Hili neno "Umehonga" linawapa msongo wa mawazo wanaume. Tafadhali tusilitumie kwa wanaume wetu

Hili neno "Umehonga" linawapa msongo wa mawazo wanaume. Tafadhali tusilitumie kwa wanaume wetu

cutelove

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2017
Posts
3,448
Reaction score
7,972
Wanawake tuliowengi kwa sasa tunaendeshwa na hisia tu badala ya uhalisia

Kwa sasa tunaamini na kuhisi kwamba iwapo mmeo hakupi pesa ya matumizi ya kutosha au akakwambia hana pesa kwa muda huo basi neno litakalotamkwa na mke wake au mpenzi wake ni kuwa amehonga pesa wanawake na kumnyima mkeo au mpenzi.

Hata Kama mwanaume anafanya saving kwa ajili ya kununua kitu fulani au kujenga na mwanamke atataka ajue huwa anasave Wapi na huwa anasave kiasi gani na asipoona hiyo saving basi neno kuhonga hutamalaki katika ndoa hiyo au mahusiano hayo

kuna mwanaume alimwambia mke wake kuwa pesa aliyokuwa nayo amemtumia mama yake kiasi cha laki 4,lakini mwanamke hakuamini na kupiga sim kwa mama mkwe kuuliza Kama baba D amemtumia pesa na ni kiasi gani?

Nashauri wanawake wenzangu tusiwape wanaume wetu msongo wa mawazo kwa kuwatuhumu kuwa wanahonga ,sikatai kuwa hawahongi ila wapo wanaohonga serious ila wengine wanahonga pesa za ziada extra money

Tuepuke kuhonga,kila kitu Umehonga,akiteteleka jambo fulani amehonga,akisusua kulipa kodi ya nyumba au ada ya shule amehonga

Tusiamini katika kuhonga ili wanaume wasiwe na msongo wa mawazo
 
Public sympathy

Mwanaume alieoa ni lazima atimize mahitaji ya mkewe

Kama hawezi asioe, nothing more nothing less!

Ila kama anatimiza mahitaji na chenchi zinabaki basi asiulizwe pale anapohudumia na mistresses wa nje (asipangiwe idadi ya michepuko)
 
Wajibu wa mwanaume kuhudumia familia yake
Huduma ni wajibu ila matarajio ya kuwa kila anachomiliki mwanaume ni cha mwanamke si sahihi.

Kinachoteteresha ndoa nyingi ni wanawake kuhisi wana haki ya moja kwa moja katika kipato cha mwanaume kiasi cha kuhoji kila senti inapokwenda.

As long as mwanaume anatimiza majukumu yake, hapaswi kuhojiwa ama kuhitajika kutoa ithibati ya vipi katumia pesa yake.
 
Public sympathy
Mwanaume alieoa ni lazima atimize mahitaji ya mkewe
Kama hawezi asioe, nothing more nothing less!
Ila kama anatimiza mahitaji na chenchi zinabaki basi asiulizwe pale anapohudumia na mistresses wa nje (asipangiwe idadi ya michepuko)
Mmmmh
 
Hii ni kwa mujibu wa utaratibu wa jamii gani?Maisha yangekuwa simple kama hivi kesho tu dunia isingekuwepo.
 
Wanawake tuliowengi kwa sasa tunaendeshwa na hisia tu badala ya uhalisia...
 
Hii ni kwa mujibu wa utaratibu wa jamii gani?Maisha yangekuwa simple kama hivi kesho tu dunia isingekuwepo.
Dunia haijashikiliwa na Vitu vidogo vidogo kama ndoa nk. Mkuu
Taratibu za kijamii sio "laws of nature" zinabadilishwa TU na life linasonga.

Kama "Mwanamke" anapewa privilege ya kuhudumiwa na "Mwanaume" Unconditionally kama jamii Yako inavyotaka basi Hana haki ya Kumpangia Mumewe maisha.. kinyume na hapo Utakua ni unyonyaji na ubinafsi Kwa Mwanaume husika!
 
Hivi mwanamke anahitaji huduma zipi kutoka kwa mwanaume? (Nataka ni kupime kweli unajua huduma zako za msingi kama mwanamke).

Vp na ww unaujua wajibu wako kwa mwanaume au mwanaume atafaidika na nini kupitia kukutimizia mahitaji yako ya msingi?
Mbona viko wazi
 
Back
Top Bottom