Hirizi ni mzigo mzito sana

Hirizi ni mzigo mzito sana

Hata mimi nikivaa hirizi ni imani yangu, tena sio kiunoni kwa siri, ni shingoni lionekane wazi. Tasibihi ivaliwe bila woga ila hirizi ivaliwe kwa woga!! Imekaaje?
 
Uko sahihi kabisa na wala hakuna wa kukupinga kama haikusaidii wewe, huyu na yule unavaa ya nini?? angalia kwanza;Kamwe mtu huwezi kumeza chloroquine au kuchomwa sindano kama huumwi ugonjwa unao husiana na sindano hiyo...
Ila uchawi ni sayansi kali sana,imagine mtu anakaa kwenye ungo,anachanganyachanganya mizizi halafu anapaa ndani ya muda mfupi yuko Dar tayari tokea kigoma hii hatari sana
 
Nilipewa Azima nitembee nayo dah Siku moja tu nikaanza kuichoka. Kiufupi ni upuuzi ambao una mwisho wake bora kumtegemea Mungu upo free una enjoy ila ayo mambo ya hirizi kazi kweli kweli
 
Nilipewa Azima nitembee nayo dah Siku moja tu nikaanza kuichoka. Kiufupi ni upuuzi ambao una mwisho wake bora kumtegemea Mungu upo free una enjoy ila ayo mambo ya hirizi kazi kweli kweli
Hukua na matatizo pengine ila sisi wenye matatizo hatuchoki kufuata masharti ya azma
 
Hata mimi nikivaa hirizi ni imani yangu, tena sio kiunoni kwa siri, ni shingoni lionekane wazi. Tasibihi ivaliwe bila woga ila hirizi ivaliwe kwa woga!! Imekaaje?
,[emoji3]ya giza si ya nuruni.. Hubaki kifichoni
 
TITO 3 : 9

Lakini maswali ya upuzi ujiepushe nayo, na nasaba, na magomvi, na mashindano ya sheria. Kwa kuwa hayana faida, tena hayana maana.
TITO ni yesu wako huyo!! uko sahihi, hanihusu wala hanitishi!!!

Isipokuwa ukicheza neno la Yesu wangu, na kuniletea huyo wako lazima ugombane na mimi! tena waziwazi, ungekuwa hapa karibu nakutia vitasa kabisa ukamsimulie vizuri!! wala sikuhurumii!! sijakosea narudia Yesu wangu ni jibu, anaweza!!
 
Ila uchawi ni sayansi kali sana,imagine mtu anakaa kwenye ungo,anachanganyachanganya mizizi halafu anapaa ndani ya muda mfupi yuko Dar tayari tokea kigoma hii hatari sana
Kabisa mkuu sijui kwa nini waafrica waliikataa!!! wakakubaliana na Mzungu wakachanganya na yesu fake mpaka leo watu wanamzimia na wanaenda Vatican kuhiji!!
 
Sikumbuki kama niliwahi kubebeshwa huo mzigo na wala sidhani kama siku moja nitakuja kuubeba kwa ridhaa yangu mwenyewe, ingawaje wakati mmoja nilishawahi kuchanjwa kwa wembe nikiaminishwa kuwa ni kinga dhidi ya Wachawi/wanga.
Wadogo tuliburuzwa sana. mgonjwa mama lakini tiba mnajumuishwa. Nilikimbia chale kwa bibi nikadakwa katika shamba la mahindi mbali kabisa, nikala chale za kutosha nikapakwa dawa inauma hatari. nashukuri zile alama zilifutika baadaye. Loh!
 
Hukua na matatizo pengine ila sisi wenye matatizo hatuchoki kufuata masharti ya azma
Kuna mtu alifika kijijini kwetu akaiba akakamatwa akapigwa sana kufa hafi, mawe fimbo wapi. Hadi mwenyewe akaomba poo kwa kusema 'jamani naumia kuna hirizi mkononi karibu ya bega ikateni nateseka" ilivyotolewa fasta aka RIP.
 
Duh[emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064]
 
Kuna jamaa yangu mmoja yeye azma yake aliambiwa isiingie povu na ilikuwa na uwezo wakumfanya apendwe na kila mtu yaani mwarabu,, mzungu, mwafrika na hata mchina pia aliambiwa itamsaidia ktk masuala business.

Kama ilivyo ada vitu vya kishirikina vinakikomo siku moja alijisahau akafuria yaani alijisahau na ilikuwa kwenye mfuko wa suruali na akaanika then akaenda kupata breakfast ile anarudi akakuta nyumba aliyopanga inawaka moto na ilianza upande wa chumba chake.

Basi mali zake zote ziliteketea alipojaribu kurudi kwa yule mganga akakuta hayupo yaani kaenda jail ikawa ndiyo mwisho wa maagano ya hirizi.

Blaza Mshana Jr siyo kama tunapenda kuingia huko kwenye maagano ya mahirizi( azma) hapana ila ni manyanyaso yaliyojaa hapa ulimwenguni na dhiki zetu hizi ndiyo maana tunaamua kwenda upande wa pili walau tuweke heshima kwa ndg na jamaa nalogi off.

Let no one make you regret kuingia upande wa pili, umaskin unanuka sana
 
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]Babu mshana hapa umenifurahisha na kunichekesha pia yaani kaka katika vitu ambavyo sijawahi kuvielewa basi hiki ni kimojawapo.

Yaani binadamu sisi sijui hata unaanzaje kuamini kitu km hirizi. Ni afadhali hata wale wanaochanja kuliko KUVAA mahirizi. Halafu naskia Kuna mahirizi mengine huwaga yanapumua hii nayo imekaaje mzee baba?!

Usikute we ndo mtumiaj mzur umeyajaza kwako
 
Hukua na matatizo pengine ila sisi wenye matatizo hatuchoki kufuata masharti ya azma
Mi nilikosea jambo moja mi nilimtegemea mungu japo nilikuwa nakula shaba zingine zinapita zingingine zinanipata na hii nikwasababu ya kupuzia mambo ya ibada sometimes ukienda kazini ofisini unakuta mavi ya paka. Kosa nilofanya nikwenda kwa mganga bwana bwana bwana kumbe kama nimewapa connection ya kushindana aise nilikuwa napokea makombora mazito mazito

Dakika ya mwisho usiku lilipigwa kombora usingizini dah siwezi kusahau ndugu zangu wachawi wabaya sana ilikuwa ivi azma niliweka pembeni bwana mvua ilipiga ya hatari radi kama zote kkujicheki azma sina hali nilokuwa nayo haielezeki nikajitahidi nikavuta azma karibu ilikuwa pembeni ndiyo nikapata awheni.

Kesho nikapaki mabegi nikaandika barua ya kuacha kazi uyo safari nisije nikafa bure au kuwa chizi vita ilinizidi. Nilijaribugi ile ya chumvi ya mshana nimeenda nayo badae wakaja wakapindia we mtu kila siku unamwaga chumvu ndani ila dah Ukingia mtaani kama Hujajipanga vyema aidha kwa mungu au kwa shetani basi utateseka sana.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom