Hili la walimu kuchangishwa michango ya Mbio za Mwenge kwa lazima likomeshwe

Hili la walimu kuchangishwa michango ya Mbio za Mwenge kwa lazima likomeshwe

Nani awasemee walimu, au wakasemewe wapi? Sehem gani mwalimu wa nchi hii walimu wanasikilizwa? Nani boss wa mwalim?

Nchi hii mwalim hana mahali pakupeleka malalamiko yeyote

Mwalimu anadharauliwa na mtu kuanzia mwanafunzi mwenyewe, mzazi, jamii na kila mtu.

Sekta ya elimu kwasasa ndio sekta yatima zaidi

Kosa dogo atakalofanya mwalimu litatangazwa nchi nzima

Shule za private kuna walimu wa degree wanalipwa hadi laki 2 na kazi anafanya kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa nne usiku anasimamia prepo na kuna sometimes prepo pia ina ratiba ya vipindi ili kumaliza mada mapema,

Walimu ,walimu walimu walimu, walimu wa nchi hii

Nasema hivi

KWAKUWA SEKTA YA UALIMU IMEDHARAILIWA KWA KIASI HIKI ANGALIENI KWA SASA PRODUCT ZINAZOTOKA SHULE KWA SASA, mwalimu amekuwa sio mlezi tena bali kila mtu afe kivyake na mtoto wake.
Mkuu umeongea point sana
 
CWT ilipaswa kuingilia kati kakini "cwt" nilichama la kukarushwa nashangaa tamisemi na takukuru wakowapi!!
Hawa wajinga wanaendesha mambo yao kianolojia ili kuiba kirahisi. Wanapeana pesa mkononi eti ili kufanya malipo yakiasi kirudishwacho kwa walimi. Kama tuna takukuru kwanini wasiwalazimishe waende kidigitali
Kama chama cha walimu kilipaswa kuwa cha mfano wengine kuiga lakini kinyume chake kimekuwa ni chama chakipumbafu mmmno kitoacho mfano wahovyo na wa aibu kwa taifa kuliko chama kingine chochote hapa nchini yaani kinafuatia baada ya chama cha freemason kwa upuuzi...
 
Kila mtu ana uhuru wa kusema atakavo ila wakati mwingine walimu hawapendi kabisa kulipa iyo michango ila ili kuepusha shari na wakubwa inambidi alipe tu maisha ya endelee maana elfu tano sio kitu kiivo unaweza usinipe alafu unaitwa halmashauri unatumia nauli elfu kumi kwenda na kurudi sasa apo kipi bora kulipa 5000 au uende kwa kwa wakubwa utumie 10000 nauli?
 
Kila mtu ana uhuru wa kusema atakavo ila wakati mwingine walimu hawapendi kabisa kulipa iyo michango ila ili kuepusha shari na wakubwa inambidi alipe tu maisha ya endelee maana elfu tano sio kitu kiivo unaweza usinipe alafu unaitwa halmashauri unatumia nauli elfu kumi kwenda na kurudi sasa apo kipi bora kulipa 5000 au uende kwa kwa wakubwa utumie 10000 nauli?
Bora nitoe elfu kumi kwenye nauli ila sio kufaidisha matapeli ya mbio za mwenge
 
Watu wenyewe hawajielewi mnahangaika nao wa nn, sisi kuna boya mtendaji alikuja kwenye frem et anakusanya pesa ya Mwenge tukamwambia ishia huko huko kabla hatujakupasua vipande, yule mtendaji hakurudi tena.
Hizo Hela watumishi wote wa idara zote wanachanga,Cha ajabu nini hapo
 
Mkurugenzi wa Halmshauri ya Ifakara ameandikia Barua Walimu wa shule kutaka walipe mchango wa kufanikisha shughuli za Mwenge. TAMISEMI mmeagiza Halmshauri kufanya hivi? Huo Mwenge hauna bajeti? Mbona hamna huruma na walimu nchi hii? Barua hii ibatilishwe, fedha zirudishwe kwa walimu.

Na hii sio tuu ifakara, Gairo huko DMO anawalazimisha watumishi wa Afya kutoa mchango wa Mwenge, Morogoro DC Mkurugenzi anawalazimisha walimu kutoa michango ya Mwenge na hii inaonekana ni maeneo mengi nchini na sio mwaka huu tu, kila mwaka wakati wa mbio za Mwenge walimu na watumishi wa Umma walio chini ya TAMISEMI wanachangishwa fedha.

