Hili suala la wastaafu kupeana Mahekalu, Mwalimu alisema ipo siku Watanzania watalidai Azimio la Arusha

Huyo shujaa wako ndiye aliyewajengea mahekalu. Samia kafanya kukabidhi tu maana wakati Mwinyi anakabidhiwa na shujaa wako, hekalu la Kikwete lilikuwa halijaisha. Muasisi wa mahekali ni shujaa mwendazake.
 
1. Wanapeana mishahara mikubwa kuliko wafanyakazi wengine,

2. Pamoja na ukubwa wa mishahara yao, hawalipi kodi,

3. Licha ya ukubwa huo wa mishahara, wamewekeana posho kibao za mafuta ya gari, gari, nyumba, bima za afya daraja la kwanza zisizotokana na makato ya mishahara yao.

4. Wanapeana pension ambazo siyo makato ya mishahara yao. Yaani pension la kujichotea tu kutoka hazina

5. Wakitoka madarakani wanapeana majumba, magari na kuwarithisisha watoto wao vyeo.

Sisi hata viajira vya Laki 5 kwa mwezi, Magu aliona kama watu watafaidi sana.

Kinachofanyika, masikini baba, mama, mtoto, mjomba, shangazi mkisikia Mwanasiasa anapita hudhurieni kwenye mikutano yao,

Msisahau kuwaimbia na kuwatukuza,

..........baba babaaaaa baba huyo 🎶🎶🎶

Mkiwa mnaimba hakikisheni mnaruka ruka juu.
 
Kiufupi tulipaswa kupata kiongozi atakayekwenda kukata marupurupu na mishahara ya kinyonyaji hapa nchini, kwenye mihimili yote Sio bunge, mahakama au serikali.Kwa mfano Sheria inayoruhusu majaji kutolipa Kodi ifutwe wakiwemo na wabunge
 
Huyo shujaa wako ndiye aliyewajengea mahekalu. Samia kafanya kukabidhi tu maana wakati Mwinyi anakabidhiwa na shujaa wako, hekalu la Kikwete lilikuwa halijaisha. Muasisi wa mahekali ni shujaa mwendazake.
..yaani bado hatujapata kiongozi mtetezi wa kweli wa rasilimali za nchi zaidi ya watumbuaji tu
 
Nakubaliana na wewe ila nadhani wapo wenye misimamo thabiti. Si unajua msafara wa mamba kenge nao wapo. Mikenge ndiyo hiyo inajitoa. Tuone na wao wapinzani watafanya vipi. Tukiwapiga chini fisiemu na kuwapa hawa upinzani plus katiba mpya nzuri itakayowabana viongozi. Wakifanya mchezo tunawapiga chin na wao.
 
Ila huyo Mwalimu unaemtolea mfano nae alijengewa hekalu baada ya kustaafu
 
Una akili timamu?
 
Ila huyo Mwalimu unaemtolea mfano nae alijengewa hekalu baada ya kustaafu
Mwalimu hakujilimbikizia mali na alikuwa na nyumba ya kawaida sana sana. Alikataa walipotaka kumjengea nyumba. Jeshi lilijenga kimya kimya na kumlazimisha aipokee. Na unajua wanajeshi wanajenga kwa jasho lao. Hapo gharama zilikuwa materials tu. Pia pensheni ya mwalimu ilikuwa ndogo sana na mshahara wake alipokuwa raisi. Baada ya kustaafu aliishi maisha ya kawaida sana. Alikuwa analima yeye mwenyewe kwa jembe la mkono. Huyu angalau alikuwa na uchungu na rasilimali za taifa hili pamoja na mapungufu yake.
 
