Uchaguzi 2020 Hili la Sheikh Ponda liacheni. Hatua ya Ponda ni kwa maslahi ya Waislam na Watanzania

Uchaguzi 2020 Hili la Sheikh Ponda liacheni. Hatua ya Ponda ni kwa maslahi ya Waislam na Watanzania

Kusema ukweli Sh Ponda kashatufungua macho waislamu wengi wanamuamini 90% kuliko Bakwata, akiendelea hizi siku zilio baki za kampeini, CCM ni kwaheri, kumbukeni CCM kwa mda mrefu imetumia ignorance ya waislamu kozoa kura zao, tena kumbukeni waislamu tuko 60% ya watanzania.......na tuna Imani na Ponda kuliko Bakwata
Miaka yote CCM imewatumia Waislam kama daraja lao kufikia matamanio yao ya kutawala milele, safari hii wamekwama lazima tuwafurushe wahuni hawa.
 
Ponda, nae ni mtanzania ana mapenzi binafsi ya itikadi ya kisiasa kama alivyo alhad na wengine wanaoshabikia ccm

Uzuri wa ponda hayumo kwenye payroll ya ccm, hao wengine wanafanya kazi ya shetani kwa kupokea malipo haramu ili watanzania wanyime haki na kukandamizwa

unafiki wenu ni kuona mtu ni msomi,mkweli,msimamia haki,au ana akili sana kwa sababu tu anaipinga serikali.

hapa ndipo mnapoonekana wazandiki tu.
yaani leo hii hata makonda akiamua aunge juhudi za lissu anatakata on the spot.
 
Kila mtu asimamie anachokiamini.

Mambo ya kusemeana sio jukumu la ponda wala kiongozi yeyote wa kiislamu.
Sisi Waislamu tunafurahi kusemewa na Sheikh Ponda, na kwa hakika tunakubaliana na kile tunachoambiwa na Sheikh Ponda!! Sasa wewe usie Muislamu unapata wapi mamlaka ya kujaribu kutupangia Waislamu kuhusu mwenye jukumu la kutusemea?!
 
Sisi Waislamu tunafurahi kusemewa na Sheikh Ponda, na kwa hakika tunakubaliana na kile tunachoambiwa na Sheikh Ponda!! Sasa wewe usie Muislamu unapata wapi mamlaka ya kujaribu kutupangia Waislamu kuhusu mwenye jukumu la kutusemea?!

kama sheikh ponda anaweza kuwasemea,basi yeyote anaweza kuwasemea pia.

hilo la kufurahi ama kutofurahi,inategemea anayekusemea mna mahusiano yepi.
 
unafiki wenu ni kuona mtu ni msomi,mkweli,msimamia haki,au ana akili sana kwa sababu tu anaipinga serikali.

hapa ndipo mnapoonekana wazandiki tu.
yaani leo hii hata makonda akiamua aunge juhudi za lissu anatakata on the spot.
Uwezo wako mdogo wa kufikiri, kaa kimya.
Lowasa je yupo wapi kwa sasa?
Alipokuwa upinzani mlisema anajinyea jukwaani kwenye kampeni, leo hii mmemchamba kwa maji ya kijani? Makonda kwetu ni zwazwa tu
 
Mtu anyependa haki anatukana wazee kuwa ni professorial rubush, anashiriki ndege na mali za nchi zikamatwe, anashiriki kwa wezi wa madini yetu, anashiriki nchi isipate misaada muhimu, anadharau kwa watu wengine na kujiona yeye ni msomi kuliko wengine, anataka kujitenga na zanziba, aliyemtukana babawa taiga na kumzodoa.

Anapendelea ndoa ya jinsia moja.

Je, huyo ndi mnamtaka?
NDIYOOOOOOOOOOOOO!!! Nimegonga meza X1000 kama wabunge wenu mjengoni
 
Waislam watamchagua Lissu na sisi wakristo inabidi tuwaambie makardinali wetu kuwa watangaze kuwa kura zetu ni kwa Magufuli.

Katika watu ma-bogus huyo Sheikh ni mmoja wa wanaoingia kumi bora.
 
kama sheikh ponda anaweza kuwasemea,basi yeyote anaweza kuwasemea pia.

hilo la kufurahi ama kutofurahi,inategemea anayekusemea mna mahusiano yepi.
Waislamu tunasemewa na Sheikh Ponda, na hao wengine acha wakusemehe wewe manake sie Sheikh Ponda anatosha!!
 
