watanzania

Kwenu Masheikh na wahadhiri wetu
Nawasalimien Assalam Aleikum.

Jana mmefanya press conference, mmezungumza na kutoa kauli yenu kuhusu hatua ya Sheikh Ponda kusimama na kuwataka Waislamu na wananchi wamchague mheshimiwa Lissu katika uchaguzi huu.

Mmepinga vikali kauli yake kuwa Waislamu wamekubaliana kumchagua Ndugu Lissu katika uchaguzi huu, naomba niwakumbushe yafuatayo.

1. Je, mnafahamu kuwa kuna waraka wa shura ya maimamu unaoelezea mtu gani anafaa kuchaguliwa?
Kabla hamjamuita Sheikh Ponda muongo kwamba eti waislamu hawana makubaliano juu ya mtu gani wa kumchagua, ningependa muurejee waraka wa majuzi wa shura ya maimamu, umetoa orodha ya Sifa nyingi sana za mtu anayefaa kuchaguliwa sifa mojawapo awe mtu anayependa HAKI.

Sasa nyie Masheikh wetu hebu tuambieni, kama kwenye waraka wa Shura maimamu wamekemea suala la kutokuwepo kwa haki nchini katika utawala huu wa rais Magufuli, hapo Shura ya Maimamu ina maana gani inaposema waislamu wachague mtu wa HAKI?, Kiufupi shura inaelezea kuhusu kubadili utawala kwenye uchaguzi huu na hicho ndicho Sheikh Ponda anachokifanya sasa hivi, Yaani kujaribu kusimamia azimio la Shura la kuondoa utawala wa dhulma na kuleta nchini utawala wa HAKI. Waislamu tunasimama na wapenda haki wote nchini bila kujali dini zao.

2. Wahadhiri na Masheikh wetu mmeonyesha double standard
Kwenye hiyo press conference mliyofanya hapo jana, mlikuwa chumba kimoja na Masheikh wanaoipigia kampeni CCM waziwazi, mlikuwa na Alhadi (huyu siyo sheikh anyway ni mjanjamjanja tu aliyesoma dini), Pia alikuwepo Sheikh Majini, wote hawa wameipigia kampeni CCM waziwazi, Tena huyo Alhadi amefanya kufuru kubwa kwa kuomba kwa jina la asiye ALLAH, na mnafahamu Qur'an imefundisha nini kuhusu wale wafanyao shirki kwana hukumu gani mbele ya ALLAH.

Kwenye hiyo press conference nilitegemea Ustaadh Mazinge umpe kwanza huyo Alhadi vifungu vya Bible na Qur'an kuonyesha kuwa amekosea kwa sababu wewe ni mtaalamu wa elimu ya Comparative religions (yaani malinganisho ya dini mbalimbali kwa kutumia vitabu vyao) na tunakupenda na kukuheshimu sana kwa kazi uliyoifanya kwa Takriban zaidi ya miaka 25 sasa. Tulitegemea umuambie Alhadi auombe radhi umma wa Waislamu kwa kuidunisha dini yetu, wakati inapaswa iwe juu na kusiwepo kuchanganya haki na batili hata kidog katika dini. Sasa utamnyoosheaje Kidole Ponda wakati pembeni yenu wamekaa wakosaji wa wazi?

3. Waislamu tunaumizwa sana na Masheikh wetu walioko jela kiuonevu
Leo hii sisi ni wakiwa, Masheikh wetu wako jela, wako jela Dar, Arusha, Mtwara, wako Jela kila mahali. Sisi waumini tunaumia, nyoyo zetu zimepigwa ganzi, tumejishika tama, tunahuzunika sana. Ni nani atakayetufundisha neno la ALLAH, ni nani atakayetupa faraja ya mtume wetu, ni nani atakayetufundisha mema tupate faida za duniani na mbinguni kama siyo Masheikh wetu walio jela?. Wamewekwa ndani na serikali ya CCM, wananyakuliwa mmoja mmoja kama mwewe anyakuavyo kifaranga na kuswekwa ndani. Sasa kweli nyie wahadhiri Mnamnyooshea kidole Ponda mtu anayetaka aingie madarakani mtu wa HAKI ili awatoe jela Masheikh wetu?.
Uislamu umefundisha, ukiona Jambo baya liondoe kwa mkono wako, ukishindwa kemea, na ukishindwa hata kukemea basi chukia, ila hiyo option ya mwisho ni udhaifu wa Imani. Hebu nyie wahadhiri wetu mnaomnyooshea kidole Sheikh Ponda leo, Mmekemea lini mbele ya hadhara ya Watanzania suala la Masheikh wetu kukaa ndani bila haki?

