Hili ndilo Jicho langu la Kiufundi kabisa kwa matokeo ya leo na kwanini Mfalme wa Nyika amefanyiwa Kitu mbaya na Wamakonde

Manula kakosea nini jana? Point hii na ya sijui mwanasiasa imenifanya nikuone sio mtu wa mpira bali siasa kama kawaida... tuachie michezo mkuu, nenda siasani...
Lile goli kama kuamua kumlaumu mtu ni Kagere...hivi ulitegemea Manula kawapanga vizuri kwenye ukuta alafu yeye anakaa sehemu nyingine akiamini ukuta utafanya kazi alafu baada ya mpigaji faulo kupiga kagere anakwepa ulitaka manula afanyaje?

Ishu kubwa ni kujiamini kupita kiasi, wachezaji, viongozi na mashabiki...pia kuamini kwamba afrika kila mtu ashinde kwake..
 
Narudia tena hamna mbrazil mbovu hata mmoja pale, mmekaririshwa. Nafasi ya Kotei Fragha anacheza tena kwa akili na ufanisi mkubwa sana, nafasi ya Wawa anacheza Dos Santos vizuri sana. Shida ya Simba sio usajili ni kocha asiyekuwa na mbinu za kimpira.
 
Simba inatakiwa kwanza kuachana na mambo ya kizamani ya kiujanja ujanja kama kununjua tim pinzani na marefa au kupulizia dawa vyumba vya tim pinzan ili kupata ushindi.
Rubbish
 
Simba inatakiwa kwanza kuachana na mambo ya kizamani ya kiujanja ujanja kama kununjua tim pinzani na marefa au kupulizia dawa vyumba vya tim pinzan ili kupata ushindi.
"Ni bora kutumia yale ya kuruka ukuta au kutumia mlango usio rasmi sio"
 
Wamatopeni Uwanjani Mnaingia Na Matokeo Yenu.

Vibanda Umiza Navyo Mnaingia Na Matokeo Yenu Mfukoni.


Tulieni Dawa Ipenye
 
Kujiamn kupita kiasi ndicho kitu kilichowagharm simba
Nani aliyejiamini wachezaji au mashabiki, kama mashabiki hata wakijiamini hawana athari yoyote, kama timu kujiamini sio kweli, Simba wamecheza na Azam vizuri sana, wamesajili vizuri sana wamefanya preaseason vizuri sana, kama wangekuwa wanajiamini wasingefanya yote hayo. Kushindwa kufuzu ni matokeo ya kocha Aussems na anatakiwa awajibike haraka sana.
 
Hili la mkuu wa mkoa ni ubuyu tu wala siwezi kukuamini, mnachojua toka Aussems anaingia Simba huwa sio mzuri wa kupanga timu, kufanya subs na hata kimbinu ni mtupu sana na ndio maana walihombana na Masoud Djuma.
 
Akili za kimbumbumbu hizi.

Mtaani kupo kimya, zile fyokofyoko hakuna tena shenzi kabisa.
Mashabiki lazima waishangilie timu yao ikifanya vizuri hiyo ipo dunia nzima, au hujui mpira.
 
Kwenye kocha tu umekosea, aondoke tumuweke hata Matola anatosha ubingwa mapema kwa kikosi hiki.
 
Kujiamini kupita kiasi kivipi, wamesajili vizuri, wamefanya preseason vizuri, wamejituma sana kwa Azam, unasemaje wamejiamini sana
 
Umepost as if wapinzani ni timu ndogo sana. UD SONGO ni timu iliyokuwa pamoja zaidi ya miaka 3 na ilitishia mwaka jana kuitoa Tp Mazembe. Kosa la Simba kuacha kucheza Kagame yenye pressure na kuishia kirafiki tu. Timu bado ila wachezaji wapo.. kwa Manula nakubali sijawahi ridhika nae ila ana nyota ya kupendwa. Kimataifa Simba ilimhitaji Kaseja hata tubishe vipi. Okwi na Kotei kuachwa ni sawa kwani mwisho wao ungefika tu. Kiufundi nadhani Kanda acheze na Kagere na sio Chama. Mwisho tuna shida ya kutokubali kuwa football ni game na sio process. Matokeo yake hayapangiki on equilbria. Ndio maana inachezwa muda fulani kwa dakika fulani i.e ingechezwa muda mwingine tungeweza pata matokeo tofauti that’s game for the played time. Lets take a breath and move on. That’s football.
 
Vipi yule mpemba wako hakusema chochote?
 
Simba inatakiwa kwanza kuachana na mambo ya kizamani ya kiujanja ujanja kama kununjua tim pinzani na marefa au kupulizia dawa vyumba vya tim pinzan ili kupata ushindi.
Naona UGORO ulio bwia UMEKUZIDI NGUVU.
 
Narudia tena hamna mbrazil mbovu hata mmoja pale, mmekaririshwa. Nafasi ya Kotei Fragha anacheza tena kwa akili na ufanisi mkubwa sana, nafasi ya Wawa anacheza Dos Santos vizuri sana. Shida ya Simba sio usajili ni kocha asiyekuwa na mbinu za kimpira.
Unaweza kumlaumu kocha kihivyo iwapo tu una hakika usajili wa hao Wabrazili ni uamuzi wake. Inahitaji kocha mlokole mno kujenga imani kwa mchezaji asiye chaguo lake.
 
Mikia FC mtajiju aka kujibeba.
 
Vipi yule mpemba wako hakusema chochote?

Nimeshawahi kusema hapa kuwa Mimi cleverbright najuana sijui na Mpemba? Kama jibu lako ni ndiyo naomba uthibitishe na ukiweza uweke hapa hadharani na huo Ushahidi wako tafadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…