Aalim wa Ustadhi wangu juzi aliomba dua kwa kusema

"Ewe Mungu mlezi wa ulimwengu wote tunakushukuru kwa rehma zako ulizotupatia! Tunakuomba utusamehe madhambi yetu na madhambi ya ndugu zetu waliyotangulia na uwasamehe masheikh zetu waliyotangulia, na tunakuomba utunufaishe kwa urithi waliyorithi kutoka kwa Mtume. Utupe amani na salama katika nchi yetu! Amani na salama kipindi hiki cha uchaguzi ndani ya nchi yetu na utupatie kiongozi mwenye manufaa kwenye nchi....."
 
Uwezo wako mdogo wa kufikiri, kaa kimya.
Lowasa je yupo wapi kwa sasa?
Alipokuwa upinzani mlisema anajinyea jukwaani kwenye kampeni, leo hii mmemchamba kwa maji ya kijani? Makonda kwetu ni zwazwa tu

lowassa huyu huyu ambaye upinzani ulimnadi ni fisadi papa,halafu 2015 akawa wa mabadiriko.

au kuna mwingine,ulikiwa hujazaliwa mkuu??
 
Waislam watamchagua Lissu na sisi wakristo inabidi tuwaambie makardinali wetu kuwa watangaze kuwa kura zetu ni kwa Magufuli.

Katika watu ma-bogus huyo Sheikh ni mmoja wa wanaoingia kumi bora.
Hakuna mkristo wa kweli anayemjua Mungu - Jehova - Yahweh, Yesu Kristo na Roho Mtakatifu, na kuijua biblia vyema kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu anayeweza kumchagua JPM.
Hakuna
Hakunaaaaaa.
Hakunaaaaaaaaaaaa.
 
na ndiye atawapigia kura.
Kutusemea ndo kutupigia kwenyewe huko!!

Btw, mbona ni kama unaumia sana kuona Waislamu wanaona Sheikh Ponda ndie msemaje wao?!

Mbona ni kama unaumia sana kuona Waislamu wanakubaliana zaidi na Sheikh Ponda kuliko hao wengine?!
 
Kwenu Masheikh na wahadhiri wetu
Nawasalimien Assalam Aleikum.

Jana mmefanya press conference, mmezungumza na kutoa kauli yenu kuhusu hatua ya Sheikh Ponda kusimama na kuwataka Waislamu na wananchi wamchague mheshimiwa Lissu katika uchaguzi huu.

Mmepinga vikali kauli yake kuwa Waislamu wamekubaliana kumchagua Ndugu Lissu katika uchaguzi huu, naomba niwakumbushe yafuatayo.

1. Je mnafahamu kuwa kuna waraka wa shura ya maimamu unaoelezea mtu gani anafaa kuchaguliwa?
Kabla hamjamuita Sheikh Ponda muongo kwamba eti waislamu hawana makubaliano juu ya mtu gani wa kumchagua, ningependa muurejee waraka wa majuzi wa shura ya maimamu, umetoa orodha ya Sifa nyingi sana za mtu anayefaa kuchaguliwa sifa mojawapo awe mtu anayependa HAKI.

Sasa nyie Masheikh wetu hebu tuambieni, kama kwenye waraka wa Shura maimamu wamekemea suala la kutokuwepo kwa haki nchini katika utawala huu wa rais Magufuli, hapo Shura ya Maimamu ina maana gani inaposema waislamu wachague mtu wa HAKI?, Kiufupi shura inaelezea kuhusu kubadili utawala kwenye uchaguzi huu na hicho ndicho Sheikh Ponda anachokifanya sasa hivi, Yaani kujaribu kusimamia azimio la Shura la kuondoa utawala wa dhulma na kuleta nchini utawala wa HAKI. Waislamu tunasimama na wapenda haki wote nchini bila kujali dini zao.

