Uchaguzi 2020 Hili la Sheikh Ponda liacheni. Hatua ya Ponda ni kwa maslahi ya Waislam na Watanzania

Uchaguzi 2020 Hili la Sheikh Ponda liacheni. Hatua ya Ponda ni kwa maslahi ya Waislam na Watanzania

..uchaguzi ni kati ya Lissu na Magufuli.

..kati ya hao wawili Sheikh Ponda ameona Lissu ndio muadilifu.

..Sheikh Ponda ameona linapokuja suala la HAKI, Lissu atasimamia haki za kila Mtanzania.

..Magufuli ameshajionyesha ktk miaka yake mitano kwamba ni mtu asiyeheshimu haki, na asiyetaka kufuata sheria.
Asiyetaka kufuata sheria mbona mkibolewa Nyumba kwa mujibu wa sheria mnalalamika.
Watu walimdhiaki Yesu na miujiza yote ile itakuja kuwa mwanadamu JPM .
Hamtutishi ubabe ni 28OCT tunaenda na JPM .
 
Kwenu Masheikh na wahadhiri wetu
Nawasalimien Assalam Aleikum.

Jana mmefanya press conference, mmezungumza na kutoa kauli yenu kuhusu hatua ya Sheikh Ponda kusimama na kuwataka Waislamu na wananchi wamchague mheshimiwa Lissu katika uchaguzi huu.

Mmepinga vikali kauli yake kuwa Waislamu wamekubaliana kumchagua Ndugu Lissu katika uchaguzi huu, naomba niwakumbushe yafuatayo.

1. Je, mnafahamu kuwa kuna waraka wa shura ya maimamu unaoelezea mtu gani anafaa kuchaguliwa?
Kabla hamjamuita Sheikh Ponda muongo kwamba eti waislamu hawana makubaliano juu ya mtu gani wa kumchagua, ningependa muurejee waraka wa majuzi wa shura ya maimamu, umetoa orodha ya Sifa nyingi sana za mtu anayefaa kuchaguliwa sifa mojawapo awe mtu anayependa HAKI.

Sasa nyie Masheikh wetu hebu tuambieni, kama kwenye waraka wa Shura maimamu wamekemea suala la kutokuwepo kwa haki nchini katika utawala huu wa rais Magufuli, hapo Shura ya Maimamu ina maana gani inaposema waislamu wachague mtu wa HAKI?, Kiufupi shura inaelezea kuhusu kubadili utawala kwenye uchaguzi huu na hicho ndicho Sheikh Ponda anachokifanya sasa hivi, Yaani kujaribu kusimamia azimio la Shura la kuondoa utawala wa dhulma na kuleta nchini utawala wa HAKI. Waislamu tunasimama na wapenda haki wote nchini bila kujali dini zao.

2. Wahadhiri na Masheikh wetu mmeonyesha double standard
Kwenye hiyo press conference mliyofanya hapo jana, mlikuwa chumba kimoja na Masheikh wanaoipigia kampeni CCM waziwazi, mlikuwa na Alhadi (huyu siyo sheikh anyway ni mjanjamjanja tu aliyesoma dini), Pia alikuwepo Sheikh Majini, wote hawa wameipigia kampeni CCM waziwazi, Tena huyo Alhadi amefanya kufuru kubwa kwa kuomba kwa jina la asiye ALLAH, na mnafahamu Qur'an imefundisha nini kuhusu wale wafanyao shirki wana hukumu gani mbele ya ALLAH.

Kwenye hiyo press conference nilitegemea Ustaadh Mazinge umpe kwanza huyo Alhadi vifungu vya Bible na Qur'an kuonyesha kuwa amekosea kwa sababu wewe ni mtaalamu wa elimu ya Comparative religions (yaani malinganisho ya dini mbalimbali kwa kutumia vitabu vyao) na tunakupenda na kukuheshimu sana kwa kazi uliyoifanya kwa Takriban zaidi ya miaka 25 sasa. Tulitegemea umuambie Alhadi auombe radhi umma wa Waislamu kwa kuidunisha dini yetu, wakati inapaswa iwe juu na kusiwepo kuchanganya haki na batili hata kidog katika dini. Sasa utamnyoosheaje Kidole Ponda wakati pembeni yenu wamekaa wakosaji wa wazi?

