Semeni ukweli - wakale usema "msema ukweli ni mpenzi wa Mungu" mkuu ni hivi: Merikani wala haikuhusika chochote katika usambaratikaji wa Soviet Union, sijui kwa nini media za magharibi upendelea sana kueneza taarifa za uongo na za kubuni tu, watu wengi Duniani wali amini sana uzushi huu.
Ukweli ni kwamba Russian Federation na former Soviet Republics walikaa chini wakakubaliana kutengana kila republic ijitawale yenyewe washirikiane tu kwa mambo ya biashara nk, hapakuwepo shinikizo lolote kutoka Merikani wala nini sijui.
Wanzilishi wa kusitisha vita baridi ni Wamerikani yenyewe sio Urusi - mkewe Rais Reagan, Mrs Nancy Reagan ndiye alimshauri mumewe kwamba ajaribu kumpigia simu Gorbachev amshurutishe kwamba wasaidizi wao wakutane na kufanya taratibu za wao kukutana na kumaliza tofauti zao, hasa hasa usitishaji wa vita baridi (cold war) najua watu wengi watanipinga kwamba iweje mke wa Rais awe na uwezo wa kuwa mwanzilishi wa yote haya, kwani alikuwa na cheo gani Serikalini - ukweli wa mambo ni kwamba she did it na kufanikiwa by 100%!!
Watu wengi wanao fahamu kwa karibu familia ya Reagan usema ingawa Nancy alikuwa mdogo kwa umbo na mfupi, lakini alikuwa na akili nyingi na hekima sana na Reagan mwenyewe alikuwa anasikiliza sana ushauri wa Nancy na kuuchukulia seriously, huo ndio ulikuwa ndio mwanzo wa kusitisha vita baridi mwanzilishi kama nilivyo sema tangu mwanzo kwamba wanzilishi wakikuwa ni Wamerikani wenyewe na wala si Warusi - kwa bahati mbaya au kimakusudi vyombo vya habari vya magharibi ueneza habari tofauti kabisa na za Uongo, eti: Urusi ilishindwa vita baridi baada ya kishindwa kumudu gharama za ushindani wa uundaji wa silaha za kijeshi baina yake na Merikani - waongo wakubwa sana hawa, uzuri ni kwamba wenye kufuatia kwa karibu kuhusu ukweli kwa kile kilicho tokea wanajua ukweli huko wapi na sio western inept propaganda 24X7, hata uwezi kujua deep down wanakuwaga na malengo gani kwa kueneza taarifa za kutunga tu na kushinikiza Dunia kiaina ili ikubaliane na uongo wao.