Hili la walimu kuchangishwa michango ya Mbio za Mwenge kwa lazima likomeshwe

Hili la walimu kuchangishwa michango ya Mbio za Mwenge kwa lazima likomeshwe

Asitokee hapa mtu kwasababu tu yup kwenye chama au taasisi yoyote ya umma au binafsi akaleta sheet kuhusu watumishi wa umma bila kuishi huo mfumo atakuwa anadanganya. Nimuulize nondo angekuwa mwalimu huko marinyi angefanyaje? Nondo ulishawah kushiriki sherehe ya mai most?lengo la shetehe maazimisho yale nn? President appointee.kama DC Anakuja pale kumuakilisha nani? Unajua mabango ya siku ile yanaansikwa wapi? Ni kwa DSO Akishikiana na DAS? Nondo anajua haha?
Hofu na woga tuu ,Mwalimu wangu alinifundisha yupo Igunga Paul Msabila alipinga unyonyaji wa CWT amekamatwa amewekwa ndani Kwa agizo la Mkurugenzi siku 6 ,akatolewa lakini bado msimamo wake upo palepale akipinga CWT . Hamuwezi kuleta mabadiliko kama wengine kama ww ni waoga hata kuhoji
 
Kama uliacha sawa. Ila ungekuwa umefukuzwa, ndiyo ungeona namna mchakato wake ulivyo mgumu.

Inaweza kuwa rahisi sana kwa mwajiri kumfukuza mtumishi wa umma, kwa makosa ya jinai. Ila siyo kwa kwa kugomea kuchangia mbio za mwenge.

Hapo watu wanatishiwa tu nyau, na mwisho wa siku watumishi waoga watatoa, na wale wanaojiamini hawatatoa! Na hakuna chochote kitakacho watokea.
Sahihi kabisa
 
Walimu ni kundi la kuliombea,90%ya walimu uwezo wa kujikimu hauzidi mwezi mmoja kwa maana kuwa endapo mwalimu hatalipwa mshahara Kwa mwezi mmoja kuna probability kubwa akafa Kwa msongo wa mawazo au njaa, mishahara wamechukulia mikopo mpaka mwisho na wamekabidhi ATM card kwenye taasisi za fedha kama dhamana ya mikopo, na wanadaiwa kwenye maduka n.k,

CHAKUSHANGAZA Bado mwajiri analazimisha mchango wa mwenge,fedha hiyo inaenda kuchezewa siku ya mwenge Kwa Kuna pombe na vyakula siku ya mkesha WHILE aliyetoa mchango ameshindwa hata kuwanunulia watoto wake sukari. Huu ni uonezi mkubwa sana,jambo halipo kisheria lingekuwepo basi watumishi wangekatwa kwenye mishahara Yao,huu ni wizi wa mchana kweupe.
 
Mkurugenzi wa Halmshauri ya Ifakara ameandikia Barua Walimu wa shule kutaka walipe mchango wa kufanikisha shughuli za Mwenge. TAMISEMI mmeagiza Halmshauri kufanya hivi? Huo Mwenge hauna bajeti? Mbona hamna huruma na walimu nchi hii? Barua hii ibatilishwe, fedha zirudishwe kwa walimu.

Na hii sio tuu ifakara, Gairo huko DMO anawalazimisha watumishi wa Afya kutoa mchango wa Mwenge, Morogoro DC Mkurugenzi anawalazimisha walimu kutoa michango ya Mwenge na hii inaonekana ni maeneo mengi nchini na sio mwaka huu tu, kila mwaka wakati wa mbio za Mwenge walimu na watumishi wa Umma walio chini ya TAMISEMI wanachangishwa fedha.

Jambo hili la walimu na watumishi wa umma chini ya TAMISEMI kuchangishwa michango ya namna hii linapaswa likomeshwe. TAMISEMI wapo kimya, Waziri yupo kimya, huenda jambo hili wanalijua na wao ndiyo wameagiza.

Halmshauri kuagiza michango ya namna hii huku TAMISEMI ikiwa kimya, sisi tutajua TAMISEMI ndiyo wameagiza.

1. Tunataka kujua msimamo wa Serikali/TAMISEMI katika hili.

2. Kama TAMISEMI hawahusiki, tunataka tuone waraka wa kubatilisha michango ya namna hii kwa Halmshauri zote nchini.

Chama cha Walimu kipo kimya, kimekuwa butu!

Tangu kuondolewa kwa Katibu wa CWT, Deus Seif kutokana na mashtaka na shutuma zilizokuwa zinamkabili kabla ya kushinda Rufaa ya kesi yake, Chama cha Walimu kimekuwa na migogoro mikubwa sana hadi sasa. Kwa sasa ni kama kime-paralyze na hakiwezi kufanya jambo lolote kutetea maslahi ya walimu.