3. Waislamu tunaumizwa sana na Masheikh wetu walioko jela kiuonevu
Leo hii sisi ni wakiwa, Masheikh wetu wako jela, wako jela Dar, Arusha, Mtwara, wako Jela kila mahali. Sisi waumini tunaumia, nyoyo zetu zimepigwa ganzi, tumejishika tama, tunahuzunika sana. Ni nani atakayetufundisha neno la ALLAH, ni nani atakayetupa faraja ya mtume wetu, ni nani atakayetufundisha mema tupate faida za duniani na mbinguni kama siyo Masheikh wetu walio jela?. Wamewekwa ndani na serikali ya CCM, wananyakuliwa mmoja mmoja kama mwewe anyakuavyo kifaranga na kuswekwa ndani. Sasa kweli nyie wahadhiri Mnamnyooshea kidole Ponda mtu anayetaka aingie madarakani mtu wa HAKI ili awatoe jela Masheikh wetu?.
Uislamu umefundisha, ukiona Jambo baya liondoe kwa mkono wako, ukishindwa kemea, na ukishindwa hata kukemea basi chukia, ila hiyo option ya mwisho ni udhaifu wa Imani. Hebu nyie wahadhiri wetu mnaomnyooshea kidole Sheikh Ponda leo, Mmekemea lini mbele ya hadhara ya Watanzania suala la Masheikh wetu kukaa ndani bila haki?

4. Sheikh Ponda yuko sahihi, hatua yake ni kwa maslahi ya umma wa kiislamu
Katika nchi hii vyama vya siasa, chaguzi na haki za kikatiba ni vitu halali na vya kisheria. Ni mfumo wa kubadili uongozi ili kila mtu au kundi fulani la jamii kuweka utawala ambao wanahisi watanufaika au kupata ahueni, fursa na manufaa fulanifulani. Napenda kuwafahamisha wahadhiri wetu kuwa kumekuwepo kilio katika jumuia za kiislamu kuhusu Udini wa wazi katika awamu hii, Shura ya maimamu ilitoa waraka wenye kuonyesha kisayansi kabisa teuzi zilizofanywa na awamu hii zinavyonuka udini. Teuzi zimelalia upande wa imani moja mpaka aibu almost kwa uwiano wa 80:20.

Haya kwanza kabisa aliyakemea Sheikh Khalifa na baadae Shura ya maimamu ikatoa waraka mzito, wa kishujaa na wa kukumbukwa juu ya jambo hili. Sasa kwa ubaguzi huu wa dhahiri kabisa usio na aibu nyie wahadhiri wetu mnaanza kumpiga mishale mtu ambaye anatumia taratibu halali zilizoko nchini ili kusimika utawala utakaotenda haki kwa wote?

Hatua anayoichukua leo Sheikh Ponda ni hatua kama ambazo Masheikh wetu walichukua kumsaidia Nyerere ili kumtoa mkoloni ili kusimika utawala mpya utakaoheshimu maslahi yao na haki yao. Sheikh Ponda hana tofauti na masheikh akina Tambaza, Ramia, Chaurembo na wengineo waliosimama bega kwa bega na Nyerere kung'oa utawala dhalimu na kuleta utawala wa haki.

5. Masheikh na wahadhiri wetu tunaomba mtuache, tarehe 28 tuna jambo letu
Dhulma huondolewa kwa mkono na kauli. Kauli yetu ni HAKI, UHURU na MAENDELEO YA WATU na mkono wetu ni Kura zetu. Tunawaomba wahadhiri wetu mtuache, hii ni nafasi adimu na adhimu ya kuondoa Dhulma na Uonevu katika nchi. Huyu Tundu Lissu anayetetea haki zetu Si Muislamu lakini ni Mtu wa Haki, huyu hana tofauti na Annajaashi (King Negus of the ancient Ethiopia), alikuwa ni Mfalme Mkiristo lakini mpenda Haki na muadilifu, huyu ndiye aliyeunusuru Uislamu na Waislamu kwa kuwapa hifadhi katika himaya yake wanafunzi wa mtume waliokimbia mateso na manyanyaso ya wapagani wa Makka. Tundu Lissu ni mkiristo mpenda haki, huyu ndiye anayetufaa na siyo yule ambaye hatupi nafasi za kutosha kwenye serikali yake halafu anatuhadaa kutujengea misikiti, lini sisi tumewahi kuwa na shida ya kujengewa msikiti na mtawala?. Sisi Shida yetu ni HAKI, UHURU na MAENDELEO YA WATU!

Mwisho kabisa nitoe nasaha kwa Watanzania wenzangu
Hatua ya Sheikh Ponda ni hatua ya kizalendo sana, Si hatua ya Udini hata kidogo, Maana kama Ponda angekuwa mdini maana yake angemuunga mkono Hashim Rungwe au Lipumba ambao ni waislamu wenzie. Ponda kamuunga mkono Lissu ambaye yeye Lissu na Magufuli ni wa Imani moja na dhehebu moja ila tofauti yao kuu ni kuwa Lissu ni mtu wa Haki wakati Mgombea wa CCM si mtu wa haki hata kidogo (Ana double standard na ndimi mbili). Tuungane kumuweka Lissu madarakani ili atuondolee dhulma ya kutisha katika nchi!
Hebu tuacheni kuichezea dini, siasa hii ya kibinafsi na dini hazina uhusiano. Tusifikie kukufuru, siasa kwenye Uislamu ruksa ila si ya aina hii iliyopo hapa
 