Jambo hili la walimu na watumishi wa umma chini ya TAMISEMI kuchangishwa michango ya namna hii linapaswa likomeshwe. TAMISEMI wapo kimya, Waziri yupo kimya, huenda jambo hili wanalijua na wao ndiyo wameagiza.

Halmshauri kuagiza michango ya namna hii huku TAMISEMI ikiwa kimya, sisi tutajua TAMISEMI ndiyo wameagiza.

1. Tunataka kujua msimamo wa Serikali/TAMISEMI katika hili.

2. Kama TAMISEMI hawahusiki, tunataka tuone waraka wa kubatilisha michango ya namna hii kwa Halmshauri zote nchini.

Chama cha Walimu kipo kimya, kimekuwa butu!

Tangu kuondolewa kwa Katibu wa CWT, Deus Seif kutokana na mashtaka na shutuma zilizokuwa zinamkabili kabla ya kushinda Rufaa ya kesi yake, Chama cha Walimu kimekuwa na migogoro mikubwa sana hadi sasa. Kwa sasa ni kama kime-paralyze na hakiwezi kufanya jambo lolote kutetea maslahi ya walimu.

Migogoro ni mikubwa sana ndiyo maana Rais Samia aliona ni busara kutatua migogoro hiyo kwa viongozi wote wa sasa kuwapa U-DC kuanzia Rais wa CWT Leah Ulaya aliyeteuliwa kuwa DC wa Mbogwe, kaimu Katibu wa CWT Japhet Maganga aliyeteuliwa kuwa DC Kyerwa, Makamu wa Rais wa CWT Dinah Mathamani aliyeteuliwa kuwa DC wa Uvinza na Cornel Maghembe.

Waliokubali uteuzi wa Rais tena baada ya kujifiiria sana ni Makamu wa Rais CWT Ndug. Dinah Mathamani na Cornel Maghembe, ila Rais wa CWT Leah Ulaya na Kaimu Katibu wake Ndug. Japhet Maganga waligomea uteuzi wa Rais wakaandika barua kwa Rais kumshukuru kwa uteuzi na wakisema wametosheka na nafasi zao.

Unaweza kuwaza kipi ambacho wanakipata huko CWT wakati hawafanyi kazi zozote ingawa sasa wana kesi ya kimaadili inaendelea.

Na hawa viongozi ndiyo waliomponza RC Omary Mgumba wa Tanga, mlikuwa mnajiuliza kwanini aliondolewa wengi wakisema ni issue ya yeye kukemea madaktari wakati wa ajali ila kuna sababu nyingine, baada ya uteuzi wa Rais kwa viongozi hao wa CWT.

Viongozi hao walienda kufanya kikao Tanga, wakamualika RC Mgumba, RC akatamka wachape kazi hata kama Rais amewateua wao bado ni viongozi wa CWT hii nayo ilikuwa sababu ya utenguzi wa RC Mgumba.

Leo hii Rais Leah Ulaya na Katibu wake wanataka kuwaondoa watendaji wote wa CWT Makao Makuu sababu eti ni watu wa Katibu aliyepita Deus Seif, hivyo wanataka waweke watu wao.

Kesi nyingi za walimu Mahakamani zilizo chini ya CWT haziendelei sababu wanasheria hawalipwi. Walimu wana changamoto lukuki CWT ipo kimya, viongozi wa CWT wananufaika kwa michango ya walimu ikiwa hawafanyi kazi ya kuwasemea na kuwatetea walimu.

Walimu nyie ndiyo mlitufundisha hadi sisi tumefika hapa tulipo. Sasa kwanini mnakubali kuongozwa na watu wa CWT wasio na uwezo? Kwanini mnakubali kudhulumiwa? Kwanini mnakubali kuchangishwa michango ya namna hii, kwanini mnakubali kuonewa namna hii?

View attachment 2567451
Mbona imeandikwa ki michapo michapo?

Amandla...
 