Binafsi nafikiri itafika tu siku vyote Hv watarejesha. Si sawa MTU analipwa salary bora kabisa HD kufa, na marupurupu tele, bado ndiye abayepewa upendeleo wa mema yote. Naamini ingetakiwa MTU afe ili wao waishi yaani tusingekikuwepo. Mfumo wetu sio mzuri
 
Ila huyo Mwalimu unaemtolea mfano nae alijengewa hekalu baada ya kustaafu
Tofautisha kujengewa kama hisani na kujengewa eti ni stahiki yako wakati una mijumba kedekede.

Mwalimu hakuacha sheria ya wastaafu kupeana mabenzi, mahekalu, mshahara 80% ya mshahara wa rais aliyeko madarakani. Hiyo sheria ilitungwa wakati wa BWM ambapo Kikwete na Magufuli walikuwa sehemu ya serikali, na walipokuja kuwa maraisi wakaendelea nayo hiyo sheria, hawakuifuta!

Nyerere alijengewa na Jeshi, Sasa mambo ya Jeshi ni ya jeshi wale wana sheria zao tofauti na ufanyaji mambo tofauti na huku uraiani.
 
Npo gizani
 
Yaani kwa kweli inafurahisha.......... Viongozi (ambao walikuwa watumishi wa Uma) wanapata;
Nyumba za Bure
Usafiri wa Bure
Ulinzi wa Bure
Matibabu Bure
Pension e.t.c

Wastaafu (ambao nao pia walikuwa watumishi wa Uma)
Pension wanapata kwa kuhangaishwa na mpaka wahakikiwe
Matibabu ndio wawekwe kwenye Bima za watoto wao ambao wana Bima ????

waturuhusu tu kuwe na ugombea binafsi (Wote tunatamani kuwa viongozi aisee)
 
Mkuu watumishi wa umma wakishastaafu wakipata hata hicho kiunua mgongo japo kidogo wamshukuru mungu, ulitaka kuona usumbufu wa mifuko ya hifadhi ya jamii staafu, Mara utaambiwa lete barua yako ya kwanza ya ajira, Mara leta mkataba wa ajira, Ni full usumbufu.Wako wastaafu Wana zaidi ya miaka miwili hawajawahi pata kiunua mgongo Chao kamwe.
 
hapo kwenye shujaaa umekosea sababu hiyo nyumba amejengewa na huyo huyo anaeitwa shujaaa sijui shujaaa wa nn,wote ni wanyonyaji tu.
 
Na ndio wengi wenye maisha ya shida na wala rushwa hayo maaskari yanayolinda majizi yanayogawana nchi
Hii thread natamani viongozi wetu na wakuu wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama wakiwemo na maaskar wetu wote waje wapitie hapa kuna kitu watajifunza maana wametufanya kama watumwa kweny nchi yetu wanasahau kabisaa kama sisi ndo wenye nchi yetu na ndo tuko wengi wao niwachane mno sisi raia ndo wengi kuliko wao kwa iyo wawe makini kuna siku hayo majeshi yao, vifaru,na bunduki hazitafanya kazi kuwalinda wala kuwaokoa ikiwa wenye nchi tukiamua kwa umoja wetu.. maana wamekosa hata huruma na utu kwa wananchi bila kujali umaskini tulionao,

fikiria ni wizi kiasi gani na kujirimbikizia mali wanafanya na wengi wao hawafanywi chochote hata makamani hawapelekwi zaidi ya kulindana na kumahishana na kubadilishana vituo vya kazi mfano kama ameharibu kigoma anapelekwa singida au mwanza nk na maisha yanendelea

kuna viongozi wazazi wao wote baba na mama walikuwa viongozi tena wakubwa nchi hii wao pia ni viongozi na wnafabya chini juu na watoto wao pia wawe viongozi nao pia wanafanya kila liwezekalo na wanao pia watakuwa Viongozi sasa unaziuliza hii kamba ya kuwekana, kuteuana wao kwa wao sisi wengine ambao hatuna ndugu walioko juu tunakosa ajira na kazi kisa hatuna wa kutupendelea wala kutusaidia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…