Muitikio wa Waisilamu kumpa kura zote walizokuwa nazo kwa Mhe Tundu Antipas Lissu umekuwa mkubwa sana tokea Sheikh mpenda HAKI na Maendeleo ya WATU Sheikh Ponda Issa Ponda alipopanda jukwaani na Tundu Lissu
 
Asiyetaka kufuata sheria mbona mkibolewa Nyumba kwa mujibu wa sheria mnalalamika.
Watu walimdhiaki Yesu na miujiza yote ile itakuja kuwa mwanadamu JPM .
Hamtutishi ubabe ni 28OCT tunaenda na JPM .

Aliyewakwapua watu mashamba yao kule Tanga na kuzila pesa za wale waliopata msiba wa tetemeko kule Kagera ??
 
Hebu tuacheni kuichezea dini, siasa hii ya kibinafsi na dini hazina uhusiano. Tusifikie kukufuru, siasa kwenye Uislamu ruksa ila si ya aina hii iliyopo hapa


Siasa ipi unayotaka kutuambia , au ya kuwaweka hawa aliotudhulumu muda mrefu ??? Ndugu zetu wako majela kwa makosa ya kubambikiziwa na Majambazi hawa , unataka tujikalie kimya ??
 
Mkuu Sasa waislamu nao wana haki ya kuchagua mgombea wanaomtaka na chama wanachokitaka,2010 aliwaambia waislamu wampigie kura Kikwete ila hakuna walichopata waislamu na sasa huyo huyo Ponda anatuambia tumpigie Lissu. Huyu Ponda anawatumia tu waislamu kwa manufaa anayoyajua mwenyewe.

Sasa ulitaka awaambie watu wampigie kura ndugu wa kikwete katika kuuwa aitwaye Magufuli . Mtu ambaye anawaongoza watu wasiojulikana waliompiga risasi Lisu??
 
kwani anapelekeka mahakamani ?
Hivi wewe Magufuli anashika bunduki kwa nini msimtuhumu waziri wa ulinzi mwenye bajeti ya vifaru unatupa lawama kwa JPM wakati yeye yupo too busy kujenga nchi pigeni kelele sana Ikulu hamuingii .
Tumechelewa mnooo...Tanzania sasa Middle income msiturudishe nyuma.
 
Muitikio wa Waisilamu kumpa kura zote walizokuwa nazo kwa Mhe Tundu Antipas Lissu umekuwa mkubwa sana tokea Sheikh mpenda HAKI na Maendeleo ya WATU Sheikh Ponda Issa Ponda alipopanda jukwaani na Tundu Lissu
Labda Sheikh Ponda na Wahamadiya wachache lakini wale ninaowajua mimi ambao Wanaswara pia ni marafiki zao hawawezi kumuingia mfiraji Ikulu .
 
Asiyetaka kufuata sheria mbona mkibolewa Nyumba kwa mujibu wa sheria mnalalamika.
Watu walimdhiaki Yesu na miujiza yote ile itakuja kuwa mwanadamu JPM .
Hamtutishi ubabe ni 28OCT tunaenda na JPM .
..Na kule Mwanza hawakubomolewa kwasababu wamempiga kura Jiwe?

..Waliobomolewa Kimara ilikuwa ni kinyume na sheria kwasababu kulikuwa zuio la MAHAKAMA.

..Hakuna anayemdhihaki Jpm, ila tunasema ukweli kwamba ni mbaguzi, fisadi, na asiyejali utu na haki za waTz.

NB:

..Jpm anasema waziwazi bila kificho kwamba hapeleki maendeleo mahali ambapo hawajachagua CCM.

..Je, huyo siyo mbaguzi? Je, huyo anafuata sheria? Je, anajali haki? Kwanini viongozi wa DINI hawamkemei?
 
Shehe Ponda ndie muislam anae umizwa Zaidi na suala la mashehe kuwekwa magerezani kuliko shehe wowote nchi..Yaani Ponda wale mashehe ni kama wadogo zake au kaka zake wa tumbo moja..Kwa Misimamo ya shehe Ponda isinge wezekana yeye kujishusha na kujidhalilisha chini ya Lissu..Ila Shehe ni kama mashehe wa gerezani wanalilia sikioni mwake..
 
Haiwezekani mzee tulia tuu
Tatizo mshaingiza mambo ya udini mshaharibu tayari
Muislamu yeyote anayekerwa na Udini wa Maguful hana budi kumpigia kura mtu wa haki Tundu Lissu

Angalia teuzi mbalimbali za Magufuli, Waislamu wako kiduchu kwelikweli.