Asitokee hapa mtu kwasababu tu yup kwenye chama au taasisi yoyote ya umma au binafsi akaleta sheet kuhusu watumishi wa umma bila kuishi huo mfumo atakuwa anadanganya. Nimuulize nondo angekuwa mwalimu huko marinyi angefanyaje? Nondo ulishawah kushiriki sherehe ya mai most?lengo la shetehe maazimisho yale nn? President appointee.kama DC Anakuja pale kumuakilisha nani? Unajua mabango ya siku ile yanaansikwa wapi? Ni kwa DSO Akishikiana na DAS? Nondo anajua haha?
Jifunze kuandika mkuu wa halamshauri ya Chattle, naona unapuyanga errors kibao [emoji23][emoji23]
 
Huwezi kupinga uonevu wa namna kama unaogopa viongozi wa Halmshauri.
Ktk vitu ambavyo huwa ninasumbuana na msimamizi wangu ni michango ya aina hii.

Baada ya kuona post hii nimeongea na kaka yangu yuko Mkoani Ruvuma,jamani sikufahamu km kuna watumishi wa mma wanateswa namna nilivyoelezwa.

1 Halmashauri ya Wilaya Mbinga sii tu watumishi wanalazimishwa kuchangia mbio za mwenge,bali pia wanachangishwa ujenzi wa ofisi za CCM,uchaguzi wa CCM.

2 Tunduru wao mtumishi km hajafikisha miaka mi tatu kazini halipwi fedha za nauli za likizo na haruhusiwi kuomba likizo pia.

3 Mbinga ni haki ya mwanafunzi wa kike kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Mwl na wazazi hutoa baraka hasa Mwl akiwa tayari kumhudumia huyo mwanafunzi mahitaji yake lkn pia hata mama akiwa anapata japo sukari,kitenge nk.

Kimbembe ni kwa Mwl ambaye siyo mwenyeji wa huko,hapo kunakuwa na vita kali ya chini kwa chini kati ya wenyeji na huyu mgeni na ikatokea binti akawa na kibendi,hapo wana wanakuchezesha mpaka unawatafuta Maboto,Plantinum na wengineo ili umalize soo. Wajomba wanachochea unavuta 6m,kumbe mzazi ana ambulia 600K inayo baki mchocheaji ananeemeka,ikumbukwe hiyo michakato unakuwa unafanya bila uhuru.

3 Huko Ruvuma kuvujisha mitihani ni lazima,ni maagizo,upende usipende Maafisa elimu wanataka ufaulu wa 100% . Sasa ndugu yangu kaenda huko na misimamo na taratibu za Mara,weee anasema afisa anaweza kuondoa chapu ndani ya chumba cha mtihani.

Sasa nije kwenye suala hili uliloleta hapa.

Binafsi niliamini kuwa HAMZA YULE WA PALE UBALOZINI ALITOA SOMO LKN NAONA KUMBE BADO TUNADHARAHULIANA SANA TU.

MIMI NIMEMWAMBIA KAKA ASITOE HALAFU SIKU AKIJIROGA HUYO SIJUI MKURUGEGENZI KUMUITA KWA AJILI YA KUMUULIZA KUHUSIANA NA HUO WIZI WAKE ASISAHAU KWENDA NA PODA NYEUSI LKN PIA NA KISU CHENYE MAKALI KUZIDI CHA BUCHANI.

WANASHINDWA WAPI KUCHUKUA HIZO FEDHA JUU KWA JUU KABLA HAZIJAWAFIKIA WATUMISHI HAWA?

JE NI NANI HUWA ANAKAGUA MATUMIZI YA HIZI FEDHA?

JE,NI KWELI KWAMBA BUDGET YA MWENGE INAYO WASILISHWA BUNGENI HAITISHI?


ONA MATUMIZI YA HIZI FEDHA SASA;
1 KUWAPA RUSHWA WENYE MWENGE WAO ILI WAFUMBIE MACHO UHOVU NA UBADHILIFU.

2 KUNUNUA POMBE NA ANASA ZINGINE ZA NAMNA HIYO KWENYE MIKESHA YA MWENGE.

AJABU ZAIDI JAMAA ANASEMA ILI KUWAFUMBA MACHO MKURUGENZI KAWAAMBIA KUNA ACCOUNT IMEFUNGULIWA KWA AJILI YA HIZO FEDHA.

