Hili ni tunda au mboga au kitu gani jamani inaitwaje kwa kiswahili?

Hili ni tunda au mboga au kitu gani jamani inaitwaje kwa kiswahili?

Tunaita sodum apple au kwa jina la kisayansi ni solenum incanum ni tunda lisilo liwa na wanyama wengi ingawa kuna wengine wanakula kama vile sungura na Tandara.

Naomba uniruhusu nifanye correction kwenye post yako! S/Name should be in Latin, so inapaswa kuwa Solanum incunum Hope kama na wewe ni mwanasayansi mwenzangu hutakwazika.
 
Hizo ni ndulele ...udogoni sie hizo zilikuwa na kazi mbili kuu...tulikuwa tunawadungua nazo wakorofi na pia tulikuwa tunazisugua chini kwa kutumia miguu tukiona mtu mwenye kipara!!!!utashangaa na hadi leo sijui connection iliyokuwepo kwani walikuwa wanakuna vipara vyao ile mbaya...kuna mzee mmoja aliwahi kudondoka kwenye pikipiki kwa kuwasha tulipokuwa tunasugua ndulele!!!
 
Mhhhh! sasa zikiingia kwenye nyeti hazina madhara kweli ya kusababisha nyeti kuathirika kwa namna moja au nyingine!?


Ndulele...huwa haziliwi ila maji yake yanatumika kurefusha mashavu ya uke na kicmi! Unazibabua kidogo kwenye moto unakamua yale maji yake unapaka kwenye sehemu husika unavuta kidogo x2. 🙂
 
Sidhani kama hili tunda ndulele linaliwa na binadamu kwani toka nilipokuwa mtoto nilisikia kuwa lina sumu pia ni dawa asilia hivyo tulikuwa tunachumaga na kuwapiga watoto wenzetu mitaani kabla ya kurudi nyumbani kupata kipigo kwa mama (kwa ajili ya utundu). Kuna baadhi ya watu walisemaga ndulele linaongeza mapumbu urefu na mboo kuwa kubwa kama ukichanjia na kusemea. Tulijaribu enzi zile za utotoni lakini sijuwi kama zilifanya kazi kweli au nimejaliwa tu umbile langu, sina uhakika.
 
Kaka mkubwa hiyo ya funza umenikumbusha mbali sana, wakati huo twasoma ukiingiwa na funza lazima ukamatwe na kutafutiwa hizo ndulele.

Halafu pia kulikuwa na ugonjwa fulani sisi tulikuwa twauita "matuse"...mashavu sehemu za jaws huvimba na kuuma sana. Basi hizo ndulele zilikuwa zachomwa kama mshikaki halafu unakandwa nazo.
Baada ya siku kadhaa uvimbe hupotea na maisha kusonga.

long tym sana duu kitu cha ndulele ni noma..
 
ila kuna tofauti kati ya nyanya chungu na ndulele,ndulele hailiwi halafu mziki wake yale maji yaguse macho,ila nyanya chungu(ngogwe) inatumika kama viungo vya msosi
Yap yap...zile zitakula ndulele bana
 
Ndulele...huwa haziliwi ila maji yake yanatumika kurefusha mashavu ya uke na kicmi! Unazibabua kidogo kwenye moto unakamua yale maji yake unapaka kwenye sehemu husika unavuta kidogo x2.
Mkuu bombah987 Unasema ukweli lakini? Maneno yako?
 
Last edited by a moderator:
Dah zimenikumbusha mbali, kidogo, kipindikile Benjamin Mkapa high school palikuwa dampo, basi kuzunguka hapo ziliota kwa wingi sana. Zina matumizi mengi sana. Nakumbuka Ligi Daraja la tatu ilikuwa sana Karume na kuna mda mechi zinapigwa kwenye viwanja hivyo, basi hizi Ndulele ama Tura zilitumika kishirikina kuloga Mechi, utaona mchezaji anaenda kwenye Goli na kuzipiga kuelekea Nyavuni.
Pia ukisikia Tumbo linakata na hakuna daktari ww chukua mizizi ya hiyo kitu tafuna.


Mimi nilikuwa napenda kutumia kupiga kwakuwa haziiumizi sana hasa zikiwa zimeiva na kuwa za Njano.
 
Nimestuka kidogo...
Kuna rafiki yangu [Mtanzania] nimemuonesha hii picha akanithibitishia kwamba hizi ni ndulele na zinaliwa kwa baadhi ya watu. Nahisi amezifananisha na ngogwe [nyanya-chungu pori], Lakini akaniambia zinaliwa, ngoja nitajaribu kidogo kuonja kama zinafaa kisha ntakuja kuwaambia hapa siku moja.

Alinielekeza kwamba zikichanganywa na bamia zinakuwa makini kweli. Mh, maisha ni mwendo mrefu kweli.


Rafiki mwingine [Visiwani] anasema kuwa hii inatumika kutoa mimba. Sasa hapo sijafahamu. ila naamini kuwa wajuvi humu wanaweza kututhibitishia hayo kama kweli au la
 
Zina jina lake la asili ila kwa sisi tuliokulia mjini tumekuwa tunaziita NDULELE,
Matumizi yake na ikiwemo mizizi yake ambapo hutumika kwa mwanamke ambaye anaenda hedhi iliyopitiliza. Anapaswa kuchemsha mizizi yake na kunywa kutwa mara mbili kwa kipimo cha bilauri [dawa za asili huwa hazina masharti ya vipimo].

Tunda zake zinatumika sana kutibu funza wanaoingia vidoleni, unachopaswa kufanya ni kuitoboa ndulele na kuvisha kwenye kidole chenye mdudu kwa muda unaozidi dakika 10. Mdudu atakufa na kukauka kabisa.

Naamini hii ni tofauti sana na nyanya chungu. Hii ni chachu na ina kemikali nyingi sana.

Haya, kwenye red watani zangu wanahusika, Kakobe, Maha, Muhehe, Luyagaza, Rungu, Bitomazi, Bonabucha, Kaseja na waliwa funza wengine dawa hiyooo, Mungu awape nini?

Hizo zinaitwa TUNGUJA MWITU na ni sumu. Wazaramo wasije kusolve matatizo ya nyanya chungu za kuungia nguru
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Hahahahahah....hamna bwana nlikua nachezea mdako!

Mhmmm!!! Leo unanikana mpendwa jamani wakati tulikuwa tunajificha wote kwenye lile jumba bovu halafu wewe ulikuwa mama na mimi ndo baba. Hata Anorld mpiga chabo anakumbuka.
 
Back
Top Bottom