4. Sheikh Ponda yuko sahihi, hatua yake ni kwa maslahi ya umma wa kiislamu
Katika nchi hii vyama vya siasa, chaguzi na haki za kikatiba ni vitu halali na vya kisheria. Ni mfumo wa kubadili uongozi ili kila mtu au kundi fulani la jamii kuweka utawala ambao wanahisi watanufaika au kupata ahueni, fursa na manufaa fulanifulani. Napenda kuwafahamisha wahadhiri wetu kuwa kumekuwepo kilio katika jumuia za kiislamu kuhusu Udini wa wazi katika awamu hii, Shura ya maimamu ilitoa waraka wenye kuonyesha kisayansi kabisa teuzi zilizofanywa na awamu hii zinavyonuka udini. Teuzi zimelalia upande wa imani moja mpaka aibu almost kwa uwiano wa 80:20.

Haya kwanza kabisa aliyakemea Sheikh Khalifa na baadae Shura ya maimamu ikatoa waraka mzito, wa kishujaa na wa kukumbukwa juu ya jambo hili. Sasa kwa ubaguzi huu wa dhahiri kabisa usio na aibu nyie wahadhiri wetu mnaanza kumpiga mishale mtu ambaye anatumia taratibu halali zilizoko nchini ili kusimika utawala utakaotenda haki kwa wote?

Hatua anayoichukua leo Sheikh Ponda ni hatua kama ambazo Masheikh wetu walichukua kumsaidia Nyerere ili kumtoa mkoloni ili kusimika utawala mpya utakaoheshimu maslahi yao na haki yao. Sheikh Ponda hana tofauti na masheikh akina Tambaza, Ramia, Chaurembo na wengineo waliosimama bega kwa bega na Nyerere kung'oa utawala dhalimu na kuleta utawala wa haki.

5. Masheikh na wahadhiri wetu tunaomba mtuache, tarehe 28 tuna jambo letu
Dhulma huondolewa kwa mkono na kauli. Kauli yetu ni HAKI, UHURU na MAENDELEO YA WATU na mkono wetu ni Kura zetu. Tunawaomba wahadhiri wetu mtuache, hii ni nafasi adimu na adhimu ya kuondoa Dhulma na Uonevu katika nchi. Huyu Tundu Lissu anayetetea haki zetu Si Muislamu lakini ni Mtu wa Haki, huyu hana tofauti na Annaajashi (King Negus of the ancient Ethiopia), alikuwa ni Mfalme Mkiristo lakini mpenda Haki na muadilifu, huyu ndiye aliyeunusuru Uislamu na Waislamu kwa kuwapa hifadhi katika himaya yake wanafunzi wa mtume waliokimbia mateso na manyanyaso ya wapagani wa Makka. Tundu Lissu ni mkiristo mpenda haki, huyu ndiye anayetufaa na siyo yule ambaye hatupi nafasi za kutosha kwenye serikali yake halafu anatuhadaa kutujengea misikiti, lini sisi tumewahi kuwa na shida ya kujengewa msikiti na mtawala?. Sisi Shida yetu ni HAKI, UHURU na MAENDELEO YA WATU!