MIMI NAIOMBA SERIKALI IANGALIE UHALALI WA HILI JAMBO,KINYUME NA HAPO KUNA MTU ATAJITOA MUHANGA ILI AWAKOMBOE WENGI NA NIMEMWAMBIA MSIMAMIZI WANGU HUKU NILIKO KUWA NITACHOMA MTU KISU NA SITA KICHOMOA HATA AKIWA AMESHAKUFA,NITANG'ANG'ANIA MPAKA NAFIA HAPOHAPO NIMESHIKILIA HICHO KISU HUKU KIKIWA KIMEZAMA NYAMANI MWAKE.
 
Mimi kws Upande wangu nina mtizamo tofauti kwa izoefu. Kwa HALMAMSHURI huko WILAYANI mkesha wa Mwenge ndio FIESTA yao, ndio mtoko wao, ndio SHEREHE KUBWA inayowakutanisha watumishi wa Kada zote katika Halmashauri kucheza, Kunywa, kufanya michezo nk.
Mind you fedha inayochangwa inatumika na Kamati zao wao wenyewe kwa ajili ya kununua chakula chao na Vinywaji vyao. PESA INAYOCHANGWA HAILIWI NA MWENGE bali hutumika kwa matumizi yao ya Kibinadamu wakati wa Mkesha ikiwemo kukodi Mahema, Kuleta Msanii Mkubwa Eg.Mbosso, kukodi PA Mziki mnene CD 700, Kuleta Wachekeshaji Eg Braza K.
Sasa sisi tuliopo Dar kinachotuwasha ni kipi, sie tuna mitoko ya Fiesta, Mara Mechi Taifa, Mara Beach Kidimbwi nk nk yaani kila siku ni sherehe.
Tuacheni Watumishi nao watumie Mwenge kama sehemu ya Kujitoa Out na tuelewe kuwa MWENGE HAUTAFUNI PESAAAA na bajeti yake haitoki mawilayani wala haimtegemei mwalimu wala nesi. Hiyo michango yao ni maandalizi yao wao kwa matumizi yao.
Vp kwa mtumishi ambaye hana mipango na ulivyo viainisha,inakuwaje kwa upande wake?
 
Tulia uandike vizuri mkuu.
Kwani hizo sherehe huwa hazina budget?

Ni kwa nini kifanywe kitu ambacho uwezeshwaji wake ni mgumu?

Masuala ya mabango na fedha ya mtumishi vinahusianaje?

Kwani haiwezekani kukata hiyo fedha ya mbio za mwenge juu kwa juu mpaka waende kumharibia mtumishi budget zake binafsi?
Asitokee hapa mtu kwasababu tu yup kwenye chama au taasisi yoyote ya umma au binafsi akaleta sheet kuhusu watumishi wa umma bila kuishi huo mfumo atakuwa anadanganya. Nimuulize nondo angekuwa mwalimu huko marinyi angefanyaje? Nondo ulishawah kushiriki sherehe ya mai most?lengo la shetehe maazimisho yale nn? President appointee.kama DC Anakuja pale kumuakilisha nani? Unajua mabango ya siku ile yanaansikwa wapi? Ni kwa DSO Akishikiana na DAS? Nondo anajua haha?a
 
Ccm acheni kunyanyasa walimu wetu, toeni hela kwenye ruzuku yenu mchangie huo mwenge.
 
Yaani nchi hii kuna mambo ya ajabu sana. Walimu nao wapo kimya kwasababu wanatumiwa kama toilet paper.

Kwa sababu sio mtumishi wa umma ndio maana una Shangaa !!
 
Umenena kweli bwana Nondo. Ila tatizo kubwa liko kwa walimu wenyewe. Nadhani tangazo linajieleza kuwa siyo lazima ni hiari.

Walimu wetu wanapenda kujipendekeza sana ili wateuliwe ukuu au umeki.

Kama wangeungana pamoja kukataa huu uhuni nadhani tungekuwa mbali sana.

CWT si mtetezi wao tena. Ni mnyonyaji wao.

Hebu ona Katibu wa CWT wilaya mojawapo ya jiji la Mwanza bwana Onesmo Makota ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Maswa. Je ataweza kuishurutisha serikali ya CCM?
Mgongano mkubwa sana wa maslahi
 
Kama mwenge unamulika mipaka ya nchi na kuondoa chuki pale penye udhia kama wasemavyo wakulungwa lakini nimaoni yangu kwamba MWENGE UNAPOPITA HUFANYIKA NGONO SANA HIVYO KUONGEZA UWEZEKANO WA MAAMBUKIZI YA VVU.
 
Back
Top Bottom