Hili ni sahihi kweli kwamba England haina katiba

Hili ni sahihi kweli kwamba England haina katiba

KUHUSU KATIBA YA UINGEREZA (UK) NA SIYO ENGLAND:

KATIBA YA IMEANDIKWA KAMA KATIBA NYINGINE ILA IPO KWENYE VITABU TOFAUTI TOFAUTI

Katiba ni seti ya kanuni ambazo hutumika kuongoza nchi hupangwa na kwa kawaida huwa katika KITABU kimoja.

Hata hivyo nchini Uingereza katiba yao haijawahi kuwekwa kwenye KITABU kimoja na badala yake ipo kwenye Vitabu mbalimbali vinavyojumuisha sheria mbalimbali, mikataba mbalimbali, maamuzi mbalimbali ya mahakama na mikataba mbalimbali ambayo, ikichukuliwa kwa pamoja, inasimamia jinsi Uingereza inavyoendeshwa, kwa pamoja inaitwa KATIBA YA UINGEREZA ( UK)

Hivyo Uingereza wanayo Katiba iliyoandikwa kwenye vijitabu mbalimbali tofauti na huku Tanzania KATIBA yetu imeandikwa kwenye KITABU kimoja

The United Kingdom constitution is composed of the laws and rules that create the institutions of the state, regulate the relationships between those institutions, or regulate the relationship between the state and the individual. These laws and rules are not codified in a single, written document.
 
Ndio maana hua nacheka nikiona watu wanavyopiga makelele kuhusu katiba mpya wakati hata hii iliyopo hawawezi kukueleza inavyo waathiri.
Mkuu katiba ni zaidi ya ufahamu wa wananchi na pia katiba inabeba mustakabali wa taifa kwa vizazi vijavyo ambavyo hata havipo sasa. Mfano issues za rasilimali za nchi na mazingira.

Ndio maana mwanzo wa mchakato wa katiba wanahusishwa wataalam wa sheria ili kusaidia kuweka tamaduni, mila, taratibu na miiko ya jamii husika katika muktadha wa kisheria.

Ok, Kwa uchache, unaweza kuelezea kuelezea utakachokipata Kwa katiba mpya na unachokikosa Kwa katiba iliyopo?

Kwa ufupi katiba iliyopo inatekelezwa ipasavyo?
Kusema kuwa katiba ya sasa haitekelezwi sio conclusive evidence kuwa hatuhitaji mabadiliko ya katiba, inawezekana madhaifu ya katiba iliyopo ndiyo yanafanya katiba isitekelezwe na hakuna atakaye wajibishwa.

Utii, usimamizi, ulinzi na utekelezaji wa katiba unatafsiriwa na katiba husika.

Kwa kutambua kuwa masuala ya kisheria ni taaluma na si kila mtu anayamudu ndiyo maana hata mahakamani kuna uwakilishi unatumika kupitia wanasheria.
 
Mkuu katiba ni zaidi ya ufahamu wa wananchi na pia katiba inabeba mustakabali wa taifa kwa vizazi vijavyo ambavyo hata havipo sasa. Mfano issues za rasilimali za nchi na mazingira.

Ndio maana mwanzo wa mchakato wa katiba wanahusishwa wataalam wa sheria ili kusaidia kuweka tamaduni, mila, taratibu na miiko ya jamii husika katika muktadha wa kisheria.

Kusema kuwa katiba ya sasa haitekelezwi sio conclusive evidence kuwa hatuhitaji mabadiliko ya katiba, inawezekana madhaifu ya katiba iliyopo ndiyo yanafanya katiba isitekelezwe na hakuna atakaye wajibishwa.

Utii, usimamizi, ulinzi na utekelezaji wa katiba unatafsiriwa na katiba husika.

Kwa kutambua kuwa masuala ya kisheria ni taaluma na si kila mtu anayamudu ndiyo maana hata mahakamani kuna uwakilishi unatumika kupitia wanasheria.

Ahsante Kwa maelezo mazuri yaliyojitosheleza. Si kwamba sielewi umuhimu wa katiba Kwa mapana yake, hayo maswali yalitokana na majibu ya niliyemnukuu.
 
Ni kweli haina katiba isipokua inafata sheria kadhaa ikiwemo; Magna Carta, Bill of Rights na Human Rights Act ya mwaka1998.
Haya ndio maelezo sahihi kwa lugha nyepesi inayoeleweka hata na mkulima wa kijijini atayaelewa.

Maelezo yaliyotolewa mmoja wetu kuwa eti wanayo katiba lakini haikuandikwa si kweli. KATIBA HAWANA.
 
Sasa kama Rais (na viongozi wote walioapa kuilinda,kutenda kwa mujibu wa katiba) amesema katiba ni kijitabu tuu,kuna umuhimu gani wa hao asilimia 90 ya Watanzania kuisoma "hiko kijitabu"!!??
Hakuna.

Swali la kijinga.

Jibu la kijinga.
 
Hilo linawezekana kwenye jamii ya watu wastaarabu wanaoheshimu utu.
Kwahiyo ni Uingereza tu dunia nzima ndio wastaarabu? Maana nchi zengine zote duniani Zina katiba zilizoandikwa. Na kama utasema ndio, basi, juhudi kubwa ifanyike kwenye psychic yako kuondoa hiyo British colonial mentality.
 
Back
Top Bottom