Hili la Yanga kupokea Sh.1,300 kati ya Sh.35,000 ya jezi, linatia uchungu sana

Hili la Yanga kupokea Sh.1,300 kati ya Sh.35,000 ya jezi, linatia uchungu sana

Mleta mada amesahau kusema kuwa Faida anayoipata GSM kwenye jezi anatumia:-

1. Kulipa mishahara wachezaji

2. Kusajili wachezaji wapya

3. Kuhudumia timu kwa Ujumla
Kwani Mikataba mingine ya Yanga na makampuni mengine haiingizi pesa? Kama zinaingia kazi yake ni ipi ikiwa pesa za GSM tu ndizo zinaendesha timu?
 
Kwani Mikataba mingine ya Yanga na makampuni mengine haiingizi pesa? Kama zinaingia kazi yake ni ipi ikiwa pesa za GSM tu ndizo zinaendesha timu?
Malizaneni na ponjoro wenu Mwamedi mambo ya Yanga hayawahusu.

Enjinia wa ukweli, Rais wa Yanga ndugu Hersi amewaahidi wana Yanga kujenga uwanja wa Kaunda pale jangwani utakaobeba watu 20,000.
 
Ukishaona mtu anaanza kuhesabu garama za kitu ambacho hajakichangia na waka hajui uzalishaji wake ni shilingi ngapi huyo kashavuka kwenye level ya unaskini ni mchawi bingwa.

Wewe unashani hiyo 35,000 wanayouza ni faida tupu, kumbuka na wao wamenunua kwa mzalishaji ili nao wapate faida wagawane na timu.

Kumbuka kati ya jezi walizonunua kuna zinazokula faida karibia zote kwa kuto kuuzika kama zile wachezaji wa azogawa bure kwenye mechi

Tambua hizi jezi wanaopata faida ni wale wazaliji wa jezi feki zenye low quality ambao ndio nyingi zipo mitaani na zimekuwa zikishindana na original
 
mambo ya pesa hayana umuhimu sana kama wachezaji hawalalamiki wanajaza makombe tu kabatini na wanamchinja mnyama Simba! hela ziende tu huko GSM burudani na raha ndo tubaki navyo mashabiki.

hakuna mwekezaji anaekuja kutafuta biashara yenye hasara

makombe kwanza pesa baadae! makombe huleta pesa!!
Sawa unasema makombe huleta pesa, hilo hakuna anaebisha. Je hizo pesa zinakwenda wapi?
 
Unawastuwa usingizini wakiamka wana mataji yote matatu, ni kichaa tu ndio anaweza kukuelewa.
Kana kwamba msimu uliopita Simba Sc hakuyachukua hayo matatu?

Zikija hoja mnakimbilia kwenye makombe utafikiri Simba Sc haijayachukua kwa miaka 100 hivi? [emoji23]
 
Mkuu binafsi sitaki kuingilia suala la mauzo ya jezi hilo ni makubaliano yao tu. Lakini napinga kuwa GSM anaweza kuwa ndo anapoteza.

Kumbuka GSM ni mdhamini wa klabu anatumia brand ya klabu kutangaza bidhaa zake sawa tu na wadhamini wengine kama nbc wanavyodhamini ligi au sportpesa anavyozidhamini simba na yanga.

Udhamini unalipa zaidi so GSM ananufaika kwa njia hiyo hayo ya jezi ni mengine

Udhamini wa GSM kwa Yanga hauwezi kumuingizia GSM faida ambayo inayoweza ku-supress expenses ambazo GSM anatumia kugharamia timu.

Gharama ya kuigharamia timu kwa mwezi kwa msimu uliokwisha ni takribani milioni 291 (salary structure iko ndani ya hii cost).

Je unataka kusema GSM anatengeneza faida zaidi ya milioni 291 kwa MWEZI?

Je biashara za gharib zina zaa faida kiasi gani kwa mwezi?

Fikiria kidogo

na wakati unafikiria kumbuka Eng Hersi alipata kusema kuwa Klabu inajiendesha kwa hasara.

Kwani Mikataba mingine ya Yanga na makampuni mengine haiingizi pesa? Kama zinaingia kazi yake ni ipi ikiwa pesa za GSM tu ndizo zinaendesha timu?

Pesa zinazo ptikana kutokana na Mikataba ni ndogo sana ukilinganisha overall expenses za klabu.

Kama tungetegemea hizo pekee basi leo hii Yanga wasingeweza kucover salary payments za kila mwisho wa mwezi

Mapato ya klabu pekee hayafikii hata asilimia 49 ya jumla ya gharama zitumikazo kuendesha klabu.

Na ndio maana Eng Hersi aliwahi kusema kuwa klabu kwa sasa inajiendesha kwa hasara.
 
Ina maana Kwa msimu uliopita Yanga ilihitaji mapato ya wastani wa 100 milioni Kwa wiki je! Ilo linawezekana?
 
Mleta mada amesahau kusema kuwa Faida anayoipata GSM kwenye jezi anatumia:-

1. Kulipa mishahara wachezaji

2. Kusajili wachezaji wapya

3. Kuhudumia timu kwa Ujumla
Umesahau kuwa anauza magodoro kupitia jina la yanga
 
Pesa zinazo ptikana kutokana na Mikataba ni ndogo sana ukilinganisha overall expenses za klabu.

Kama tungetegemea hizo pekee basi leo hii Yanga wasingeweza kucover salary payments za kila mwisho wa mwezi

Mapato ya klabu pekee hayafikii hata asilimia 49 ya jumla ya gharama zitumikazo kuendesha klabu.

Na ndio maana Eng Hersi aliwahi kusema kuwa klabu kwa sasa inajiendesha kwa hasara.
Hujui biashara gsm anauza sana magodoro yake kupitia yanga
 
Kwani yanga hiyo 1300 ni ya nini kila kitu analipa gsm hata angechukua zote sawa tu!
 
Back
Top Bottom