Hili ni sahihi kweli kwamba England haina katiba

Maamuzi mbalimbali ya bunge, mabaraza na mahakama ndio yanafanya katiba ya Uingereza.
 
SI KWELI.
Katiba wanayo, isipokuwa Katiba yao haijaandikwa (Unwritten Constitution),kama 'document' nayo ni aina ya Katiba; sisi ya kwetu Tanzania imeandikwa (Written Constitution). Katiba isiyoaandikwa ni kama vile mila, desturi na mambo yote yanayofanywa na kufuatwa na jamii fulani kwa kurithishana kizazi hata kizazi na hayapo katika maandishi. Ndivyo ilivyo hata katika mila za makabila yetu.
Katiba ya Tz kaiandika Nyerere kwa maslahi ya chama chake , akalazimisha Afro Shirazi iungane naye huku aki force itumike katiba aliyoitunga yeye , Dictator
 
mwenye ufahamu anisaidie?
Katika lugha za mambo ya katiba,kama mnatumia vitabu zaidi ya kimoja kama katiba yenu basi hyo katiba inakuwa haijaandikwa,mkitumia kati a il I yo kwenye kitabu kimoja ndo tunasem imeandikwa.UINGEREZA WANA VITABU VUNGI AMBAVYO UKIVIWEKA PAMOJA NDO UNAPATA KATIBA YAO.KUNA MAGNA CARTA YA 1215AD ,KUNA PETITION OF RIGHTS YA 1629,KUNA SHERIA ZA BUNGE ,KUNA BILL OF RIGHTS NK .Tanzania katiba yetu I ko kwenye kitabu kimoja hivyo imeandikwa
 
mwenye ufahamu anisaidie?
Wanaosema hivyo ni waongo na wasioelewa chochote.

UK ina katiba ila katiba yake siyo document moja kama ilivyo kwa baadhi ya mataifa.

Mathalani katiba yetu ina vitu vyote kwenye document moja, wakati kwa UK, executive ina document yake, Parliament ina document inayojitegemea. Judiciary ina document inayojitegemea.

"The UK is often said to have an 'unwritten' constitution. This is not strictly correct. It is largely written, but in different documents."
 
SI KWELI.
Katiba wanayo, isipokuwa Katiba yao haijaandikwa (Unwritten Constitution),kama 'document' nayo ni aina ya Katiba; sisi ya kwetu Tanzania imeandikwa (Written Constitution). Katiba isiyoaandikwa ni kama vile mila, desturi na mambo yote yanayofanywa na kufuatwa na jamii fulani kwa kurithishana kizazi hata kizazi na hayapo katika maandishi. Ndivyo ilivyo hata katika mila za makabila yetu.
Rudia. Sikuwahi kujua hili jambo. Na sina uhskika kama ulichosema ni kweli....Nimeshangaa sana.
 
Ni kweli haina katiba isipokua inafata sheria kadhaa ikiwemo; Magna Carta, Bill of Rights na Human Rights Act ya mwaka1998.

Hupo sahihi. Inayo katiba ambayo ipo kwenye documents tofauti tofauti. Zote kwa pamoja ndiyo katiba ya UK.

"The UK is often said to have an 'unwritten' constitution. This is not strictly correct. It is largely written, but in different documents."

"In the UK a constitution has never been codified in this way; instead, the various statutes, conventions, judicial decisions and treaties which, taken together, govern how the UK is run are referred to collectively as the British Constitution".
 
Hizo zinaitwa Hati tu ila sio katiba mkuu
 
Sahihi, unwritten constitution means uncodified ipo kwenye vipande vipande tu vya sheria (statute) na maamuzi ya mahakama

Sio kwamba hakuna maandishi kabisa.

Kwanza kusema unwritted ni makosa. Uncodified ni sahihi, na kuwa uncodified haimanishi haijaandikwa bali documents mbalimbali hazijawekwa kwenye document moja.

Wanaosema haijaandikwa ni kwa sababubya kukosa maeneno sahihi kwenye kiswahili. Lakini kinachomaanishwa ni kuwa hakukuwahi kuwepo mchakato mmoja wa kuandaa katiba. Bali documents mbalimbali zilizoidhinishwa na kukubaliwa zimefanywa kuwa sehemu ya katiba.
 
Mkuu fungua KVant unywe ila uwe na zaidi ya miaka 18. NENO HAPA NI CODE (CODED/CODIFIED au UNCODED/UNCODIFIED)
 
Back
Top Bottom