Hili punguzo la wafanyakazi wa idara ya ulinzi kampuni hii linakubalika ?

Hili punguzo la wafanyakazi wa idara ya ulinzi kampuni hii linakubalika ?

Wamweru

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2015
Posts
635
Reaction score
485
Hi
Poleni na majukumu ya kila siku, rejea kichwa Cha habari hapo juu kampuni ya uchimbaji wa madini ya MMG gold iliyopo Seka Musoma inafanya mchakato wa kupunguza wafanyakazi kwa mtindo ambao naomba wajuvi waje kutoa ushauri kama njia hii INAKUBALIKA?

Tarehe 29/05/2025 waliwafukuza wafanyakazi wa idara ya ulinzi na kuleta kampuni ya SumaJKT na tarehe 30/05/2025 kampuni ya SumaJKT wakaanza kazi,waliokuwa walinzi wa kampuni wakagoma kuondoka mgodini,tarehe hiyo hiyo ya 30/05/2025 wakatoa tangazo la punguzo la wafanyakazi idara ya ulinzi kikao hicho kinafanyika mida hii.

Je, hiyo imekaaje kwani majadiliano yanafanyika wakati tayari wafanyakazi wa idara ya ulinzi ya mgodi imeshavunjwa na kufukuzwa? na wakati huo huo kunywa wafanyakazi wako Rotational leave wao hawana taarifa ya kinachoendelea nao wamepunguzwa.

Ushauri naambatanisha na tangazo la kusudio la kupunguzwa wafanyakazi.

1000036512.jpg
 
Zimezingatiwa kivipi hapo ndugu y

Haki za wafanyakazi zimezingatiwa, hakuna tatizo. Kampuni inafanya biashara, lazima iendeshwe kibiashara.
Kwa uchache najua haya kuhusu rudundancy operatios.
Suala la kutaka kupinguza wafanya kazi(redundany) ni lazima afanye haya:
1) kumpa notisi muajiriwa huyo ya kumjulisha kuhusu kuondolewa kazini
2) kumpa sababu za msingi kwanini anamuondoa kazini
3)kumpa nafasi ya kujiandaa kutafuta ajira nyingine kwa kumpa mda maalum na wakutosha.
4) na kuzingatia mkataba unasema nini juu ya matokeo ya kufanya redundancy.
Hivyo ikumbukwe kuwa muajiri akishindwa kufuata utaratibu wa kumuondoa kazini muajiriwa mahakama au bodi yoyote inayohusika na kusuluhisha migogoro ya wafanyakazi inaweza kumuamuru musjiri haya:
1)kumrudisha kaxini muajiriwa na kumlipa fidia ya pesa ya mshahara wa miezi 12,au kumlipa malipo yote aliostahiki kulipwa kwa kuhesabu tangu siku anafukuzwa mpaka amri inatolewa na mahakama/bodi.
2)kumlipa tu fidia ya mshahara wa miezi 12.
Kumlipa fidia ya mshahara wa miezi 12 na kubadilisha vipengele vya mkataba.
 
Rejea kwenye mkataba wako wa kazi, iwapo upande mmoja anavunja makubaliano/mkataba ni nini kifanyike.

Hilo tangazo, nimeona kipengele f kinajaribu kuwafikiria kuhusu stahiki.​
 
Mambo yanaweza kua magumu kwa hao walinzi kama walifanya kazi bila mkataba, maana kampuni nyingi za ulinzi zina ajiri kitapeli sana bila kuwapa watu mikataba ya kueleweka
 
Kampuni kufanya retrechment cyo jambo geni hata pale Bulyanhulu Gold Mine mwaka 2017 kilifanyika kitu kama hicho lkn issue iko kwenye Je kampuni inaachanaje na Mwajiriwa wake!!!!!.Barrick by then ACACIA waliachana vizuri mno na waliokuwa wafanyakazi wake kipindi cha zahama yao na RAIS WA KIPINDI HICHO, kila mtu alipewa kilichomstahili na kuweza kuendelea na maisha mengine nje ya ACACIA.Chama cha wafanyakazi pamoja Serikali wakae na kampuni waangali namna bora ya mwekezaji kuachana na wafanyakazi wake.
Kwenye biashara kuna mengi, kuna kuona wafanyakazi wako wamezeeka au wamechoka kiasi kwamba hawawezi tena kumudu majukumu yao, hapo retrechment haikwepeki.
 
Mambo yanaweza kua magumu kwa hao walinzi kama walifanya kazi bila mkataba, maana kampuni nyingi za ulinzi zina ajiri kitapeli sana bila kuwapa watu mikataba ya kueleweka
Mkataba upo mkubwa maana wameajiriwa na mgodi kama wafanyakazi wa mgodi idara ya ulinzi
 
Kampuni kufanya retrechment cyo jambo geni hata pale Bulyanhulu Gold Mine mwaka 2017 kilifanyika kitu kama hicho lkn issue iko kwenye Je kampuni inaachanaje na Mwajiriwa wake!!!!!.Barrick by then ACACIA waliachana vizuri mno na waliokuwa wafanyakazi wake kipindi cha zahama yao na RAIS WA KIPINDI HICHO, kila mtu alipewa kilichomstahili na kuweza kuendelea na maisha mengine nje ya ACACIA.Chama cha wafanyakazi pamoja Serikali wakae na kampuni waangali namna bora ya mwekezaji kuachana na wafanyakazi wake.
Kwenye biashara kuna mengi, kuna kuona wafanyakazi wako wamezeeka au wamechoka kiasi kwamba hawawezi tena kumudu majukumu yao, hapo retrechment haikwepeki.
Uko sawa mkubwa
 
Rejea kwenye mkataba wako wa kazi, iwapo upande mmoja anavunja makubaliano/mkataba ni nini kifanyike.

Hilo tangazo, nimeona kipengele f kinajaribu kuwafikiria kuhusu stahiki.​
Mkataba unasema
" In the course of the contract period,this contract may be terminated by either party giving 30 (Thirty) days written notice.
 
Kama huna mkataba wa kazi unaondoka kama ulivyokuja, yani ukitoka kazini wewe ni mzururaji, ukiwa kazini mfanyakazi.
 
Back
Top Bottom