Watu wanaosema 850 ni kubwa ni kufananisha na makampuni mengine ya simu Africa/nchi zinazoendelea, sio kwamba wameona tu 850 ni kubwa unavyofikiri.
Vodacom IPO share price highly valued: experts
Kwa kuangalia dividends wanayotarajia kutoa Voda kwa share ni 20-50 shillings hii ni 2%-6% ya 850!
Kwenye fixed deposit benki unaweza kupata 8%-10+% tena kwenye fixed deposit hakuna risk ya mtaji wako kupotea unless benki ifilisike value ya shares inaweza kushuka siku yoyote, kwa hiyo dividend investing haimake sense kwa soko la Tanzania, inamake sense nchi kama marekani ambapo fixed deposit unapata kama 1% returns.
So tumebakia na capital gains, hapa swali ni je growth ya Vodacom itatoka wapi? Teyari ni namba moja TZ na market share yao inashrink kila siku, Tigo wako only 2% nyuma yao, Halotel anakamata share na yeye, so tujiulize growth ya Voda itatoka wapi?
Kama hii IPO iko undersubscribed namna hii, kuna habari za kuaminika kuwa wameuza maybe 1/3-1/2 ya shares zao maana yake hakuna demand na share zitashuka bei zikiwa listed kwa style hii.