Hili la Waziri husika kuhoji Yanga Kupeleka kikosi B Dodoma ni Sawa??

Hili la Waziri husika kuhoji Yanga Kupeleka kikosi B Dodoma ni Sawa??

Jana waziri Mwakyembe alilazimika kutoka uwanjani ( Jamhuri stadium Dodoma ) kwa hasira kisa YANGA wamepeleka uwanjani kikosi cha pili ili kucheza mechi ya kirafiki na kimbaini ya timu ya vikosi vya ulinzi,ameongea maneno mengi kwa hasira hadi watu wanashangaa na akasahau kuwa yanga inakabiliwa na mashindano makubwa ikiwemo jumapili dhidi ya mbao fc.
Mwambieni Yanga ni timu ya soka sio siasa. Na wizara ya michezo, haihitaji hasira!

Kama alikuwa ana hamu kubwa ya kumuona Kamusoko na Niyonzima, au Tambwe mabao na kijana wetu Msuva, basi ajisikie huru kujongea Kirumba tutakapokuwa tunachana mbao na chain saw
 
Nimejaribu kuperuzi habari mbalimbali za michezo nje na ndani ya nchi kubwa nililokutana nalo ni hili la Waziri husika Kuhoji uhalali wa Yanga kupeleka kikosi B kucheza na Kombani ya Majeshi Dodoma na kutoka sare ya 1-1 kikosi B cha Yanga kipo chini ya kocha Shedrack Nsajigwa.

Ukiangalia Kikosi cha wakubwa cha Yanga kinamichezo migumu&muhimu sana na pia wachezaji wengi muhimu walikua majeruhi,Sijui labda kama ni makubaliano yalifikiwa na upande mmoja ukavunja makubaliano hayo hapo sawa sheria ichukue mkono wake ila kama Kulikua hakuna makubaliano sidhani kama kuna haja ya kulichukulia hili suala siriazi kihivyo.

Sio mbaya tukitoa sapoti kwa Timu zetu za Vijana nao wapate michezo kadhaa ya kujiweka sawa,na pia timu inapopata majeruhi klabu ndio huingia gharama za matibabu kuanzia mwanzo mpaka mwisho.

Je wewe mdau wa mpira unasemaje juu ya hili?
[quote uid=430452 name="j kisumu" post=20867237]Ivi kwann huwa anapaniki na kijibu maswali kwa jazba kwamfano kwenye mkutano wa Roma baada ya kutekwa waandishi walikua wanamuuliza maswali kuhusu ahadi ya bashite kwamba kina Roma wangepatikana kabla ya j Pili . au tatizo ni ile tindikali au anafanya kazi kwa maelwkezo ya nani[/QUOTE]<br Huyo Waziri boya tu siku hizi. Jana tena kakurupuka kuwataka viongozi wa Yanga kutoa maelezo kwa nini walipeleka kikosi B kule Dodoma kucheza na kombaini ya Vikosi vya Ulinzi kana kwamba Yanga ni timu ya Serikali. Kwani wakati Yanga inawasajili hao wachezaji yeye alishirikishwa? Tunakuwa na mashaka kwamba alikuwa na nia ovu kwa timu yetu wakati imebanana na michezo ya VPL na ile ya FA ili wachezaji wetu waumizwe na kufanya kikosi kuwa finyu. Kama kuna wachezaji alitaka awaone basi namshauri aende CCM Kirumba Jumapili akajionee kinachomkuta Mbao FC kupitia kwa hao wachezaji anaowataka. SHAME ON U MWAKYEMBE..!!
 
Mwambieni Yanga ni timu ya soka sio siasa. Na wizara ya michezo, haihitaji hasira!

Kama alikuwa ana hamu kubwa ya kumuona Kamusoko na Niyonzima, au Tambwe mabao na kijana wetu Msuva, basi ajisikie huru kujongea Kirumba tutakapokuwa tunachana mbao na chain saw
Nadhani rangi zinamchanganya anafikiri yanga ipo chini ya UVCCm
 
si kwa ubaya

huyu mzee apumzishwe, ubongo usha choka kwa sumu na kukumbatia maovu. mtu hadi anakana andiko lake lazima ana matatizo
 
Hayo maneno ulimsikia akiyasema au umeyasikilizia wapi?
Ikiwa huna ufahamu na jambo lililo wekwa hapa bora upite kimya, kwa taarifa yako ni kwamba Mh. Waziri kahojiwa na kutamka kwamba ametoka mapema uwanjani kwa sababu Yanga wamepeleka kikosi cha pili, amekwenda mbali zaidi kwa kuwataka viongozi wa timu wakajieleze kwake kwa kosa hilo
 
Nakushangaa unanisema sababu ya kuuliza halafu unanijibu. Ungejibu tu ungekatika vidole.

Nani alikuambia kuuliza swali ni ujinga?
 
Jana waziri Mwakyembe alilazimika kutoka uwanjani ( Jamhuri stadium Dodoma ) kwa hasira kisa YANGA wamepeleka uwanjani kikosi cha pili ili kucheza mechi ya kirafiki na kimbaini ya timu ya vikosi vya ulinzi,ameongea maneno mengi kwa hasira hadi watu wanashangaa na akasahau kuwa yanga inakabiliwa na mashindano makubwa ikiwemo jumapili dhidi ya mbao fc.

Msamehe huyo alishapitiwa na polonium pentoxide or whatever it was
 
Anakasirika wakati hata uwanjani hajalipa kiingilio.. je hiyo mechi ilikuwa ya kugombea kitu gani??
 
Jana waziri Mwakyembe alilazimika kutoka uwanjani ( Jamhuri stadium Dodoma ) kwa hasira kisa YANGA wamepeleka uwanjani kikosi cha pili ili kucheza mechi ya kirafiki na kimbaini ya timu ya vikosi vya ulinzi,ameongea maneno mengi kwa hasira hadi watu wanashangaa na akasahau kuwa yanga inakabiliwa na mashindano makubwa ikiwemo jumapili dhidi ya mbao fc.
Jee ametoa picha gani Kwa vijana Wa yanga???waziri hana uvumilivu hatufai.Ina maana yeye anabagua wachezaji???
 
Jee ametoa picha gani Kwa vijana Wa yanga???waziri hana uvumilivu hatufai.Ina maana yeye anabagua wachezaji???
Ametoa picha mbaya sana kwa hao vijana na kama waziri ambaye anajua kuwa msingi wa soka ni vijana angewasifu lkn kwa ubongo wake akafanya hayo aliyoyafanya
 
Back
Top Bottom