Angela Merkel, Cyril Ramaphosa , Nana Akuffo Adoo, Abiy Mohamed, Emmanuel Macron, TRUDEAU
Wewe ni hewa kweli kweli, Ramaphosa watu wanakatwa vichwa south africa kila kukicha alafu unasema utawala hauna doa, Wasauzi wabaguzi vile wanaua weusi wenzao ambao si wasauzi alafu unasema eti utawala safi ule.
Abiy wa ethiopia ni msafi yule, kama ni msafi unadhani kwanini wamoroni wanaandamana kila kukicha wakitaka haki sawa.
Na umesahau juzi tu hapa miezi miwili iliyopita yule msanii wa Ethiopia aliyekuwa anaimbaga nyimbo za kiu wanaharakati alikutwa umeuwawa kikatili mno hadi watu waethiopia waliandama nchi nzima kutaka haki itendeke.
una fikiri kama abiy anaiongoza vizuri nchi bila madhaifu ni kwanini mara kwa mara waethiopia wanakamatwa kwenye malori na mafuso huku kwetu Tanzania wakiwa wahamiaji haramu wanaikimbia Ethiopia.
Believe me, hakuna mtawala ambaye yuko perfect hapa chini ya jua, narudia tena hayupo.
Wapo watawala ambao wameongoza nchi zao zikafanikiwa sana lakini si kwamba wao ni watenda haki sana.
Kuna watawala kama Jin Ping wa china, amaongoza nchi imefanikiwa sana na wanamkubali sana lakin bado unaona china ndiyo nchi inayoongoza kunyonga watu duniani hadi sasa kuliko taifa jingine lolote.
Kuna Mtu kama putin wa Urusi ameipa heshima Urusi kwenye dunia lakini mzingue uone kama hajakukata kichwa.
Tunae Jirani yetu hapa Kagame wa rwanda ameifanya rwanda imeonekana kwenye dunia lakini nafikiri unaona wapinzani wanavokalia kuti kavu.
Kulikuwa na Gadaffi ambae alikuwa anawapa Walibya kila kitu lakini angalia waliokuwa wanampinga walichokuwa wanakutana nacho.
My take : Mtu kama lissu hapaswi kuranda randa hapa Tanzania zaidi anafarakanisha watanzania tu.