Mwisho kabisa nitoe nasaha kwa Watanzania wenzangu
Hatua ya Sheikh Ponda ni hatua ya kizalendo sana, Si hatua ya Udini hata kidogo, Maana kama Ponda angekuwa mdini maana yake angemuunga mkono Hashim Rungwe au Lipumba ambao ni waislamu wenzie. Ponda kamuunga mkono Lissu ambaye yeye Lissu na Magufuli ni wa Imani moja na dhehebu moja ila tofauti yao kuu ni kuwa Lissu ni mtu wa Haki wakati Mgombea wa CCM si mtu wa haki hata kidogo (Ana double standard na ndimi mbili). Tuungane kumuweka Lissu madarakani ili atuondolee dhulma ya kutisha katika nchi!
Sheikh Ponda siku zote ni mtu wa kuaminika na haoni woga wala aibu kusimamia kile anachokiamini. Hali hii imemfanya kuwa mmoja wa masheikh pendwa na wanaoaminiwa na umma wa waislamu. Sheikh Ponda kwa kuaminiwa kwake amepata uungwaji mkono na makundi mbalimbali ya kijamii waislamu na wasio waislamu, wasomi na watu wa kawaida.

Sioni uhalisia wa madai ya wahadhiri wetu juu ya Sheikh Ponda. Hata kama yana ukweli fulani, lakini naona Kama hayakuja wakati muafaka au wametumwa kukinusuru chama changu kisiangamie? Wasiwasi wangu ni mmoja tu, Sheikh Ponda si miongoni mwa watu wenye makandokando. Sheikh Ponda ana population kubwa nyuma yake ukilinganisha na hao wahadhiri au masheikh wa bakwata na taasisi zetu nyingine.

Anachokisema Sheikh Ponda ana uhakika kwa sababu anajua ana kubalika na umma. Wanaotaka kufanya makubaliano na Sheikh Ponda nani kuwatuma?
 
Comparative religions we fala unatulete midhara kwenye nchi ambayo haina udini.
Udini upo Tanzania. Angalia uteuzi wa JPM amejaza Wakristo tu. Ila usilete hoja ya Majaliwa na Samia kwa kuwa hakuwa na options
 
Udini upo Tanzania. Angalia uteuzi wa JPM amejaza Wakristo tu. Ila usilete hoja ya Majaliwa na Samia kwa kuwa hakuwa na options
Kabisa Mkuu,
Kwa jinsi teuzi za jamaa zilivyo basi Bakwata wangekua sio wanafiki wangejitenga nae kitambo tu.

Swala la pili la Bakwata kujitenga na Jamaa ni kuhusu kesi ya wale Masheikh wa Uamsho namna wanavyotendewa.
 
Kwani wale Masheikh walifanya nini ?
 
mimi sijui,ila tareh 28 waislamu watatumia akili zao binafsi,sio mahaba ya sheikh ponda.
Bado hujui km hujui.wewe ni msemaji wa waislamu.? Ponda waislamu wanamwelewa.Najua hujui ni kwann waislamu wanamwelewa Ponda.Hujui kinachoendelea Bakwata.
 
mimi sijui,ila tareh 28 waislamu watatumia akili zao binafsi,sio mahaba ya sheikh ponda.
Labda waislamu wanafiki lakini waislamu wa haki tunaosononeshwa na mateso ya mashekh wetu tupo na Sheikh Ponda
Kura zetu kwa Lissu
Waislamu wanafiki wapo na BAKWATA kura zao kwa yule katili anaetutesa
 
Labda waislamu wanafiki lakini waislamu wa haki tunaosononeshwa na mateso ya mashekh wetu tupo na Sheikh Ponda
Kura zetu kwa Lissu
Waislamu wanafiki wapo na BAKWATA kura zao kwa yule katili anaetutesa
Huko Jela kuna waislamu wangapi ambao wako huko bila hatia? ila wewe umeona hao masheikh tu na ndio unataka kumpigia mtu kura awe rais ili tu akawatoe masheikh jela?

Ndio maana waislamu huwa tunadharaulika tunaoneka hatuna akili na hatujakwenda shule.

Mwaka 2010 huyo Sheikh Ponda alimpigia kampeni Kikwete kwa waislamu sababu tu ni muislamu mwenzetu na sasa kageuka tena anampigia kampeni Asiye muislamu,ama kweli waislamu wa Tz ni wajinga Ponda anawageuza geuza tu anavyotaka.
 
