Salaam, shalom!!
Lengo la mada hii ni kuwasaidia wote waombao Kwa Mungu ulinzi wa kimwili na kiroho.
Lengo lingine pia ni kuwaondoa HOFU wale waombao Kwa mashaka, ulinzi atoao Mungu Kwa mwanadamu ni mkubwa kuliko ulinzi apewao Mfalme wa tawala za WANADAMU.
Turudi kwenye mada.
( 1 Mambo 21:1-17).
Shetani anaingia kwenye mawazo ya mfalme Daudi, ghafula akapata wazo la kuwahesabu Wana wa Israeli,
Ni sawa tu na Askofu au Mchungaji Leo apate wazo la kuwahesabu walokole, Wana wa Mungu,waliopigwa chapa nyusoni mwao, Hilo wazo litakuwa ni la Mwovu, Waliookoka hesabu Yao ni Siri, imefichwa, shetani angependa kuijua hesabu ya walokole Ili ajue silaha za kuwashambulia, lakini uwezo huo Hana.
Basi Mfalme Daudi akidhani Yale ni mawazo yake kuwahesabu Wana wa Israel, akaitisha sensa, wakahesabiwa baadhi lakini Si wote, alifichwa pia.
Hasira ya Mungu ikawaka juu ya mfalme na juu ya nchi Kwa kosa la mfalme Daudi. Malaika akatumwa awaue Wana wa Israel maelfu Kwa maelfu,
SIZE YA UMBO LA MALAIKA KATIKA MACHO YA NYAMA.
Daudi akamwona Malaika urefu wake ulikuwa wa kuogofya, Malaika alikuwa ameshika upanga na kuuelekezea mji mkuu Jerusalem.
Miguu ya Malaika huyo ilisimama ardhini na urefu wake ulifika Mbinguni.
Daudi kuona hivyo, akasalimu amri, akaomba Toba, akasamehewa na kipigo kilipungua, walikufa wananchi wengi sana Kwa kosa la mfalme wao Daudi.
FUNZO.
1. Tuchaguapo viongozi wa Nchi, tuwaombee na kuombea washauri wao maana shetani anao uwezo wa kupitisha mawazo yake vichwani mwa WAFALME bila kujua hayo ni mawazo ya kishetani.
2. Nchi na wananchi wasio na hatia, wanaweza kufa au kuadhibiwa na Mungu Kwa makosa ya mfalme au kiongozi wao. Njaa inaweza kuikumba Nchi Kwa makosa ya viongozi,nk nk.
3. Uombapo uwe na uhakika na Imani juu ya ulinzi atoao Mungu, Malaika .Moja anaweza kuangamiza mji mzima Kwa sekunde, sasa ashindwe vipi kukulinda na wanga mtaani mwako wasikisumbue?
Ikiwa huna HAKI ya kupata ulinzi wa Mungu kupitia Malaika wake, fuatisha Sala hii:
EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, ULEVI USINISHINDE, UZINZI USINISHINDE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. AMEN
Karibuni 🙏