Hili ni tunda au mboga au kitu gani jamani inaitwaje kwa kiswahili?

Hili ni tunda au mboga au kitu gani jamani inaitwaje kwa kiswahili?

Nimestuka kidogo...
Kuna rafiki yangu [Mtanzania] nimemuonesha hii picha akanithibitishia kwamba hizi ni ndulele na zinaliwa kwa baadhi ya watu. Nahisi amezifananisha na ngogwe [nyanya-chungu pori], Lakini akaniambia zinaliwa, ngoja nitajaribu kidogo kuonja kama zinafaa kisha ntakuja kuwaambia hapa siku moja.

Alinielekeza kwamba zikichanganywa na bamia zinakuwa makini kweli. Mh, maisha ni mwendo mrefu kweli.


Rafiki mwingine [Visiwani] anasema kuwa hii inatumika kutoa mimba. Sasa hapo sijafahamu. ila naamini kuwa wajuvi humu wanaweza kututhibitishia hayo kama kweli au la

Oh maama... RIP Paw in advance.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: Paw
MziziMkavu unachanganya picha ya ndulele na nyanya chungu,
lakini unachotaka kusema umeeleweka,
 
Last edited by a moderator:
Mhmmm!!! Leo unanikana mpendwa jamani wakati tulikuwa tunajificha wote kwenye lile jumba bovu halafu wewe ulikuwa mama na mimi ndo baba. Hata Anorld mpiga chabo anakumbuka.
Hahahahaha acha hizo bwana
 
Kwetu zinaitwa TURA, haziliwi bali mizizi yake ni tiba ya matatizo mengi, na zenyewe pia hutumika kupekecha zongo, wakina mama wafanyabiashara ndogondogo utakuta pia huziweka kwenye biashara zao kujikinga na ulozi, kwa wale wanaoamini.
kweli wazigua kiboko...
 
Maisha bila utafiti ni sawa na kufumba macho wakati unakatiza busy road ya magari.
Nilikuwa sokoni this weekend kwa shopping. Nilifanya udadisi kutaka kujua kama ndulele ni kweli zaliwa. Nilichoambulia kwa watu wawili watatu ni kwamba YES zinaliwa. Ila ni zile ambazo ni cnaha yaani ambazo hazijakomaa tena zikiwa bado ndogo. Zikishakomaa hazifai. Mapishi yake hayatofautiani na ngogwe

Naamini kuwa zinaweza kuliwa, ntaendelea kutafiti hadi nijithibitishie kwa vitendo
 
sijajua unazungumzia tunda gani,labda ungeweka picha yake,mimi nayajua matunda yote kwa kiswahili.au unazungumzia ndula?
Nalog off
 
Kaka mkubwa hiyo ya funza umenikumbusha mbali sana, wakati huo twasoma ukiingiwa na funza lazima ukamatwe na kutafutiwa hizo ndulele.

Halafu pia kulikuwa na ugonjwa fulani sisi tulikuwa twauita "matuse"...mashavu sehemu za jaws huvimba na kuuma sana. Basi hizo ndulele zilikuwa zachomwa kama mshikaki halafu unakandwa nazo.
Baada ya siku kadhaa uvimbe hupotea na maisha kusonga.
dah huu ugonjwa wa kuvimba mashavu umenikumbusha mbali sana

huu ugonjwa ulipokuwa unatukamata tulikuwa tunapaka mashavuni ile rangi ya blue tuliyokuwa tunaweka kwenye mashati ya shule

dah zama hizo miaka ya 2000 mwanzoni huu ugonjwa siku hizi haupo
 
Back
Top Bottom