2. Wahadhiri na Masheikh wetu mmeonyesha double standard
Kwenye hiyo press conference mliyofanya hapo jana, mlikuwa chumba kimoja na Masheikh wanaoipigia kampeni CCM waziwazi, mlikuwa na Alhadi (huyu siyo sheikh anyway ni mjanjamjanja tu aliyesoma dini), Pia alikuwepo Sheikh Majini, wote hawa wameipigia kampeni CCM waziwazi, Tena huyo Alhadi amefanya kufuru kubwa kwa kuomba kwa jina la asiye ALLAH, na mnafahamu Qur'an imefundisha nini kuhusu wale wafanyao shirki kwana hukumu gani mbele ya ALLAH.

Kwenye hiyo press conference nilitegemea Ustaadh Mazinge umpe kwanza huyo Alhadi vifungu vya Bible na Qur'an kuonyesha kuwa amekosea kwa sababu wewe ni mtaalamu wa elimu ya Comparative religions (yaani malinganisho ya dini mbalimbali kwa kutumia vitabu vyao) na tunakupenda na kukuheshimu sana kwa kazi uliyoifanya kwa Takriban zaidi ya miaka 25 sasa. Tulitegemea umuambie Alhadi auombe radhi umma wa Waislamu kwa kuidunisha dini yetu, wakati inapaswa iwe juu na kusiwepo kuchanganya haki na batili hata kidog katika dini. Sasa utamnyoosheaje Kidole Ponda wakati pembeni yenu wamekaa wakosaji wa wazi?

3. Waislamu tunaumizwa sana na Masheikh wetu walioko jela kiuonevu
Leo hii sisi ni wakiwa, Masheikh wetu wako jela, wako jela Dar, Arusha, Mtwara, wako Jela kila mahali. Sisi waumini tunaumia, nyoyo zetu zimepigwa ganzi, tumejishika tama, tunahuzunika sana. Ni nani atakayetufundisha neno la ALLAH, ni nani atakayetupa faraja ya mtume wetu, ni nani atakayetufundisha mema tupate faida za duniani na mbinguni kama siyo Masheikh wetu walio jela?. Wamewekwa ndani na serikali ya CCM, wananyakuliwa mmoja mmoja kama mwewe anyakuavyo kifaranga na kuswekwa ndani. Sasa kweli nyie wahadhiri Mnamnyooshea kidole Ponda mtu anayetaka aingie madarakani mtu wa HAKI ili awatoe jela Masheikh wetu?.
Uislamu umefundisha, ukiona Jambo baya liondoe kwa mkono wako, ukishindwa kemea, na ukishindwa hata kukemea basi chukia, ila hiyo option ya mwisho ni udhaifu wa Imani. Hebu nyie wahadhiri wetu mnaomnyooshea kidole Sheikh Ponda leo, Mmekemea lini mbele ya hadhara ya Watanzania suala la Masheikh wetu kukaa ndani bila haki?

4. Sheikh Ponda yuko sahihi, hatua yake ni kwa maslahi ya umma wa kiislamu
Katika nchi hii vyama vya siasa, chaguzi na haki za kikatiba ni vitu halali na vya kisheria. Ni mfumo wa kubadili uongozi ili kila mtu au kundi fulani la jamii kuweka utawala ambao wanahisi watanufaika au kupata ahueni, fursa na manufaa fulanifulani. Napenda kuwafahamisha wahadhiri wetu kuwa kumekuwepo kilio katika jumuia za kiislamu kuhusu Udini wa wazi katika awamu hii, Shura ya maimamu ilitoa waraka wenye kuonyesha kisayansi kabisa teuzi zilizofanywa na awamu hii zinavyonuka udini. Teuzi zimelalia upande wa imani moja mpaka aibu almost kwa uwiano wa 80:20.

Haya kwanza kabisa aliyakemea Sheikh Khalifa na baadae Shura ya maimamu ikatoa waraka mzito, wa kishujaa na wa kukumbukwa juu ya jambo hili. Sasa kwa ubaguzi huu wa dhahiri kabisa usio na aibu nyie wahadhiri wetu mnaanza kumpiga mishale mtu ambaye anatumia taratibu halali zilizoko nchini ili kusimika utawala utakaotenda haki kwa wote?

Hatua anayoichukua leo Sheikh Ponda ni hatua kama ambazo Masheikh wetu walichukua kumsaidia Nyerere ili kumtoa mkoloni ili kusimika utawala mpya utakaoheshimu maslahi yao na haki yao. Sheikh Ponda hana tofauti na masheikh akina Tambaza, Ramia, Chaurembo na wengineo waliosimama bega kwa bega na Nyerere kung'oa utawala dhalimu na kuleta utawala wa haki.

