Hili la Wabunge 50 kutoka Zanzibar yenye wapiga kura wasiozidi laki tano, wakati Temeke wapiga kura 1.5M Wabunge 6 limewaliza Watanzania

Hili la Wabunge 50 kutoka Zanzibar yenye wapiga kura wasiozidi laki tano, wakati Temeke wapiga kura 1.5M Wabunge 6 limewaliza Watanzania

Bush Dokta

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2023
Posts
24,831
Reaction score
45,154
Wakati Watanzania wanaendelea kula Dozi ya Ubongo( Brain Vitamins) kutoka kwa Wakili Nguli na Mpigania haki Mh Makamu Mwenyenyekiti wa Chadema kwenye ziara zake.

Mh Lissu ambaye yuko ziarani ktk harakati zake za Kuendesha Maandamano mikoa yote Tanzania na mikutano ya kisiaaa ametoa Takwimu zilizoacha midomo wazi watanzania.

Hizi ni Takwimu ambazo zilikuwa hazifahamiki kwa wengi.

Kwamba Zanzibar inachangia idadi ya Wabunge wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania takribani 80 wakati ina idadi ndogo ya wapiga kura na ukubwa wa majimbo mdogo sana.

Amesema kuna baadhi ya majimbo yanawapiga kura elfu 7 tu huku Temeke jimbo moja lina wapiga kura zaidi ya Laki nne.

Taarifa hizi zimewaliza watanzania wengi waliokuwa mkutanoni na wengi waliofikiwa na taarifa hizi kupitia mitandao ya kijamii na vyomvo vya habari.

Mh Lissu hoja yake ilikuwa kufafanua namna serikali inayotumia pesa nyingi za walipa kodi kunemeesha baadhi ya watu bila sababu za msingi badala ya kuwaletea maendeleo Watanzania.

Haichukui nafasi ya Mhasibu Mkuu wa Benki kutambua kuwa kimahesabu Kama Nchi tunakula Hasara.

Kwamba Nchi yenye malengo inawezaje kutumia pesa nyingi kiasi hiki ku secure vyeo na anasa wakati ni Nchi maskini inayotegemea mikopo kwa asilimia kubwa?
 
Ni fikiria waliwazanini kufanya hivyo sielewi
Kama ambavyo nasikia Arusha au hata Mbeya itagawanywa hivi karibuni upande mmoja wa Peter Msigwa na huu mwingine wa Dokta Tulia ili kila mtu apate.😂😂😂
 
Back
Top Bottom