Migogoro ni mikubwa sana ndiyo maana Rais Samia aliona ni busara kutatua migogoro hiyo kwa viongozi wote wa sasa kuwapa U-DC kuanzia Rais wa CWT Leah Ulaya aliyeteuliwa kuwa DC wa Mbogwe, kaimu Katibu wa CWT Japhet Maganga aliyeteuliwa kuwa DC Kyerwa, Makamu wa Rais wa CWT Dinah Mathamani aliyeteuliwa kuwa DC wa Uvinza na Cornel Maghembe.

Waliokubali uteuzi wa Rais tena baada ya kujifiiria sana ni Makamu wa Rais CWT Ndug. Dinah Mathamani na Cornel Maghembe, ila Rais wa CWT Leah Ulaya na Kaimu Katibu wake Ndug. Japhet Maganga waligomea uteuzi wa Rais wakaandika barua kwa Rais kumshukuru kwa uteuzi na wakisema wametosheka na nafasi zao.

Unaweza kuwaza kipi ambacho wanakipata huko CWT wakati hawafanyi kazi zozote ingawa sasa wana kesi ya kimaadili inaendelea.

Na hawa viongozi ndiyo waliomponza RC Omary Mgumba wa Tanga, mlikuwa mnajiuliza kwanini aliondolewa wengi wakisema ni issue ya yeye kukemea madaktari wakati wa ajali ila kuna sababu nyingine, baada ya uteuzi wa Rais kwa viongozi hao wa CWT.

Viongozi hao walienda kufanya kikao Tanga, wakamualika RC Mgumba, RC akatamka wachape kazi hata kama Rais amewateua wao bado ni viongozi wa CWT hii nayo ilikuwa sababu ya utenguzi wa RC Mgumba.

Leo hii Rais Leah Ulaya na Katibu wake wanataka kuwaondoa watendaji wote wa CWT Makao Makuu sababu eti ni watu wa Katibu aliyepita Deus Seif, hivyo wanataka waweke watu wao.

Kesi nyingi za walimu Mahakamani zilizo chini ya CWT haziendelei sababu wanasheria hawalipwi. Walimu wana changamoto lukuki CWT ipo kimya, viongozi wa CWT wananufaika kwa michango ya walimu ikiwa hawafanyi kazi ya kuwasemea na kuwatetea walimu.

Walimu nyie ndiyo mlitufundisha hadi sisi tumefika hapa tulipo. Sasa kwanini mnakubali kuongozwa na watu wa CWT wasio na uwezo? Kwanini mnakubali kudhulumiwa? Kwanini mnakubali kuchangishwa michango ya namna hii, kwanini mnakubali kuonewa namna hii?

View attachment 2567451
Acha kazi kwenye seriakali kajiunge na CHADEMA huko. Yaani umepanga na mwenye nyumba anapata msiba wewe unawezaje kuendelea na birth day party halafu uendelee kuwa mpangaji? Mnajitoa ufahamu wakati mwingine. Mtumishi wa serikali kweli ugomee shughuli ya serikali?
 
Acha kazi kwenye seriakali kajiunge na CHADEMA huko. Yaani umepanga na mwenye nyumba anapata msiba wewe unawezaje kuendelea na birth day party halafu uendelee kuwa mpangaji? Mnajitoa ufahamu wakati mwingine. Mtumishi wa serikali kweli ugomee shughuli ya serikali?
Kwahiyo mwenge ni msiba wa serikali?ww ni miongoni mwa watu waliolifikisha taifa hapa lilipo Kwa mawazo mfu kama hayo,Kila kitu kitu mnadifend Kwa hoja uchwara
 
Kwahiyo mwenge ni msiba wa serikali?ww ni miongoni mwa watu waliolifikisha taifa hapa lilipo Kwa mawazo mfu kama hayo,Kila kitu kitu mnadifend Kwa hoja uchwara
Sijui ulisoma wapi maana uelewa wako ni mdogo sana
 
Kila mtu ajiandae na halmashauri yake kutoa mchango wa hiari kwajili ya mwenge wa Uhuru
IMG-20230324-WA0001~2.jpg
 
Walimu watasema nn wakati waajiri wao wanashirikiana na majambazi kuwafilisi ndio mana walimu wanachelewa kupata maendeleo kamshahara kenyewe kadogo halafu akafiki hata mifukoni wajanja wajanja wanawaporaa very sad
Huwezi kusikia Waziri/RC/DC wamechangia mwenge hata mia wao huwa wanalipwa na hiyo michango
 
Tate mkuu
Nilifanya hayo yote nikiwa huko Halmshauri my 10 yrs nikiwa mtumishi nayajua na nimeptia mengi mkuu. Tusikutane jf watu wajifanye hapa kama ni new mesia nw huyu hajawahi kuyapitia
Kama umepitia hayo unayyosema umepitia... kuna shida gani mtu kusema hadharani kwamba kuna tatizo linaropaswa watu kulitazama...?
 
Hakuna watumishi wanaonewa kama waalimu.....na Wana Chama chao sijui kina msaada gani...... anyway acha wawanyooshe maana asilimia 90 wasimamizi wa chaguzi ni waalimu..... nadhani wanatapika vile vijisent wanavyopewa wakati wa chaguzi
 
Back
Top Bottom