Hili ni tunda au mboga au kitu gani jamani inaitwaje kwa kiswahili?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Tunguja.jpg

AU TUNGULE? KWA KIUNGUJA ZINAITWA TUNGUJA KWA KI BARA ZINAITWAJE YAKHE?
 
Leo wapendwa nataka niwafundishe kuhusu nyanya chungu, ndio enhe hizohizo naamini wengi kama sio wote mnazijuwa zipo za iana mbili zile chungu kabisa na za baridi (ambazo sio chungu) najuwa wengi sana hawapendi kula hizi nyanya chungu kwasababu hawazijui faida zake leo nitakwambia nisikilize kwa makini mwanamke na wewe mwanaume ukalibebe umpelekee mkeo anufaike nalo.

Nyanya chungu katika mwili wa mwanamke zinasaidia katika kuongeza maji ya ukeni enhe ndio utakuta mwanamke analalamika mimi mkavu mume wangu anachukuwa muda sana kuniandaa mwengine anasema nachubuka sina majimaji ya ukeni sasa bibie dawa ndio hiyo usikose nyanya chungu nyumbani kwako kama huziwezi chungu waachie wahaya wewe nunua zile za baridi hata kama huzipendi bibie ndio uzile mpaka uzipende, sio mbaya ukiungia kama mbili kwa kuanzia baadaye utaweza kula zidi..mimi nyumbani kwangu mwiko nyanya chungu kukosekana kwenye jokofu..haihusu bibi

Unaweza kuziungia kwenye vitu tofauti na zikanoga ngoja nikwambie jinsi mimi ninavyozitumia natia kwenye mlenda, kwenye dagaa, kwenye mboga ya nyama, kuku, natia mpaka kwenye pilau yani kila ninachopika nyumbani kwangu lazima ziwemo wanawake wote nyumbani kwangu nimewazoesha kuzila ila wanaume hawali kwanza kwasababu hawazipendi na pili kwavile haziwahusu labda kurekebisha afya tu siwalazimishi.

Umenisoma chukuwa hilo kama ulikuwa haujui..Cc.@georgeallen Mkuu Boflo
 
Last edited by a moderator:
Zina jina lake la asili ila kwa sisi tuliokulia mjini tumekuwa tunaziita NDULELE,
Matumizi yake na ikiwemo mizizi yake ambapo hutumika kwa mwanamke ambaye anaenda hedhi iliyopitiliza. Anapaswa kuchemsha mizizi yake na kunywa kutwa mara mbili kwa kipimo cha bilauri [dawa za asili huwa hazina masharti ya vipimo].

Tunda zake zinatumika sana kutibu funza wanaoingia vidoleni, unachopaswa kufanya ni kuitoboa ndulele na kuvisha kwenye kidole chenye mdudu kwa muda unaozidi dakika 10. Mdudu atakufa na kukauka kabisa.

Naamini hii ni tofauti sana na nyanya chungu. Hii ni chachu na ina kemikali nyingi sana.
 
Mkuu pia mizizi yake ni dawa ya meno yaliyooza na kutoa harufu.

unachemsha na kusukutua supu yake, pia waweza kuitafuna.
 
Hahahaha.
Yaani umenifurahisha sana baba watoto. Yaani umo kila sekta. Ngoja niandike proposal ya kupambana na funza, wakenya wanakula hela ya bure. Sapraizi ya ka-nissan navara inakuhusu.

Wifi AshaDii njoo umsome kakako.
Zina jina lake la asili ila kwa sisi tuliokulia mjini tumekuwa tunaziita NDULELE,
Matumizi yake na ikiwemo mizizi yake ambapo hutumika kwa mwanamke ambaye anaenda hedhi iliyopitiliza. Anapaswa kuchemsha mizizi yake na kunywa kutwa mara mbili kwa kipimo cha bilauri [dawa za asili huwa hazina masharti ya vipimo].

Tunda zake zinatumika sana kutibu funza wanaoingia vidoleni, unachopaswa kufanya ni kuitoboa ndulele na kuvisha kwenye kidole chenye mdudu kwa muda unaozidi dakika 10. Mdudu atakufa na kukauka kabisa.

Naamini hii ni tofauti sana na nyanya chungu. Hii ni chachu na ina kemikali nyingi sana.
 
Last edited by a moderator:
Kaka mkubwa hiyo ya funza umenikumbusha mbali sana, wakati huo twasoma ukiingiwa na funza lazima ukamatwe na kutafutiwa hizo ndulele.

Halafu pia kulikuwa na ugonjwa fulani sisi tulikuwa twauita "matuse"...mashavu sehemu za jaws huvimba na kuuma sana. Basi hizo ndulele zilikuwa zachomwa kama mshikaki halafu unakandwa nazo.
Baada ya siku kadhaa uvimbe hupotea na maisha kusonga.

Back
Top Bottom