5. Masheikh na wahadhiri wetu tunaomba mtuache, tarehe 28 tuna jambo letu
Dhulma huondolewa kwa mkono na kauli. Kauli yetu ni HAKI, UHURU na MAENDELEO YA WATU na mkono wetu ni Kura zetu. Tunawaomba wahadhiri wetu mtuache, hii ni nafasi adimu na adhimu ya kuondoa Dhulma na Uonevu katika nchi. Huyu Tundu Lissu anayetetea haki zetu Si Muislamu lakini ni Mtu wa Haki, huyu hana tofauti na Annaajashi (King Negus of the ancient Ethiopia), alikuwa ni Mfalme Mkiristo lakini mpenda Haki na muadilifu, huyu ndiye aliyeunusuru Uislamu na Waislamu kwa kuwapa hifadhi katika himaya yake wanafunzi wa mtume waliokimbia mateso na manyanyaso ya wapagani wa Makka. Tundu Lissu ni mkiristo mpenda haki, huyu ndiye anayetufaa na siyo yule ambaye hatupi nafasi za kutosha kwenye serikali yake halafu anatuhadaa kutujengea misikiti, lini sisi tumewahi kuwa na shida ya kujengewa msikiti na mtawala?. Sisi Shida yetu ni HAKI, UHURU na MAENDELEO YA WATU!

Mwisho kabisa nitoe nasaha kwa Watanzania wenzangu
Hatua ya Sheikh Ponda ni hatua ya kizalendo sana, Si hatua ya Udini hata kidogo, Maana kama Ponda angekuwa mdini maana yake angemuunga mkono Hashim Rungwe au Lipumba ambao ni waislamu wenzie. Ponda kamuunga mkono Lissu ambaye yeye Lissu na Magufuli ni wa Imani moja na dhehebu moja ila tofauti yao kuu ni kuwa Lissu ni mtu wa Haki wakati Mgombea wa CCM si mtu wa haki hata kidogo (Ana double standard na ndimi mbili). Tuungane kumuweka Lissu madarakani ili atuondolee dhulma ya kutisha katika nchi!
Kwa hiyo siku hizi wa Tz tunapiga kura kwa makundi, ya kiislamu, kikristo, kihindi, halfu linakuja la kikabilia n.k .
 
Ni kumsikiliza ponda hao wakae na matamko yao ile kauli haifutiki hata wakae vikao vyote ingawaje huko mbele Ponda atakamatwa kwa kusingiziwa kutoa kauli za uchochezi yote hayo tunayafahamu...
Ila tuseme ukweli! Ile kauli ya Ponda eti Raia wailazimishe tume ya Uchaguzi kumtangaza Lissu kua Raisi ni ya vitisho na Uchochezi!!
 
Kutusemea ndo kutupigia kwenyewe huko!!

Btw, mbona ni kama unaumia sana kuona Waislamu wanaona Sheikh Ponda ndie msemaje wao?!

Mbona ni kama unaumia sana kuona Waislamu wanakubaliana zaidi na Sheikh Ponda kuliko hao wengine?!

mimi siumii na sheikh ponda kuwasemea waislamu.

naumia na waislamu kutanabaishwa kienyeji tu kwamba wao ni chadema.uislamu hauna mafungamano na chama chochote cha siasa,ila muislam ni mfuasi wa chama.

ni busara msomi huyu na mwanazuoni kukumbuka hilo.
 
Kutusemea ndo kutupigia kwenyewe huko!!

Btw, mbona ni kama unaumia sana kuona Waislamu wanaona Sheikh Ponda ndie msemaje wao?!

Mbona ni kama unaumia sana kuona Waislamu wanakubaliana zaidi na Sheikh Ponda kuliko hao wengine?!
Bakwata iko mfukoni mwa CCM,so Ponda ni sauti ya nyikani na Waislam wanaitii sauti hiyo.
 
mimi siumii na sheikh ponda kuwasemea waislamu.

naumia na waislamu kutanabaishwa kienyeji tu kwamba wao ni chadema.uislamu hauna mafungamano na chama chochote cha siasa,ila muislam ni mfuasi wa chama.
Utajua hujui
 
Back
Top Bottom