Labda waislamu wanafiki lakini waislamu wa haki tunaosononeshwa na mateso ya mashekh wetu tupo na Sheikh Ponda
Kura zetu kwa Lissu
Waislamu wanafiki wapo na BAKWATA kura zao kwa yule katili anaetutesa

masheikh wale kama alivyo ponda,wanatumia uma wa waislam vibaya ku backup ajenda zao za siri.

walifanya harakati za siasa chafu,zikafanya wafungwe.sasa wanatafuta kuungwa mkono na waislamu kwa kusema walikuwa wanawasemea.
 
Huko Jela kuna waislamu wangapi ambao wako huko bila hatia? ila wewe umeona hao masheikh tu na ndio unataka kumpigia mtu kura awe rais ili tu akawatoe masheikh jela?

Ndio maana waislamu huwa tunadharaulika tunaoneka hatuna akili na hatujakwenda shule.
Maa shaa Allah
You sound like you went to school
Kwa hio kwa sababu kuna watu wengi jela bila hatia Ndio iwe halali kwa huyu katili kuendelea kutesa mashekh?
I wish I could know your education level

Mimi nimefuatilia kampeni za Magufuli. Samia. Majaliwa na Jakaya hakuna anazungumzia kwa kukana au kukiri jambo Hilo
Sasa ndugu ilituonekane tumesoma lazima tufurahie mateso ya mashekh jela?
 
Bado hujui km hujui.wewe ni msemaji wa waislamu.? Ponda waislamu wanamwelewa.Najua hujui ni kwann waislamu wanamwelewa Ponda.Hujui kinachoendelea Bakwata.

waislam hawana utawala wa kidini nchi hii,lakini kupitia ponda baadhi yao wanadhani wanaweza kupewa mamlaka kamili.

ndipo hapo bakwata inaposimama kama msaliti.

yote kwa yote waislam hawawezi kukubali kutumika kisiasa,hii ni dharau kubwa.
 
masheikh wale kama alivyo ponda,wanatumia uma wa waislam vibaya ku backup ajenda zao za siri.

walifanya harakati za siasa chafu,zikafanya wafungwe.sasa wanatafuta kuungwa mkono na waislamu kwa kusema walikuwa wanawasemea.
Mkuu huyu ponda hakuna ushahidi kwa unayosema
Na sisi waislamu wa kweli ukiwaacha wanafiki hatujasema waachiwe huru ila kilio chetu ni kwamba,,,,,
Wapelekwe mahakamani ili haki itendeke kama wanakosa wahukumiwe kama LAA waachiwe sio kila kukicha wanawatesa kwa kuwaminya korodani mpaka wanawahasi wengine wanakufa na kufukiwa kama mzoga
Kama kinacho fanyika ni Sawa mbona Magufuli. Samia. Majaliwa wala Jakaya hawatoi tamko kama Lako kukubali au kukataa
Kwa kweli ummah wa kiislamu tumeguswa Sana Ndio maana kura kwa Lissu
 
Maa shaa Allah
You sound like you went to school
Kwa hio kwa sababu kuna watu wengi jela bila hatia Ndio iwe halali kwa huyu katili kuendelea kutesa mashekh?
I wish I could know your education level

Mimi nimefuatilia kampeni za katili. Samia. Majaliwa na Jakaya hakuna anazungumzia kwa kukana au kukiri jambo Hilo
Sasa ndugu ilituonekane tumesoma lazima tufurahie mateso ya mashekh jela?
Ndio umeongea nini hapo? bado unawazungumzia masheikh tu yani kana kwamba hao masheikh ndio tatizo pekee la waislamu Tz.

Yani wewe hao masheikh tu ndio roho inakuuma kuwa huko jela wakati kuna waislamu wengine kibao tu huko ila huna habari nao.
 
Sasa swali Lina Kuja kwa sababu kuna watu wengi jela bila hatia Ndio sisi tufurahie mateso wanayo pata viongozi wetu wa dini?
Kama wewe unafurahia ili uone Kane umesoma haupo peke yako ndani ya waislamu wapo wanafiki wengi hata Enzi za MTUME SAW walikuwepo na watakuwepo
I wish unajua kusoma Quran soma surat almunafiquun
Ni sura Ina husu wanafiki
 
Back
Top Bottom