Mimi nakumbuka profesa Kitila Mkumbo wakati huo hajaunga mkono juhudi aliandika makala kwenye gazeti kumtaka Magufuli aunde serikali yenye kubalance makundi mbalimbali ya kijamii. Ila kwa Ubishi Magufuli akateua maras, madas, Wenyeviti wa Bodi, wakurugenzi wa mashirika ya umma, Makatibu wakuu, manaibu mbalimbali, Wakuu wa wilaya Mikoa, Mawaziri, Manaibu na nafasi kedekede na katika teuzi hizo idadi ya Waislamu ni Kidogo mpaka aibu

Sasa huu ni muda muafaka waislamu kuondoa ubaguzi huu na kuweka mtu atakayetenda haki kwa wote
 
Kama huelewi uliza tukueleweshe. Other wise wewe ni mnufaika wa mfumo wa dhuluma
Ni mtazamo wako binafsi pia, ila mimi sioni mfumo wa kizulumaji bali unaweza kuta mtawala ana madhaifu kadhaa ya kibinadamu kitu ambacho kipo kwa watawala wa mataifa yote ulimwenguni, nipe mfano ni mtawala gani wa sasa kwenye taifa lolote duniani ambae anatawala kwa kufata haki zote na raia wamemkubali, mtawala wa aina hiyo sidhani kama utampata duniani
 
Tumechoka kuona damu za watu
Hatupendi mauaji yanayofanywa na watu wasiojulikana
Hatupendi kuona watu wanafilisiwa
Hatupendi kuona masheikh wanateswa na kufia jela
Haya mambo watanzania hatujawahi kuona tangu uhuru
Stagnant mind kabisa we, mmechoka kuona damu za watu, hizo damu unaziona ww tu mbona watanzania wote million 60 hawazioni ni ww tu ndiyo unaziona, ukitaka kuona damu za watu nenda Syria huko, Iraq, Yemen, Libya na kwingineko ila usiwadanganye watu hapa Jf kuwa umechoka kuona damu za watu hapa Tanzania.
 
..Na kule Mwanza hawakubomolewa kwasababu wamempiga kura Jiwe?

..Waliobomolewa Kimara ilikuwa ni kinyume na sheria kwasababu kulikuwa zuio la MAHAKAMA.

..Hakuna anayemdhihaki Jpm, ila tunasema ukweli kwamba ni mbaguzi, fisadi, na asiyejali utu na haki za waTz.

NB:

..Jpm anasema waziwazi bila kificho kwamba hapeleki maendeleo mahali ambapo hawajachagua CCM.

..Je, huyo siyo mbaguzi? Je, huyo anafuata sheria? Je, anajali haki? Kwanini viongozi wa DINI hawamkemei?
Ufisadi upi kwa mgombea yupi ulimsikia kasema kama kipindi kile kuwa CCM majizi.
Kelele zenu sasa hivi ni Haki .
Hilo halipingiki hata kama ni wewe mwanamke anaekupa Papuchi kiroho safi huwa unamfikiria hata kipindi unapopata pesa ila yule mwanamke mwingine anakuita ule papuchi kipindi una hela tu ,sasa hapo kwa ubinadamu kabisa wewe utakuwa radhi na yupi.
Mijitu inajua ipo kwenye Road Reserve na kuna Bicon na sheria inaeleza wazi ni mita ngapi kutoka upande wa barabara lakini wanaona kama walionewa wamesahau sheria iliyopo.
Ukimfurahisha kila mtu utaharibu nchi lazima wengine waji sacrify kwa ajili yetu kama JPM na ndugu yangu bahati ya mwenzio usiilale mlango wazi wana Mwanza acha wamlipe kwa mema yake na utambue Mbezi haiwezi kutuamulia 28oct 2020.
 
Ahaaaa, Cv ya Kilangi unaifahu? Unaongea kwa chuki tu.
CV yake siyo siri ana PhD na alikuwa Mwalimu SAUT. Anachopungukiwa ni kuto practice uwakili kwa miaka inayotakiwa kwenye Katiba. Ila kwa kuwa ni ndugu yetu amechukuliwa aje asimamie masilahi
 
Ni mtazamo wako binafsi pia, ila mimi sioni mfumo wa kizulumaji bali unaweza kuta mtawala ana madhaifu kadhaa ya kibinadamu kitu ambacho kipo kwa watawala wa mataifa yote ulimwenguni, nipe mfano ni mtawala gani wa sasa kwenye taifa lolote duniani ambae anatawala kwa kufata haki zote na raia wamemkubali, mtawala wa aina hiyo sidhani kama utampata duniani
Angela Merkel, Cyril Ramaphosa , Nana Akuffo Adoo, Abiy Mohamed, Emmanuel Macron, TRUDEAU
 
Back
Top Bottom