Wewe tanguliza sheria kama hirizi utajua hazina maana wakati zinafika mtakuwa wewe na mmeo/mkeo mmelala njaa na kupata tabu sana
Dharahu wanazofanya hao jamaa kwa wengine na hapa ni kwa watumishi wa umma na kusema sheria zina nguvu madhara yake wakati mwingine ni makubwa sana. Nimerejea alichofanya yule jamaa wa Tunisia kujikoka moto mbele ya ofisi ya serikali,nikarejea ya Hamza wa ubalozi wa Ufaransa pale (sina picha wala video ya tukio lile) ni matokea ya dharahu za kupindukia.
Nikiwa nyumbani Musoma miaka ya 2005 km siyo 2006 mwanzoni.
Kuna jamaa walikuwaga na kawaida ya kuwinda nungunungu mashambani kwa kutumia mbwa.
Sasa siku 1 kuna mzee m1 kwa jina Kawawa akajitoa ufahamu akawapigia yowe ya wizi kisa tu walipita eneo alilokuwa amefunga mbuzi wake.
Km unavyojua mjini habari za yowe,hakuchukua muda jamaa wale wawili wakawa wameuliwa.
Sasa miongoni mwa wana yowe baadhi wakasema mbona hawa jamaa mara nyingi huwa wanawinda nungunungu humu kwenye mashamba ya mihogo,leo wamekuwa wezi?
Basi taarifa zikawa zimefika kwao hao marehemu,ni nje kidogo ya mji.
Ndugu jamaa na marafiki wakaja,wakauliza,hawa vijana leo hii wamekuwa wezi?
Huyo Kawawa kwakuwa mbuzi wake walikuwa karibu na eneo la tukio akasema walikuwa wameiba mbuzi wangu.
Basi,watu wakasema sawa,wakafanya taratibu na kuchukua ile miili na kwenda kuzika.
Miaka mi5 baadaye Dunia nzima ilishuhudia kilichotokea kwa Kawawa mwaka 2011,watu 17 ikiwa ni watu wazima na watoto,mpaka mifugo.
Anayetaka kushuhudia ni kwa nini kuheshimiana ni mhimu aingie mtandaoni ajionee mambo yalivyo kuwa.
Lkn pia nadhani wanao unga mkono dharahu tunazofanyiwa watumishi ni wale ambao wametokea Newcastle families.
Hawajawahi kupita visiwani huko ndanindani na migodini wajionee jinsi ambavyo waliowahi kufanya matukio ya hatari wanavyoishi vyema na mkono wa sheria haujawahi hata kujaribu kuwafikia,na sidhani km utaweza kuwafikia kwa7bu tu ili defender itoke kituoni tu mlalamikaji unatakiwa utoe fedha ya mafuta.
Jamani,TUHESHIMIANE TU,DHARAHU ETI KWAKUWA TU KUNA SHERIA INAFIKIA WAKATI HAZISAIDII NA NDIYO MAANA UTAMUONA KIONGOZI WA SERIKALI AKIWA SAMBAMBA NA VIONGOZI WA DINI KWA JINA WAKIITWA KAMATI YA AMANI.