Hili la vibali vya kazi Rais ashauriwe zaidi

Kwamba SA ni wavivu hizo ni propoganda za mabeberu tu na wengi wanaamini , kuhalalisha ubaguzi wao kwa wazawa kwenye ajira.
Huku kwetu Wageni wanalipana mishahara mikubwa huku kazi zenyewe wazawa ndio wanafanya huku wakitumia bank account za nje kukwepa makato kama PAYE na NSSF.
 
Ni sawa mkuu, lakini wazawa hao hao walibagua Waafrika wenzao na kuwauwa! Ubaguzi siyo Mabeberu tu mkuu! (Kama unaamini Mtu mweupe ni beberu!) Kuna watu wenye hizi rangi zetu wenye ubaguzi wa kutusha!
Najua nationalism ni hali, lakini lazima iendane na rationalism pia! Kwa mfano kwenye eneo la elimu, ukitaka ku produce quality kwenye soko lazima utafute quality staff! Hata ukimchukua mkenya wa std 8, ukimpa interview na mwanachuo wetu hapa, utampa Mkenya kazi kirahisi tu!
 
Mkuu kwa mfano anakuja Mkenya au Mganda, wakashindana na wewe kwenye shule yangu, interview ya English teacher, unafikiri kwa hii Kiswanglish hapa, ntawaacha wale nikuchukue wewe, bwana August?
 
Mkuu kwa mfano anakuja Mkenya au Mganda, wakashindana na wewe kwenye shule yangu, interview ya English teacher, unafikiri kwa hii Kiswanglish hapa, ntawaacha wale nikuchukue wewe, bwana August?
Hivi wewe unafikiri wakenya wana kiingereza kizuri?
Inaonyesha huna interaction zuri na foreigners, au hao wakenya.
Lakini kwa average Tanzanias sawa wapo juu, lakini hawana kiingereza kizuri unavyo vikiria wewe , maybe vs U watakuwa wazuri kuliko wewe .
 
Mkuu Wewe ni mjuvi mkubwa wa mambo, labda tu, edit kidogo hapo juu, badala ya vikiria ukaandika fikiria. English yako Siyo mbaya, lakini you think in Swahili as you write in English Kwa hiyo hapo tunasema unaongea Kiswahili kwa maneno ya Kiingereza! Siyo tatizo lako, ni tatizo la Kitanzania, Sisi ni Waswahili, Sema tatizo ni pale unapo shindwa hata Kiswahili, hiyo VIKIRIA!!
 
Mwenzage aliye pita alibana wagen vizur Sana, Sasa yeye ana fungua milango ovyo Sasa wagen watajaa tutaanza kunyanyaswa tutakuwa wagen kwenye nchi yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Jaap, kuna unyanyasaji wowote wanao fanya wageni kwa wazawa kweli Au ni dhana potofu tu?! Hebu elezea manyanyaso specifically ambayo umepata kutoka kwa wageni. Kwenye comment nyingine umesema tunataka wageni wanao weza kuajiri, kwa hiyo hizo kazi ndogo ndogo, kama shambaboi ndo za Watz? Wageni wafanye za maana? Kwanini wageni wasifanye hizo kazi za hovyo na wazawa wafanye za maana?! Siyo dhana potofu hiyo?!
 

Sii kweli eti ukimpa interview std 8 wa Kenya na mwanachuo wetu basi utampa Mkenya kazi kirahisi tu????. Unawapa daraja la juu wasilostahili, Chuo cha Mweka walikuwepo wanafunzi kutoka Kenya na hawajashika number moja hata siku moja. Nenda Arusha jionee kwenye Utalii Tanzanian Guides walivyo vizuri kwenye fani zao. Hatuhitaji Serikali kutupatia pesa ila itupe mazingira mazuri ya kuzitafuta ikiwemo mikakati ya kulinda ajira za ndani tuweze wazawa kufaidika nazo.
 
Sawa mkuu, lakini ukitaka ushindani, usiwalindie wazawa kazi, wazipambanie kwa bidii zao, kwa sababu kama mzawa ana uwezo Nani ataajiri Mgeni kwa gharama? Huwezi kumwambia kocha amwache Chama eti apange kiungo mzawa ni Uzalendo! Mzawa asibebwe na uzawa abebwe na quality yake ya kazi!
 
Ndg nafikiri upo kwenye industry ambayo wageni ni wachache na huoni wamejazana,, mfano kuna makampuni ya kihindi ambayo wapo expatriate na wanna kazi nzuri tu lakini hakuna kitu kichwa mpaka vyeti?? Wanalundukana kwa kazi ambazo kwetu wapo wengi tu wenye sifa stahili kufanya, na ukiangalia you don't see fairness kwa salary Kati ya wageni na wenyeji

Kama una muda jipe utafiti mdogo tu utaona, we are speaking from the experience... Vibali vya kazi vibanwe tu tena zaidi maana lipo kundi kubwa la vijana liko tu mtaani halafu turuhusu tena free entry
 
Nafikiria kwa sehemu Upo sahihi, lakini mkuu tatizo ni ile kubeba wazawa, watu ambao wanaiba, wavivu na quality ndogo! Siyo Tanzania yote, lakini wengi hawabebeki! Tunatakiwa kuwa competence kwenye soko la elimu na kazi kwa ujumla na siyo kubebwa na uzawa! Na kama tupo vizuri Kwanini na Sisi tusivamie huko Asia, Ulaya na kwengineko?!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…